Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  4 Shawwal 1444 Na: HTY- 1444 / 21
M.  Jumatatu, 24 Aprili 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mamlaka ya Kihouthi Yamkamata Mmoja wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa sababu ya Kauli ya Hukmu ya Sharia kuhusu Zaka!
(Imetafsiriwa)

Mamlaka ya Kihouthi ilimkamata Ndugu Abdullah Ali Al-Qadi kabla ya jua kuzama mnamo Jumanne, tarehe 27 Ramadhan iliyobarikiwa 1444 H, ambapo alitekwa nyara mbele ya nyumba yake katika mji mkuu, Sana'a, katika siku tukufu, kwa shtaka la kutaja hukmu tukufu, "Zakat kati ya mfumo wa Kiislamu na mfumo wa kisekula wa Houthi." Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ] “Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa” [Al-Buruj 85:8]. Inashangaza sana! Je, kauli ya wito wa kutabikishwa Uislamu ikiwemo hukmu ya zaka inachukuliwa kuwa ni jinai?! Je, kuwaita watu wawe wabebaji da’wah na mienge ya uongofu inachukuliwa kuwa ni uhalifu?!

Kukamatwa huku kwa wabeba da’wah ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kunathibitisha kwamba madai ya Mahouthi kwamba wao ni Mwenendo wa Qur’an ni urongo mtupu na ya upotoshaji, wanafuata njia ya waliowatangulia na hawatofautiani nao kwa lolote. Walirithi kutoka kwao dhulma, ukandamizaji na udhalimu kwa kila anayewafundisha watu mema na kuwashauri kuepuka maovu, lakini hawapendi washauri!! Wanapaswa kujifunza kwa wale waliotangulia katika uhalifu na walikuwa mifano mbele ya macho yao. Nasser Mansour Hadi, wakala wa Shirika la Usalama wa Kisiasa huko Aden, Lahj, na Abyan, ambaye alikuwa akitawala juu ya watu kwa chuma, moto, ukandamizaji na mateso akawa mfungwa wao na mfungwa kwa miaka minane katika chombo hicho hicho ambacho kwacho alikuwa akifanya kazi kwa miaka mingi, ambapo aliwahi kuamuru upelelezi na kuwakamata wafuasi watiifu. Kuna tofauti kubwa iliyoje kati ya kukamatwa kwa wale wanaobeba da’wah ya kuutabikisha Uislamu na wale waliokamatwa kwa mengineyo yasiyokuwa hayo, na hivi majuzi Mahouthi wenyewe walikuwa kwenye jela za Ali Saleh aliyeangamizwa, wakionja uchungu wa kifungo, hivyo je kuna yeyote anayekumbuka?!

Mahouthi wamemuasi Mola wetu (swt) na Dini yetu kwa uadui bila aibu wala hofu. Badala ya kutabikisha Shariah ya Mwenyezi Mungu, wanawakamata wale wanaitisha utabikishaji wake. Licha ya utambuzi wao wa ukweli wa Hizb ut-Tahrir, ambao unajulikana kwa kila mtu wa karibu na wa mbali, na kwamba hawatumii vitendo vya kimada ili kufikia lengo lake, yaani kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ambayo itasimamishwa hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda. Hizb inafanya kazi mchana kweupe na historia yake ndefu ni shahidi wa hilo, adui anajua hilo hata kabla ya rafiki kulijua, na katika njia yake haimuachi mtu yeyote bila ya kuwasilisha ulinganizi huu mtukufu kwake, wakiwemo viongozi wa Mamlaka Kuu ya Zaka nchini Yemen. Ujumbe ulikwenda kukutana na Shamsan Abu Nashtan zaidi ya mara moja, lakini afisi yake kila mara ilidaiwa kuwa na shughuli nyingi!

Tunakuhutubieni nyinyi hapa kwa barua ya mwaliko na barua ya ufaradhi kwamba utabikishaji wa Uislamu ni faradhi na nyinyi hamuufanyii kazi, na kwamba wabebaji da’wah hawatanyamaza kimya kwa yeyote atakayefikia madaraka na kutekeleza kinyume na Uislamu. na akautaka kupotoshwa. Hatusemi hivi tukiwa tumeegemea kwenye sofa, bali tuko uwanjani tukifanya kazi na Ummah na tunatayarisha zana kutoka katika mtazamo mpana na kamili wa dola. Tumezieleza na kuzibatilisha katiba za dola zilizopo katika nchi za Kiislamu, kwa mfano tumezikemea katiba za Sudan, Iran, Misri na Yemen, na pia tumeonyesha kuwa mifumo ya kifalme iliyopo leo ni ya kisekula sawa na ile ya serikali ya kisekula ya kijamhuri, na munapaswa kuregelea tovuti za Hizb na Mashababu wake ili kujua njia yake, kwani ni mshauri mwaminifu na kiongozi asiyewadanganya watu wake.

Mnapaswa kujua kwamba vitendo hivi vya ukandamizaji havitawavunja moyo wabeba da'wah kutoendelea na njia yao, huku wakipata thawabu kwa kazi yao, na wafungaji wao wa jela wanathibitisha kwa mara ya elfu moja kwamba wamekuwepo tu, kama watangulizi wao, upanga wa kuwapindua wale wanaolingania utabikishwaji wa Uislamu, basi je mnakubali hili?! Kwa kufanya hivyo, wanazitumikia dola makubwa za kikoloni zinazochukizwa na Uislamu na wabebaji da’wah kwa ajili ya Khilafah inayosimamisha Dini na kukomesha athari za wakoloni, na wakati huo visingizio vyao havitawanufaisha, wala hawatatafuta toba.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ للهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَى أَلَّا تَعْدِلُوا اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى وَاتَّقُوا اللهَ إِنَّ اللهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ]

“Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” [Al-Ma’idah 5:8]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu