Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  3 Shawwal 1444 Na: HTY- 1444 / 20
M.  Jumapili, 23 Aprili 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutokana na Kuendelea kwa Mzozo nchini Yemen, Wahanga Wapya Wanaongezwa kwenye Orodha ya Misiba na Huzuni
(Imetafsiriwa)

Siku ya Alhamisi usiku, 29 Ramadhan, 1444 H, watu 78 waliuawa na zaidi ya mia moja kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na kesi za walio mahututi, katika shule ya Bab Al-Yaman katika mji mkuu, Sana'a, wakati wa kusambaza zaka za baadhi ya wafanyibiashara kwa watu. Tukio hili la kutisha linaleta wahasiriwa wapya kwenye orodha ya - wale ambao hawawajibikiwi na utawala wa kihalifu wa kimataifa, dola vibaraka za kikanda, serikali ya kitaaluma ya Aden, au Mahouthi, wafuasi wa Iran akaunti ndogo - wahasiriwa waliowatangulia wakati wa miaka minane ya vita katika pande hizo mbili, kama matokeo ya vita vya muda mrefu kati ya Mahouthi kwa upande mmoja na serikali ya Aden kwa upande mwingine, ambayo ilisababisha tu kuenea kwa kesi za mahitaji, ufukara, magonjwa na uchungaji duni kwa watu mbalimbali. Tukio hili linadhihirisha kutoaminiana kwa watu na Mamlaka ya Zaka ya Mahouthi, licha ya utangazaji mkubwa unaotangazwa na vyombo vyao vya habari na licha ya kufunguliwa kwa afisi katika kurugenzi zote za maeneo yao ya udhibiti, kutokana na tabia yake ya kutumia nje ya vigawanyo vinane vilivyoainishwa katika zakat, na mapendeleo katika usambazaji.

Tangu kuanzishwa kwa Mamlaka Kuu ya Zakat, Mahouthi wamefanya kazi kwa njia mbali mbali za kuhodhi ukusanyaji wa zaka kutoka kwa watu, na mwaka huu walizuia kabisa ugawaji wa zaka au vikapu vya chakula kutoka kwa wafanyibiashara wengine katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao, kuhodhi ugawaji wa zaka na vikapu vya chakula kwa Mamlaka ya Zakat, ambayo waliianzisha mnamo Mei 2018, na Mahouthi walihusisha mkanyagano wa watafutaji zaka na ugavi wake usio na mpangilio nje ya Mamlaka yao Kuu ya Zaka, na waliwakamata wale waliogawanya vikapu vya chakula nje ya mfumo wa Mamlaka ya Zaka.

Ni nani anayehusika na kutokea kwa jambo hili na kupotea kwa roho hizi? Hasa kwa kuwa watu wanawagawia masikini zaka zao wenyewe, hivyo watu kukosa imani nanyi na mamlaka yenu ni juu yenu kwa sababu watu wanakimbilia kwenye dola ya uadilifu inayotawala kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu, hivyo hawaikimbii kwa hofu kwa sababu wanatambua kuwa munaitumia kwa wafuasi wenu pekee. Hamkupata somo kutoka kwa waliokutangulieni, wamiliki wa vyama vinavyokimbilia Uturuki, Qatar na kwengineko, na ambao watu wanakumbuka matendo yao mabaya. Mahdi Al-Mashat aliridhika tu na kutoa rambirambi kwa familia za marehemu, na kuunda kamati ya kuchunguza mazingira ya tukio hilo, ikifuatiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kutoa rambirambi za dhati na pole kwa familia zote za wahasiriwa, na kukwepa kuwajibika kwa matokeo ya tukio hilo, ama kwa serikali ya Aden, wao ni kundi la vibaraka wezi ambao mikono yao ina madoa ya damu ya watu wa nchi hii na ambao wanahusika katika maafa yote haya.

Kinachotakiwa ni kutekelezwa kwa mfumo wa Kiislamu, ikiwemo nidhamu ya kiuchumi, na kutokuiwekea mipaka katika ukusanyaji kiasi kikubwa cha pesa za zaka kwa haki au kwa dhulma, na kuzitumia kwa njia ya Sharia. Na nyinyi hamna uwezo wa hilo! Nyinyi ni kama watawala wengine katika nchi nyengine za Waislamu, wanaotawala chini ya mfumo wa kisekula kwa majina tofauti; ya jamhuri, ya kifalme, au mengineyo, na ni dola yenye ubwana pekee inayoutabikisha Uislamu kikamilifu na bila kupungua ndiyo itakayoweza kutekeleza hukmu za Uislamu katika masuala yote ya maisha kisiasa, kiuchumi, kijamii, sera za kigeni, na mengineyo.

Hivyo basi, Hizb ut Tahrir inafanya kazi ya kusimamisha dola hii dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ili kuukomboa Ummah mzima wa Kiislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu