Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  3 Jumada I 1445 Na: 1445 / 05
M.  Ijumaa, 17 Novemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kushiriki kwa Serikali ya Uzbekistan katika Mkutano wa nchi za Kiarabu na Kiislamu uliofanyika jijini Riyadh
(Imetafsiriwa)

Mnamo Novemba 11, mkutano wa kilele wa nchi za Kiarabu na Kiislamu ulifanyika jijini Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, ambapo hali katika Ukanda wa Gaza ilijadiliwa. Waziri Mkuu wa Uzbekistan Abdulla Aripov alishiriki katika mkutano huo. Katika hotuba yake, Aripov hakuenda zaidi ya "kuwataka wahusika kufikia amani ...", ambayo sio tofauti kabisa na mwelekeo wa wasaliti iliotabanniwa na watawala wa nchi zengine. Katika hotuba yake katika mkutano huo, alisema: "Uzbekistan inaunga mkono haki ya watu wa Palestina kuanzisha dola yao huru kulingana na sheria za kimataifa. Maisha yenyewe yanathibitisha kuwa mzozo huu unaweza kutatuliwa tu kwa msingi wa kanuni ya "dola mbili huru kwa watu wawili ... ikiwa vurugu zitaongezeka, itavuruga hali ya kimataifa kwa kiwango kikubwa na kuvutia vikosi vipya katika mizozo ya kisilaha. Yote haya yanaweza kusababisha mikasa isiyotarajiwa, sio fungika tu kwa kanda ya Mashariki ya Kati pekee ... ".

Katika mkutano huu wa uhaini, watawala wa nchi zote za Waislamu walikutana kupata suluhisho la kadhia ya Palestina. Lakini suluhisho hili lazima liwe kwa maslahi ya Kafiri Marekani, na kuhifadhi umbile la Kiyahudi, na sio kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu, na hivyo ndivyo ilivyokuwa ... Mkutano huo ulifanyika baada ya zaidi ya mwezi mmoja wa mauaji ya kikatili Kufanywa na vikosi vya umbile halifu la Kiyahudi kwa watu wa Gaza - watoto wasio na hatia, wanawake na wazee - mbele ya macho ya ulimwengu mzima, na ambayo yanaendelea hadi leo. Kana kwamba wale wanaouawa huko Gaza ni wageni, sio Waislamu! Ukweli ni kwamba hata kabla ya mkutano huu, hali ya watawala wa Kiislamu ilifichuliwa. Badala ya kutangaza uhamasishaji wa kijeshi mara moja kuikomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, wasaliti hawa na waoga hawakufanya chochote isipokuwa wito wa ufunguzi wa ukanda wa kibinadamu, kusitisha mapigano, mazungumzo ya amani, nk. Kama ilivyotarajiwa, hakuna neno moja lililozungumzwa, achilia mbali uamuzi uliochukuliwa kuhusu uhamasishaji wa kijeshi ambao ungeling’oa umbile la Kiyahudi. Kwa kuongezea, mapendekezo ya kukata mahusiano ya kiuchumi na umbile la Kiyahudi, kuweka vikwazo juu yake, na kuzizuia kambi za kijeshi za Marekani katika nchi za Kiarabu kutokana kulisaidia umbile la Kiyahudi yalikataliwa. Kwa hivyo mkutano huo haukuenda zaidi ya taarifa na gumzo tupu.

Kwa bahati mbaya, hotuba ya Waziri Mkuu Abdulla Aripov, ambaye alishiriki katika mkutano huo kama mwakilishi wa Uzbekistan, haikuwa tofauti kabisa na hotuba za watawala wengine. Kama suluhisho la kadhia ya Palestina, Aripov pia alipendekeza mradi wa Marekani wa "dola mbili kwa watu wawili" kuunda serikali huru ya Palestina, ndani ya mipaka ya 1967. Suluhisho hili linamaanisha kukubali kuiachilia ardhi iliyobarikiwa ya Palestina kwa Mayahudi na kutambua uwepo wa umbile la Kiyahudi. Ni wazi kwamba watawala wasaliti, pamoja na Serikali ya Uzbekistan, ni waoga ambao hawawezi kupotoka kutokana na mstari uliochorwa na mabwana zao wa kikoloni huko Magharibi, haswa Marekani. Ukweli kwamba Jumuia ya nchi za Kiarabu na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu ni mashirika wakala na hayana ushawishi katika siasa za kimataifa, hata katika kanda hiyo, umethibitishwa tena.

Kama ilivyo kwa matukio ya sasa huko Gaza, ambayo Aripov alitaja kwa wasiwasi katika hotuba yake na hofu yake ya "uwezekano wa kuvutia vikosi vipya kwenye mzozo," hayakufungika kwa Mashariki ya Kati, kwa kweli, wakati mauaji ya halaiki ndani ya Gaza yalitikisa nchi zote za Waislamu na Ummah waliwataka watawala wahamasishe majeshi. Baada ya kukosekana hata mmoja wa watawala hawa wasaliti kujibu wito huu, Ummah ulianza kukata kuwaomba askari waaminifu katika safu za jeshi. Ukweli ni kwamba kile kinachoihofisha serikali ya Uzbekistan, ambayo iko nyuma ya Waziri Mkuu Aripov, na watawala wote wasaliti katika nchi zote za Waislamu, ni kuibuka kwa wananjeshi waaminifu kutoka miongoni mwa majeshi ya Waislamu ambao watajibu wito wa nusra leo, na kuja Kuisafisha ardhi iliyobarikiwa kutokana na miguu michafu ya Mayahudi, ndugu wa manyani na nguruwe, na kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa, na kisha hatua hii iunganishwe na usimamishwaji wa Dola ya Khilafah, ambayo ni ahadi ya kweli ya Mwenyezi Mungu, na ni waumini wa kweli pekee ndio watakaofurahi ndani yake, na wasaliti wanafiki watatetemeka kwa kuiogopa. Gaza imeugawanya ulimwengu katika sehemu mbili, na kuwaacha wanadamu wote kuchagua kati ya ukafiri na imani. Ni wazi, serikali ya Uzbekistan, kama watawala wote wa nchi za Waislamu, ilishindwa kupita mtihani huu.

Usaliti mkubwa wa "viongozi wa kidini" nchini Uzbekistan pia umefichuliwa katika mtihani huu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambao badala ya kuwasilisha mwelekeo sahihi wa Sharia wa mauaji kwa watu wa Gaza, walijaribu kupotosha umakini wa watu kwa maswala yasiyo msingi.

Matukio katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, Mwenyezi Mungu akipenda, yatatumika kama cheche itakayotoa kasi kubwa kwa kurudi kwa Khilafah. Mwishowe, tukio kubwa la ulimwengu litatokea ambalo litatishia dola za kikafiri za kikoloni na tawala zao vibaraka katika nchi za Waislamu, ambalo ni kusimamishwa kwa dola ya Khilafah kwa njia ya Utume.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ *‏ بِنَصْرِ اللهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu