Jumamosi, 25 Rajab 1446 | 2025/01/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  24 Jumada II 1445 Na: 1445 / 09
M.  Jumamosi, 06 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa nini Vituo Rasmi vya Habari vya Uzbekistan Vinaendelea Kukaa Kimya?!
(Imetafsiriwa)

Karibu saa kumi na mbili asubuhi mnamo siku ya Alhamisi, 04/01/2024, utulivu wa asubuhi ulivurugika kwa takriban familia kumi za Kiislamu katika mji wa Tashkent kutokana na "ziara" ya watu waliokuwa wakigonga milango kwa nguvu! Ukweli ni kwamba watu hao waliokuwa wamevalia sare rasmi na barakoa waliingia kwa nguvu katika nyumba hizi na kufanya upekuzi. Walipitia vitabu vya kidini kimoja baada ya kingine, wakitafuta kitu ndani yake. Walipokosa chochote, waliwachukua wenye nyumba pamoja nao. Badala ya mkuu wa familia, ambaye hakuwepo nyumbani siku hiyo, mwanafamilia mmoja alilazimika kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani bila sababu yoyote. Ni muhimu kuzingatia kwamba wenye nyumba walikuwa vijana wa Kiislamu, wote walikuwa wanachama wa Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa cha Kiislamu, na walikuwa wametumia kati ya miaka 20 hadi 22 ya ujana wao magerezani na waliachiliwa huru katika miaka ya hivi karibuni.

Inashangaza! Kwa kosa gani walipitia dhulma hiyo huku familia zao zikijawa na shangwe na furaha? Wazee katika familia waliumia moyo, nyoyo za kina mama nusura zisimame, na watoto walipiga kelele na kulia kwa hofu?! Watu hawa waliodhulumiwa, ambao hivi majuzi walitoka gerezani baada ya robo karne, wakiwakumbatia watoto na wajukuu zao, mikono yao ilifungwa tena! Wakati rais wa sasa alipowaachilia mamia ya Waislamu waliokuwa wamefungwa kwa miaka mingi kutokana na chuki ya dhalimu wa hapo awali, ilileta furaha kwa vijana na wazee wengi. Lakini tuieleweje operesheni kama hii iliyofanywa na vibaraka wa Wizara ya Mambo ya Ndani, kinyume kabisa na hatua na taarifa za hivi karibuni za Mirziyoyev? Kinachoshangaza zaidi ni kwamba wale waliopekua nyumba zao wangekwenda kule walikoambiwa ikiwa wangeitwa tu kupitia wito. Kwa hivyo kwa nini itumike mandhari ya kutisha kama hii? Kuingiza hofu miongoni mwa watu?! Je, mtaaa na majirani wa familia hizo watawatazamaje vijana hawa?

Mawazo ya awali kuhusu hili ni: Kwanza, kunaweza kuwa na mashinikizo kutoka nje kwa serikali kutoka Urusi na nchi nyingine za makafiri kufuata baadhi ya mapendekezo katika mfumo wa kupambana na ugaidi na itikadi kali. Pili, inaweza kuwa na lengo la kuingiza hofu katika nyoyo za vijana ambao wanazidi kuregea katika Uislamu. Vyenginevyo, kuna haja gani ya "utendaji" wa kutisha kama huu?! Jambo jengine muhimu hapa ni kwamba chaneli rasmi kama Kun.uz na Qalampir.uz, na hata wanablogu, hawajazungumza kuhusu hili! Hii imevutia umakini wa wakaazi wa eneo hilo. Na hatuwezi kusema kwamba walikuwa hawazijui oparesheni hizi kwa sababu hiyo inagongana kabisa na maadili ya uandishi wa habari; inakuwaje waandishi wa habari, ambao mara moja wanagundua ajali ya gari katika eneo la mbali la nchi yetu, wanawezaje kuwa hawajui tukio kama hilo lililotokea katika mji mkuu?

Kwa sababu hiyo, tunatarajia waandike maoni ya kina kuhusu ukamataji wa aina hiyo unaofanywa dhidi ya Waislamu nchini mwetu.

Jambo jengine la kuzingatiwa ni kwamba kiongozi yeyote kamwe hayuko huru na maadui wa ndani, na pengine wapo wale wanaojaribu kuchafua sifa ya mtawala mpya wa nchi, ambayo idadi kubwa ya wakaazi wake ni Waislamu, ili kumchimbia shimo la siri za dhalimu wa zamani! Wanajaribu kumakinisha fikra kwenye vichwa vya Waislamu kwamba “msimamo wa kiongozi huyu kwa Waislamu ni sawa na wa mtangulizi wake”! Muda hakika ndio utakaosema. Lakini tunataka kuamini kwamba kiongozi wa leo wa serikali ana nia ya kutokuwa mrithi wa dhalimu wa jana katika uuaji, ukandamizaji, na uharibifu wa familia, na tunataka akumbuke matokeo mabaya ya ukandamizaji! Lakini ni nani anayejua ikiwa hili ndilo chaguo lake?!

[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُون]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Surat Ash-Shu’ara:227]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu