Afisi ya Habari
Uzbekistan
H. 12 Rabi' I 1432 | Na: 1432/194 |
M. Jumanne, 15 Februari 2011 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir nchini Indonesia Yakemea Udhalimu wa Watawala wa Uzbekistan
Udhalimu wa dikteta Rais Karimov bado unaendelea. Kiongozi wa Hizb ut Tahrir nchini Uzbekistani alieleza kuwa mapema mwezi wa Februari wanachama wanne wa Hizb ut Tahrir walikufa; wawili katika jela ya Jasliq na mmoja ndani ya Andijan, na mmoja ndani ya Farghana. Ingawa serikali ilidai vifo vyao vilisababishwa na mshituko wa moyo lakini watu wengi waliamini kuwa walikufa kama mashahidi kutokana na mateso ya kikatili yanayotekelezwa na maafisa wa Gereza kama vile vifo vingi vya kabla.
Sio hayo tu, wasimamizi wa gereza la Jaslik pia kwa waliongeza muda wa vifungo kwa wanachama wengine ambao hukumu yao inakaribia kuisha. Mwanachama mmoja, Shukrullah, alipewa miaka kumi na sita zaidi, na mwengine, Shaukat, alipewa mitatu mengine, na wote wawili walihamishwa katika Gereza la wahalifu wa zamani.
Katika magereza mengine kama vile Navoi, wasimamizi wa gereza wameanza kuwapa dawa wafungwa wanachama wa Hizb ut Tahrir na kuwalazimisha wao kuzila mbele ya askari wa gereza. Dawa hizi zina chapa ‘zimetengenezwa Marekani' zimeandikwa juu yake na zinafanana na mkate rangi yake na mfumo wake. Imegunduliwa na wafungwa kuwa yeyote anayekula dawa hizi zaidi ya mara moja huanza kupoteza nguvu na uwezo wa kufikiria siku kwa siku. Kutoka miongoni mwa wafungwa hawa ni wale ambao wamehifadhi Qur’an tukufu, wakati wamekaa gerezani kwa muda mrefu.
Pia imebainika kuwa wafungwa wengi huenda zaidi ya kupoteza nguvu na uwezo wa kufikiria, na kupoteza akili zao. Kisha huhamishwa katika hospitali za serikali.
Kiongozi wa Hizb ut Tahrir nchini Uzbekistan ametafuta kupata pesti ambayo wanaiita "dawa", aidha moja kwa moja au kupitia jamaa wanao wazuru wafungwa. Lakini hawakufaulu, kwa sababu afisa wa gereza humtafiti kila mtu kwa makini anayezuru na anayetoka nje ya gereza.
Kulingana na udhalimu huo hapo juu, Hizb ut Tahrir nchini Indonesia:
1. Inakemea vikali uhalifu wa serikali ya Uzbekistan wanaoufanya dhidi ya watu wake, haswa dhidi ya wanachama wa Hizb ut Tahrir. Kwa kweli ni udhalimu unaoshangaza ambao haupaswi kufanywa na mtawala kwa watu wake kwani jukumu lake msingi ni kuwalinda na kuwapenda watu wake.
2. Inawataka watawala wa Uzbekistan kusitisha udhalimu na kuwawacha huru wanachama wote wa Hizb ut Tahrir kutoka gerezani nchini Uzbekistan. Hizb ut Tahrir Uzbekistan kama Hizb ut Tahrir katika nchi nyingine ni chama cha Kiislamu kinachopambana pasina kutumia msingi wa vurugu. Wanapambana kwa ajili ya mazuri ya nchi hiyo na wanadamu wote ulimwenguni kupitia utabikishaji wa sheria na Khilafah. Kwa hivyo, wanachama wa Hizb ut Tahrir popote walipo hawapaswi kuchangamkiwa na mamlaka kana kwamba wamefanya uhalifu mkubwa. Hakika watawala waovu pekee huwafanyia watu wao ukatili na udhalimu. Hizb ut Tahrir inamuonya Islam Karimov na serikali yake na watawala wote madhalimu kuwa Mwenyezi Mungu atamuhesabu kila dhalimu na udikteta saa hii au baadaye kesho Akhera.
3. Hizb ut Tahrir nchini Uzbekistan na popote katika nchi zote wako katika msaada wa Mwenyezi Mungu aliyetukuka hawatakuwa dhaifu dhidi ya udhalimu. Watabakia thabiti kwenye haki na subira iliyoimarika mpaka nusra ya Mwenyezi Mungu itakapokuja.
[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فِى ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيَوۡمَ يَقُومُ ٱلۡأَشۡهَـٰدُ]
“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watakapo simama Mashahidi.” [Ghafiri: 51]
Muhammad Ismail Yusanto – Msemaji wa Hizb ut Tahrir Indonesia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uzbekistan |
Address & Website Tel: |