Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 13 Shawwal 1444 | Na: HTY- 1444 / 22 |
M. Jumatano, 03 Mei 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Aden Haiwezi Kusimamia dhidi ya Mabwana Zake Walioikabidhi Madaraka ni Dola ya Khilafah Rashida Pekee ndiyo yenye Uwezo wa Kuwalinda Waislamu
(Imetafsiriwa)
Mnamo Ijumaa asubuhi, tarehe 28/4/2023, Askari wa Kikosi cha Ulinzi wa Pwani ya Yemen waliokuwa wakishika doria katika eneo la Ras Fartak na Hasween katika Jimbo la Al-Mahra, mashariki mwa Yemen, walifyatuliwa risasi na meli ya kivita ya Uingereza, na kumuua mwanajeshi mmoja na kuwajeruhi wengine. Baadaye, shughuli za biashara ya baharini za Uingereza zilitangaza kwamba zilizuia shambulizi lililoilenga kutoka kwa watu wasiojulikana, huku kukiwa na kimya cha serikali dhaifu ya Aden, kana kwamba jambo hilo haliwahusu. Huku Serikali ya Wokovu jijini Sana'a ikijiridhisha kwa kukemea tukio hilo na kwa kelele za vyombo vya habari!
Kama kawaida, Waingereza walikuwa na meli yenye sura ya kibiashara iliyokuwa na jina Kalizma, jasusi wa kijeshi iliyobeba silaha kuelekea katika eneo la Jimbo la Al-Mahra. Jibu lake kwa kufyatulia risasi doria ya Walinzi wa Pwani ya Yemen, na kutoitikia wito wa doria hii yenye boti tatu, ikizingatiwa kuwa meli hiyo ni shabaha isiyojulikana ambayo mienendo yake ya kutiliwa shaka ilifuatiliwa usiku wa kuamkia tukio hilo, inaleta kumbukumbu hadithi ya meli ya Darya Dowla iliyokwama kwenye pwani ya Abyan, iliyokuwa ya mwanamke Muislamu wa Kihindi, ambayo Uingereza ilidai umiliki wake, na kuchukua kama kisingizio cha kuikalia Aden mnamo 1839.
Kilichoifanya Uingereza kufanya hivyo ni kudumisha ushawishi wake wa kisiasa tangu wanajeshi wake walipoondoka Aden na viunga vyake mwaka 1967, kupitia kwa wale iliowakabidhi madaraka wakati huo. Leo wanaotawala nchi ndio warithi wa utiifu kutoka kwa watangulizi wao, kama inavyothibitishwa na maagizo ya Waziri wa Ulinzi kwa vikosi vya Walinzi wa Pwani kujiondoa kwenye makabiliano.
Uingereza inajitahidi kudumisha udhibiti wake wa kisiasa juu ya Yemen, kukabiliana na kusogea kwa Amerika, mkoloni mpya. Mzozo wa kikoloni kati yao uliibuka waziwazi juu ya Yemen katika jimbo la Al-Mahra ili kuidhibiti baada ya kuwasili kwa vikosi vya Saudia mnamo 2019, na kazi yake kwa Amerika katika kuikata Al-Mahra nyuma ya bomba la mafuta, jaribio lake la kushirikiana na baadhi ya masheikh na watu mashuhuri, uanzishaji wake wa miradi ya huduma katika jimbo hilo, na usambazaji wake wa uraia wa Saudia kwa wakaazi wa Al-Mahrah, kwa badali ya kazi ile ile ambayo Oman iliruhusiwa kufanya kwa Uingereza katika jimbo la Al-Mahrah tangu 2006. Kuwasili mapema kwa vikosi vya kijeshi vya Uingereza na Amerika kwenye Jimbo la Al-Mahra baada ya Machi 2015, kwa kisingizio cha kupambana na magendo, na kuunda kwao chumba cha operesheni kwenye Uwanja wa Ndege wa Al-Ghaydah mnamo 2022, na kujitahidi kuweka udhibiti wa karibu.
Mvutano wa dola mbili za Kikafiri, Marekani na Uingereza juu ya Yemen, umepelekea nchi hii na watu wake kuangamia. Hili lisingetokea bila ya watawala wanaowakilisha mwenendo duni kwa dola hizi za kikoloni za kishenzi. Watawala hawa vibaraka lazima wafagiliwe mbali na utiifu utolewe kwa khalifa mwadilifu ambaye anasimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu, ambayo iliondolewa kwenye uhalisia wa maisha leo.
Serikali ya pili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ina uwezo wa kuzima mashambulizi dhidi ya Waislamu huko Al-Mahra na nchi nyinginezo, kama ilivyoweza jana kuzuia meli za Uingereza, ikiwemo meli ya "kupaa", kutokana na kusafiri kwenye maji ya Bahari ya Arabia, iliwaondoa mabaharia wake kutoka humo na kuwaonya wasirudi kwenye maji haya. Watu wa Yemen hawana budi ila kufanya kazi na Hizb ut Tahrir ikiwa wanataka mafanikio duniani na Akhera ili kusimamisha dola ya pili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“Kisha itakuwepo Khilafah (Caliphate) kwa njia ya Utume.” [Imepokewa na Ahmad na Al-Tayalisi].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |