Afisi ya Habari
Uzbekistan
H. 19 Jumada I 1445 | Na: 1445 / 06 |
M. Jumapili, 03 Disemba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Twamuomboleza Shahidi Mpya ndani ya Magereza ya Uzbekistan
(Imetafsiriwa)
Kwa huzuni na masikitiko makubwa, tunaomboleza kwa Waislamu wa nchi yetu haswa, na kwa Ummah wa Kiislamu kwa jumla, mwanachama mwengine wa Hizb ut Tahrir ambaye amejiunga na safu ya mashahidi wa Hizb na amejiunga na wenza wa juu zaidi. Ndugu yetu, Nigmonov Ayub Khan Ismailovich, mwanachama wa Hizb Ut Tahrir, aliuawa shahidi mnamo Jumamosi, Disemba 2, katika gereza Na. 64/46 katika mji wa Nawai.
Ndugu yetu, Ayub Khan, alizaliwa mnamo Agosti 2, 1975, na yeye ni baba wa watoto watatu. Alitumia miaka 24 ya maisha yake kwa kudhulumiwa ndani ya magereza mbali mbali nchini Uzbekistan na mwishowe akauawa katika eneo hili la ukandamizaji huko Nawai. Swala ya janaza ya kaka yetu iliswaliwa katika Msikiti wa Jame Ali baada ya swala ya Adhuhuri siku iliyofuata.
Inastahiki kutaja kuwa Yusuf, Suleiman, Yunus, na Yaqub Jan, kaka za Ayub Khan, walitumikia karibu miaka 20 ya maisha yao katika hali mbaya na usimamizi mkali chini ya ukandamizaji wa serikali ya Uzbekistan, kwa sababu tu ya imani yao pekee. Hata hivyo, serikali hii ya ukandamizaji haikumuachilia huru Ayub Khan. Alihukumiwa gerezani mnamo 1999 wakati wa kilele cha ukamatwaji wa halaiki ya watu wakati huo. Baada ya kuvumilia aina mbali mbali za mateso, hatimaye aliachiliwa huru kutoka gereza la kifo. Licha ya madai kwamba sababu ya kifo cha Ayub Khan ilikuwa matatizo ya mfumo upumuaji, hatuwezi kusahau kuwa vibaraka wa serikali hii waliwarudisha ndugu zetu wengi, waliogunduliwa na hali kama hizo, kwa familia zao huku miili ikiwa imejaa michubuko, na kulazimisha familia zao kuizika mara moja ili kuzuia sauti zozote za upinzani.
Inajulikana kuwa serikali ya Uzbekistan iliwafunga jela wanachama wa Hizb ut Tahrir wakati wa utawala ukandamizaji na wa mauaji wa Myahudi Karimov. Waliua mamia ya wafungwa, ima wakati wa kuhojiwa au magerezani. Mwenyezi Mungu azikubali shahada zao na aridhike nao! Baada ya kifo cha mtawala mwenye kiu ya damu Karimov mnamo 2016, na wakati wa utawala wa Mirziyoyev, mashababu wengi wa Hizb ut Tahrir waliachiliwa huru, lakini mamia yao wangali wako gerezani hadi leo. Hukumu zao zimerefushwa mara kadhaa, na kwa sababu hiyo, wengi wao watabaki gerezani hadi 2035. Katika miaka ya hivi karibuni, tabia ya "uvamizi" kwa mashababu wetu imerudiwa, na maafisa wa Usalama wa Kitaifa walioambatanishwa kwenye magereza wanapeana maagizo juu ya ni nani anayepaswa kuuwawa kulingana na mpango, wao binafsi wakisimamia utekelezaji wa uhalifu huu. Huku watu hawa wenye kuchukiza wakiondolewa kutoka kwa magereza wakati wa utawala wa Mirziyoyev, wengine wamefunzwa na dhalimu Karimov. Pengine wakandamizaji wamewasahau ndugu zetu gerezani kwa robo ya karne, lakini Ummah na ndugu zao ambao huwaita kamwe hawatawasahau! Tunaikumbusha serikali ya Uzbekistan kuwa itawajibika kwa miili ya wanaume jasiri wa Ummah wa Kiislamu, haswa Mashababu wa Hizb ut Tahrir ambao waliibuka kutoka kwa magereza hayo kama mashahidi, na kwa kuwaweka kizuizini wale ambao wanabaki bila kuachiliwa huru kwao! Hakika, Khilafah itakayosimamishwa itakuhisabuni hivi karibuni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali na yenye uchungu!
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) akukusanye kaka yetu Ayoub Khan na bwana wa mashahidi wote, Hamza bin Abdul Muttwalib, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, na kumuingiza kwenye Firdaus ya juu kabisa ambayo Mwenyezi Mungu amewaahidi wale wanaokufa katika njia yake! Tunamuomba, Subhanahu, kuipa uvumilivu na ustawi familia yake na wapendwa wake. Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwao pamoja na dua zetu za dhati.
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uzbekistan |
Address & Website Tel: |