Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  23 Rabi' I 1444 Na: HTY- 1444 / 05
M.  Jumatano, 19 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kukamatwa kwa Wabebaji Da’wah kutoka kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir na Mamlaka za Houthi ni Jinai ambayo kwayo watahesabiwa mbele ya Al-Aziz Al-Jabbar
(Imetafsiriwa)

Mnamo Alhamisi, Oktoba 23, 2022, mamlaka za Houthi nchini Morocco zilimkamata Ustadh Muhammad Musaad Al-Warafi (miaka 57), mmoja wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir kutoka Msikiti wa Al-Hikma katika Jimbo la Ibb, baada ya kutoa hotuba ambayo kwayo ilifafanua Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara yake njema pale aliposema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Basi je, wito wa Waislamu wa kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu na ukombozi kutoka katika utumwa wa Magharibi, tawala zake na vibaraka wake, umekuwa ni uhalifu ambao mtendaji wake anastahili kufungwa jela, enyi mnaodai njia ya Qur’an?!

Profesa mashuhuri Muhammad Musaad Al-Warafi anajulikana miongoni mwa watu katika mji wa Ibb kwa wito wake na kazi yake pamoja na Hizb ut Tahrir, na ni miongoni mwa wabeba dawa waliojitolea kwa jambo hili na wanaounganisha usiku na mchana. kufanya kazi ya kuunganisha Umma wa Kiislamu na kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu duniani kwa kurudisha maisha ya Kiislamu licha ya njama za madhalimu, Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

Mheshimiwa Profesa Muhammad Musaad Al-Warafi ni maarufu miongoni mwa watu katika mji wa Ibb kwa ulinganizi wake na kazi yake pamoja na Hizb ut Tahrir, na ni miongoni mwa wabebaji dawa waliojitolea kwa jambo hili na wanaounganisha usiku na mchana kufanya kazi ya kuunganisha Umma wa Kiislamu na kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu ardhini kwa kurudisha maisha kamili ya Kiislamu licha ya njama za madhalimu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf 12:21]. Mamlaka hizo zilikosa maadili na akhlaq yoyote kwa kumtia mbaroni Profesa Muhammad Musaad Al-Warafi katika moja ya Nyumba za Mwenyezi Mungu ambayo asili yake ni kwamba anayeingia humo yuko salama, na pia maradhi, ulemavu na uzee wake hayakumshufaiya kwao, pamoja na hayo alikuwa akipeana ufahamu baada ya swala ya Maghrib kuwaeleza watu rasimu ya katiba ya Dola ya Khilafah.

Ni jambo la aibu, dhambi na la jinai kukamatwa kwa waungaji mkono ulinganizi wa Uislamu, je ni udhuru upi enyi wahalifu, mtakaotoa mtakapokutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu kesho katika siku ambayo mali wala watoto hawatafaidisha?! Kwa kufanya hivi, mumetangaza vita na Mwenyezi Mungu, Dini yake, na wafuasi wa ulinganizi wake!

Hizb ut Tahrir maarufu na sio kuwa haijulikani, mizizi yake iko kwenye kina kirefu na matawi yake yapo kwenye upeo wa macho, na imekuwa ikifanya kazi miongoni na pamoja na Ummah tangu mwaka 1953. Ipo leo katika nchi zaidi ya 40 kote duniani na ina mwelekeo jumuishi kwa ajili ya Dola ijayo ya Kiislamu, uliotokana na thaqafa ya Kiislamu kwa nguvu ya dalili, inawalingania watu wa Yemen na Waislamu wote kushirikiana nayo katika kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema ya Mtume wake (saw), kuachana kuwategemea Makafiri wa Magharibi na kusimamisha chombo cha kisiasa kwa Waislamu wote, ili watu waweze kufurahia maisha ya staha ndani ya kivuli cha uadilifu wa Uislamu, na kwa ridhaa ya Mwenyezi Mungu, na Akhera kupata pepo yenye upana mithili ya mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya watu wema.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu