Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  15 Rajab 1445 Na: 1445 / 18
M.  Jumamosi, 27 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

[وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِنْ أَهْلِهَا]

“Na shahidi aliye kuwa katika jamaa za mwanamke alisema” [Surat Yusuf:26]
Taarifa Zafichua sehemu ya Malengo ya Marekani katika Vita katika Bahari Nyekundu
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatano, Januari 17, 2024, shirika la Bloomberg la Marekani lilifichua kushindwa kwa Washington kufikia mkakati wake unaolenga kuifunga Bahari Nyekundu kwa urambazaji. Shirika hilo lilitaja kuwa takriban meli 114 na meli za mafuta zilivuka Bab el Mandeb mnamo Jumatano iliyopita, siku tano baada ya uvamizi wa majini uliofanywa na vikosi vya kijeshi vya Marekani na Uingereza katika Bahari Nyekundu. Mahouthi walijibu kwa kulenga meli zao za kivita.

Kwa upande mwingine, Dianne Pfundstein Chamberlain, mtaalamu wa sera za kigeni za Marekani na usalama wa kimataifa, aliandika kwenye tovuti ya ‘National Interest’ kuhusu kushindwa kwa vitisho vya Marekani kwa Mahouthi kutozuia meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu. Alidai kuwa Marekani haitaweza kuzuia mashambulizi yao na kuharibu safu yao yote ya makombora na droni kwa kurusha makombora kutumia ndege. Hamu ya Marekani ya kupunguza gharama ya vita inavyoendesha katika Bahari Nyekundu haitafikia malengo yake mbele ya azimio la Mahouthi la kulipiza kisasi. Hii inaleta akilini matokeo ya vita vya miaka tisa vinavyoongozwa na muungano unaoongozwa na Riyadh tangu 2015.

Ushuhuda hizi mbili kutoka kwa vyama vya Marekani, zilizowasilishwa kwa utawala wa sasa wa Marekani na ulimwengu, huzungumza kwa maneno na mistari, kufichua kile wanachoficha baina ya mistari.

Kwa hivyo, miongoni mwa malengo ya Marekani ni kuifunga Bahari Nyekundu kwa ajili ya urambazaji, na kusababisha madhara kwa Ulaya, kuifanya ifuate zaidi utawala wa Marekani na kukubali mipango na ahadi zake za kuanzisha ushirikiano kote duniani kwa njia inayoona inafaa. Sio kulazimisha Cairo na Riyadh kujiunga na Operesheni ‘Prosperity Guardian’ kwa sababu wanafuata maagizo ya Washington kwa khiyari. Pia, kujitoa kwa Uingereza kutoka kwa Muungano wa Ulaya kunaifanya kuwa karibu na Marekani na wateja wake nchini Yemen, na kuhakikisha wao si mawindo rahisi mbele ya lengo la Marekani la kuimarisha washirika wake na kuwaondoa washindani wao.

Mbali na malengo mengine yaliyoainishwa na Wamarekani, ikiwa ni pamoja na kugeuza mawazo ya ulimwengu kutoka kwa kile kinachotokea Gaza na kuimarisha vibaraka wao kaskazini mwa Yemen ili kuonyesha nguvu zao, ndani ya nchi, kikanda na kimataifa. Hii inachangia kufichua zaidi uduni wa vibaraka wa Kiingereza huko kusini na mashariki mwa Yemen.

Enyi Watu wa Yemen: Hizb ut Tahrir imewatahadharisha mara kwa mara kuhusu kushadidi mgogoro wa kikoloni wa Kimagharibi kati ya Marekani na Uingereza ili kuwapa uwezo vibaraka wao katika ardhi ya imani na hekima, ambayo iko umbali wa masafa machache kutoka Makka tukufu na Madina iliyobarikiwa. makaazi ya Mtume wenu (saw). Je, kuna yeyote anayejivunia Dini yake, ainusuru kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kutawala kwa Uislamu, na kuzuia uchokozi wa Wamarekani na Waingereza?

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu