Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  13 Rabi' II 1446 Na: 1446 / 03
M.  Jumatano, 16 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuhusu Kesi ya Mahakama ya Rufaa ya Wafungwa wa Zamani wa Kisiasa
(Imetafsiriwa)

Kama tulivyotaja awali, mahakama ya rufaa inaendesha kesi ya wafungwa 15 wa zamani wa kisiasa huko Tashkent. Wanaume kumi na watano kati ya 23 (Mashababu), ambao awali walifungwa miaka 20 kwa fikra na imani zao, walihukumiwa mnamo Julai mwaka huu kifungo cha kuanzia miaka 7 hadi 14, wengi wao walihukumiwa kifungo katika kituo maalum cha uzuizi cha serikali. Mahakama pia iligundua kuwa wengi wao walikuwa warudiaji hatari. Wanaume wanane waliosalia walihukumiwa kifungo cha nyumbani kwa hadi miaka 5. Kulingana na vyanzo vya kuaminika, mahakama ya rufaa, kama kesi zote za awali za mahakama, haifanywi kama kesi halisi, bali ni kesi ya kimaonyesho. Ni muhimu kutaja kwamba kesi hizi kubwa zinafanyika mbali na macho ya umma. Vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, vinavyofuatilia matukio ya Uzbekistan kwa karibu, kwa namna fulani “vilipuuza” tukio hili muhimu sana, lakini havichoki kuripoti miti haramu inayokatwa! Hii ndiyo sababu kazi yao kwa manufaa ya mamlaka za nchi na dola za kikoloni inathibitishwa kwa mara nyengine tena. Lakini wale wanaohukumiwa sio miti, bali watu wenye nyama na damu.

Idadi kadhaa ya Mashababu wamepinga katika Mahakama ya Rufaa, wakithibitisha kuwa majaji wake hata hawazingatii sheria walizotabanni. Hasa, wakati hakimu alipowauliza Mashababu: “Je, munathibitisha ushahidi wenu katika mahakama ya mwanzo?”, wengi wao walijibu kwa kukataa. Nizamov Muradjan alisema kwamba mahakama ilimhukumu kifungo cha miaka 12 jela bila ushahidi wowote, na kwa kuwa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 50, ilikuwa kama kifungo cha maisha jela. Zaidi ya hayo, Shabab mmoja baada ya mwengine walithibitisha kuwa mashtaka dhidi yao ni ya uzushi. Abdullaev Zabibulla pia alilalamika kwamba hukumu isiyo ya haki ilitolewa dhidi yake bila ushahidi wowote halali. Shamsiyev Alimjan alieleza katika chumba cha mahakama kuwa alinyanyaswa wakati akihojiwa, na kwamba hakutoa ushahidi dhidi ya mtu yeyote na wala hakukiri shitaka linalomkabili. Walakini, waendeshaji na wapelelezi wenye haraka walichukua njia chafu ya usaliti na kumtishia binti yake, ambaye kwa sasa anaishi Amerika, hivyo akalazimika kusaini hati waliyomtaka asaini ili ndoa ya binti yake isibatilishwe. Alimjulisha hakimu jina la afisa aliyefanya kitendo hiki na tarehe na saa ya tukio inaweza kupatikana kutoka kwa kamera ya video katika chumba cha uchunguzi. Pia aliongeza kuwa afisa huyo aliahidi kurarua hati iliyotiwa saini kwa shinikizo, lakini hakutimiza ahadi yake. Fazil Bekov Davronbek pia aliambia mahakama kwamba alidhulumiwa kwa njia hiyo hiyo. Mpelelezi alimweleza kuwa asipofanya walichosema walitishia kumleta mtoto wake na kumkamata kwa tuhuma za kuwa na kitu kisicho halali kwenye simu yake na baada ya hapo alinakili maagizo yaliyoandikwa na mpelelezi kwenye karatasi hiyo na kutia saini.

Mashababu waliiambia mahakama kuwa mnamo Julai 4, 2024, wiki moja kabla ya hukumu hiyo kutangazwa, maafisa wa upelelezi walifika gerezani na kutangaza wazi ni nani angenyimwa uhuru wake. Mashababu walijibu kwamba “mahakama itatoa uamuzi”, kisha wakasema kwa ujasiri, “Hapana, tutatoa uamuzi.” Kisha mahakama ilisoma hukumu sawa sawa na walivyosema. Baada ya hapo, swali liliibuliwa mahakamani kuwa ni vipi hukumu hiyo inaweza kuandaliwa ndani ya dakika 30 kwa kesi yenye kurasa zaidi ya 100?! Hivyo, Mashababu walitoa ushahidi mbele ya Mahakama ya Rufaa kwamba walikuwa wamejulishwa juu ya hukumu za kabla ya kesi. Hakimu alipowauliza kuhusu majina ya maafisa hao, walisema hakuna hata mmoja wao aliyeambiwa majina yao tangu mwanzo, na kwamba kama wangewasilishwa basi watakabiliana na maafisa wa idara. Mwishoni mwa mazungumzo hayo, wengi wa Mashababu waliihutubia mahakama na kusema, “Hatuombi msaada wako, lakini tunakuomba ufichue ukweli kulingana na sheria unayotabanni.” Aidha, zaidi ya wanawake 20 wa familia za Mashababu hao waliofikishwa mahakamani, walipeleka malalamiko yao kwa mahakimu hao, wakiwaonya dhidi ya kushiriki bila ya kujua kuwatesa mashababu hao wasio na hatia, wachamungu na wasafi na kuwataka wahukumu kwa hofu ya Mwenyezi Mungu... Bila shaka, haya ni majumuisho mafupi tu ya hukumu za Mahakama ya Rufaa, bila kuchimba kwa maelezo kwa undani.

Kwa yakini tunawaunga mkono ndugu hawa na wanafamilia zao, na kwa mara nyingine tena tunatoa wito kwa utawala wa Uzbekistan, vyombo vyake vya mahakama, majaji wa Mahakama ya Rufaa, waendesha mashtaka wa umma, na, kwa ufupi, wale wote walio katika nyadhifa zinazohusiana na kesi hii, wajizuie kutokana na dhulma. Hamjachelewa, kuna nafasi ya kurekebisha makosa. Kama tulivyotahadharisha hapo awali, udhalimu na unyanyasaji kamwe havimnufaishi dhalimu, lakini dhulma ni giza Siku ya Kiyama! Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَلَا تَحْسَبَنَّ اللهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Surah Ibrahim: 42].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu