Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  11 Jumada II 1445 Na: 1445 / 07
M.  Alhamisi, 28 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika Gereza la China
(Imetafsiriwa)

Uhalifu mwingine mpya imeongezwa katika orodha ya ukatili unaofanywa na serikali ya China inayoendesha vita vikali dhidi ya Uislamu na Waislamu. Utawala wa China ulitangaza kifo cha Syed Jahan Muhammad Khanovich Nodirov kutoka Andijan, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, mnamo Novemba 28, 2023. Syed Jahan, ambaye aliuawa shahidi katika gereza moja la Beijing, alikuwa mwanaharakati miongoni mwa ndugu zetu wa Uighur huko Turkestan Mashariki, akilingania kunyanyuliwa kwa neno la Mwenyezi Mungu. Alifungwa na serikali ya China katika msimu wa kiangazi wa mwaka 2000. Hata hivyo, hukumu hiyo ilisomwa baada ya miaka 19, na Syed Jahan alinyimwa uhuru wake kwa miaka 20, bila kuzingatia miaka mingi aliyokaa gerezani. Mkewe Muighur anasalia kuzuizini katika kambi ya mateso, mahali pa ukandamizaji na mateso. Jamaa zake wanasema kwamba Syed Jahan alisalia katika sehemu ya matibabu ya gereza la Beijing katika siku zake za mwisho.

Inafahamika kuwa China ambayo haina tofauti na Mayahudi katika uadui wake dhidi ya Uislamu na Waislamu inajihusisha na vitendo viovu vya ukandamizaji na mauaji ya kikatili dhidi ya Waislamu wa Turkestan Mashariki. Inawaweka mamilioni ya Waislamu katika kambi za uzuizi zinazojulikana kama "shule za ufutaji fikra" na inatumia mbinu za mateso ya kutisha dhidi yao. Leo, China inasubutu tu kuwashambulia Waislamu kwa sababu Waislamu hawana Khalifa ambaye angeweza kutumika kama ngao ya ulinzi. Serikali ya Mirziyoyev nchini Uzbekistan, kwa mfano, haiwalindi wana wa Umma huu; kinyume chake, inafanana na serikali ya China katika kutekeleza jinai dhidi ya Waislamu. Ndio maana utawala wa China unaendelea kufanya jinai za kutisha dhidi ya Waislamu bila ya wasi wasi wowote.

Mwamko wa Uislamu unakuja kupitia ushindi wa Mwenyezi Mungu Peke Yake, na mti huu wa ushindi na utukufu unanyweshwa kwa damu ya ndugu zetu mashahidi, kama Syed Jahan, ambaye alibeba mzigo wa ulinganizi huu wenye changamoto. Mashahidi wamechaguliwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe. Kwa hakika wao ni wateule na waja wa karibu wa Mwenyezi Mungu. Pamoja na kuhuzunishwa na kuondokewa na ndugu yetu Syed Jahan hapa duniani, tunampongeza kwa sababu alifikia mwisho mwema wa maisha, ambao ni Shahada (kuuawa shahidi)! Kama Mwenyezi Mungu anavyosema:

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23].

Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt), amuweke ndugu yetu Syed Jahan pamoja na ndugu zetu mashahidi wengine katika Jannah, miongoni mwa mitume, wakweli, mashahidi, na watu wema, na hawa ni maswahaba wema walioje. Hakika, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) subra na kheri kwa familia yake na jamaa zake. Hakika, Khilafah Rashida, ambayo itarejea hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kwa hakika itawalipizia kisasi ndugu zetu waliodhulumiwa na mashahidi kama Syed Jahan, kutoka kwa serikali ya China na wakoloni wengine wa makafiri.

[وَيَقُولُونَ مَتَى هَذَا الْفَتْحُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ * قُلْ يَوْمَ الْفَتْحِ لَا يَنفَعُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِيمَانُهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ]

“Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli? * Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao hawatapewa muhula.” [As-Sajda:28-29]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

- Picha za Shahidi Syed Jahan Muhammad Khanovich Nodirov kabla na baada ya Shahada yake -

 
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu