Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  12 Jumada I 1444 Na: HTY- 1444 / 07
M.  Jumanne, 06 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mfuko wa Fedha wa Kiarabu na Uharibifu wake wa Uchumi wa Yemen kwa Mikopo ya Riba
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumapili, Novemba 27, 2022, serikali ya Maeen Abdul Malik ilitia saini makubaliano na Mfuko wa Fedha wa Kiarabu (AMF) kusaidia mpango wa mageuzi ya kiuchumi, kifedha na kisarafu kwa kiasi cha dolari bilioni moja, kulingana na Shirika la Habari la Yemen. Mpango huo, unaoungwa mkono na Saudi Arabia na Imarati, unahusu kipindi cha 2022 hadi 2025. Katika wiki iliyopita, Aden ilikuwa ni angazo la msaada wa kimataifa usio na kifani, ulioanzishwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kwa kuipa serikali dolari milioni 300 kutoka Haki Maalum za Kutoa Pesa za Mfuko huo, ikifuatiwa na utoaji wa dirham bilioni 1.2 kutoka kwa emirates ya Al Zayed, sawa na dolari milioni 710.332. AMF pia ilitangaza mkopo wa dolari milioni 200 kwa serikali ya Yemen kama sehemu ya makubaliano ambayo mkopo wa dolari bilioni 1 utatolewa kwa serikali huko Aden na AMF. Kwa jumla, serikali ilipata, katika muda wa siku kumi tu, wimbi kubwa la mikopo, inayofikia takriban dolari milioni 833, katika kipindi cha rekodi ambacho hakuna nchi iliyoathirika imewahi kupokea.

Ukopeshaji wa AMF kwa Yemen sio mpya. Makubaliano yalifikiwa kati ya Yemen na Mfuko huo ya kukabidhi kwa Yemen awamu ya pili na ya mwisho ya mkopo uliotiwa saini mwaka 2013 wa kiasi cha dolari milioni 57, ikifuatiwa na makubaliano ya mkopo wa kiasi cha dolari milioni 168 katika mwaka wa 2014. Ni kipi kinacho tofauti kati ya AMF na IMF na Benki ya Dunia?!

Benki ya Dunia ilikuwa imeanza mpango wa kuangamiza uchumi nchini Yemen tangu mwaka 1995 hadi sasa chini ya jina la "mageuzi ya kifedha na kiutawala", ambapo iliondoa ruzuku kwa bidhaa zinazotokana na mafuta na ngano ambayo iliongeza mara dufu maisha ya umaskini na uchochole miongoni mwa watu nchini Yemen, na kubebesha hazina ya umma deni kubwa kutokana na mamia ya utoaji wa bili. Hazina, ambayo ilibainika kutofikia malengo yake ya kuipatia hazina ukwasi wa fedha taslimu. Leo, deni ni kubwa, na kiwango cha ubadilishanaji wa riyal dhidi ya dolari hakikusimama, lakini badala yake kiliendelea kuongezeka kwa kasi, na mfumko wa bei haukupungua, lakini badala yake uliongezeka tena. Inashangaza sana kwamba wale wanasiasa ambao hawakuridhika na kile ambacho Benki ya Dunia na IMF walifanya katika suala la uharibifu, kwamba walileta AMF kukamilisha uharibifu na kuzikabidhi shingo!

Masuluhisho ya matatizo ya kiuchumi ya Yemen na nchi nyinginezo za Kiislamu hayako kupitia kwa vita dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuchukua yale Aliyokataza kuwa ni katazo kali, kama alivyosema (swt):

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبا إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ)

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. * Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.” [Al-Baqara: 278-279]

Bali, ni kupitia kutekeleza sheria ya Kiislamu, ikiwemo mfumo wa kiuchumi katika Uislamu, kwa kuzifanya rasilimali za Bayt al-Mal (Hazina ya Dola) kuwa ni zile ambazo Mwenyezi Mungu (swt) ameziwekea sheria na kuziruhusu; kuanzia zaka ya biashara, pesa, madini, kodi, ushri, ada, ngawira, na rasilimali za fedha za umma kama vile mafuta, gesi, madini, n.k., na kuzitumia katika vipengele alivyoweka sheria, na pia kutatua matatizo mengine ya kisiasa na maisha ya kijamii, siasa za kimataifa, na elimu chini ya Dola ya Khilafah yenye kubeba masuluhisho sahihi na fanisi kwa matatizo yetu na matatizo ya dunia nzima.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu