Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 18 Jumada I 1445 | Na: HTY- 1445 / 10 |
M. Jumamosi, 02 Disemba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vitendo vya Mahouthi Vinatekelezwa kwa Ufadhili na Idhini ya Utawala wa Marekani!
(Imetafsiriwa)
Tovuti ya Al-Omama iliripoti katika habari zake chipuka mnamo Jumatano, Novemba 29, 2023, taarifa ya msemaji wa eneo wa Wizara ya Kigeni ya Marekani, Samuel Warburg, chini ya kichwa: "Wizara ya Kigeni ya Marekani: Washington Haina nia ya kuweka Vikwazo Vipya juu ya Mahouthi kwa Sababu Moja Pekee. " Katika taarifa hiyo, alisema, "Utawala wa sasa wa Marekani hauna nia ya kuweka vikwazo vipya kwa Mahouthi ili isiathiri watu wa Yemen." Vitendo vya Mahouthi haviikasirishi Washington na hutumikia njama zake.
Taarifa hii kutoka kwa Wizara ya Kigeni ya Marekani inajiri siku mbili baada ya meli yake aina ya destroyer, USS Mason, kulengwa na makombora mawili ya balistiki ilipokuwa ikijibu kujibu wato wa dhiki kutoka kwa Kawanda Kuu la meli hiyo, na watu watano waliokuwa wamepanda meli hiyo katika Ghuba la Aden walikamatwa.
Taarifa hii kutoka Washington inakusudia kuizuia jamii ya kimataifa kuweka vikwazo kwa waasi wa Houthi. Tangu lini Washington imekuwa inajali watu wa Yemen? Ni nyuma ya mzozo unaoendelea huko ili kuanzisha ushawishi wake wa kisiasa kupitia kuwaweka Mahouthi katika nafasi za madaraka, ikibadilisha ushawishi wa kisiasa wa Uingereza. Vyama vya kisiasa vinavyoungwa mkono na Washington, pamoja na chama cha Ali Saleh na chama cha Islah (Mageuzi), vilitumikia maslahi ya Uingereza, kwa kujua au kutojua. Hapo awali Washington ilizuia kuanguka kwa mji wa Hodeidah mikononi mwa Mahouthi chini ya kisingizio cha kuwalinda raia, lakini hawakuchukua msimamo huo huo katika miji ya Marib na Taiz kwa sababu Mahouthi ndio waliokuwa wanawashambulia. Washington haikuzingatia wahasiriwa na waliohamishwa makao yao wakati wa miaka tisa ya vita. Sababu iliyowasilishwa na Washington inaenda sambamba na mipango yake ya kuhalalisha utawala wa Houthi.
Washington imekuwa na hamu ya kuunga mkono Waasi wa Houthi kieneo kupitia Tehran. Hili limeonekana tangu utawala wa George W. Bush mnamo 2001, na kuendelea kupitia utawala wa Obama, Trump, na hadi sasa katika utawala wa Biden. Muegemeo huu na mipango ya Washington inalenga kuchochea mizozo ya kimadhehebu katika Mashariki ya Kati ili kuchorwa upya mipaka ya Marekani. Kwa hivyo, vitendo vya waasi wa Houthi haviikasirishi Washington; badala yake, vinatumikia njama zake.
Kwa upande mwingine, sauti za watu wa kusini, kama vile washirika wa Uingereza kama Hani bin Brik, kutoa wito kwa hija ya kwenda Jerusalem chini ya ulinzi wa Mayahudi, na Aidarous Al-Zubaidi kupigia debe uhalalishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi, zimeongezeka. Hii inafuatia bosi wao Uingereza, ambayo iliwashutumu waasi wa Houthi kwa ukamataji "haramu" wa meli ya Galaxy Leader na ikatoa wito wa kuachiliwa kwake.
Mzozo msingi katika Mashariki ya Kati, ikiwemo Yemen, unatokana na uingiliaji kati wa moja kwa moja wa dola za zamani na za kisasa za kikoloni katika eneo hilo tangu kuanguka kwa Khilafah baada ya kumalizika kwa Vita vya Kwanza vya Dunia. Mzozo huu unaendelea kwa sababu ya kukosekana kwa utawala wa Kiislamu na kugawanywa kwa maeneo yake kwa mujibu wa Makubaliano ya Sykes-Picot, pamoja na uanzishwaji wa umbile la Kiyahudi. Ushawishi unaokinzana wa dola za kikoloni utaondolewa tu kutoka katikati ya ardhi za Waislamu, Mashariki ya Kati, kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Hili ndilo ambalo Hizb ut Tahrir inalifanyia kazi. Enyi watu wa imani na hekima, msishirikiane na upande mmoja wa kikoloni dhidi ya mwingine; badala yake, kuweni na kinu cha Uislamu popote kinapogeuka.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.hizb-ut-tahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |