Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Nyinyi ni Ummah Bora

Mwenyezi Mungu (swt) anatuambia katika Quran Sura Aal-Imran:

(كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللّهِ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya Ummah waliotolewa kwa watu. Kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Aal-Imran: 110]

Kwa zaidi ya karne kumi na tatu, Ulimwengu wa Kiislamu ulishughulikia suala hili. Chini ya Khilafah, bay’ah huchukuliwa na Mtawala. Mzozo baina ya watu ulitatuliwa na Maqadhi kwa msingi wa Sharia. Mali ilikusanywa na kusambazwa kwa msingi wa Kharaj na Zakat, na bendera ya Jihad ilibebwa na majeshi ya Kiislamu. Usalama na utukufu sio tu vilitolewa kwa Waislamu, bali pia taasisi zilitoa mwanga kwa wale waliotaka kusoma na kutambua Uislam una lipi la kutoa.

Hivi leo uhalisia na majaribu ya Waislamu yanafahamika na wote na hakuhitajiki maelezo wala ufafanuzi, wala hakuhitajiki mjadala mrefu na wale walio miongoni mwa mabaki ya wakoloni wa Kimagharibi wanaotaka kuleta shaka juu ya Khilafah, uwajibu wake, au uwezo wa Uislamu kutoa uongozi kwa dunia kwa mara nyengine tena.

Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt) yanatosha pale aliposema:

(وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ اللّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءهُمْ)

“Na wahukukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamatamanio yao.” [TMQ Al Ma'idah 5:49].

Je, hautakuwa ni udanganyifu kudai kuwa Mwenyezi Mungu (swt) hakutoa njia ambayo huleta muongozo kwa wanaadamu kuhusu maisha? Au inaruhusiwa kushuhudia karne ambapo mfumo wa Kibepari wa Kisekula ukileta maangamizi kote duniani na sisi kubakia watazamaji tu? Urasilimali ni mfumo ambao urithi wake ni kuwa utajiri mkubwa ubaki kwa wachache kwa gharama ya mizozano, njaa na maradhi kwa waliobakia.

Mjadala pekee wa kweli uliobaki ni namna ambayo Nidhamu ya Kiislamu ya Khilafah inaweza kurejeshwa maishani, kwa kuwa ndio nidhamu pekee ya kweli iwezayo kuwarudisha wanaadamu kutoka katika njia ya kujiangamiza wenyewe ilioko hivi sasa.

Mwenyezi Mungu (swt) ametuletea wakumbushaji wengi ambapo kubadilisha mfumo wa kiulimwengu ni jambo rahisi Kwake. Kwa wale wanaozingingatia uchunguzi, mabadiliko hivi sasa ni yenye kuendelea. Jambo pekee kwetu la kuzingatia ni mchango gani sisi tunahitaji kuutoa katika uhuishaji huu. Tukiwa watazamaji tu, nini tutamjibu Mwenyezi Mungu (swt) wakati Anapotueleza:

(فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ“Na kwa yakini tutawauliza wale waliopelekewa Ujumbe.” [TMQ Al -Araf 7:6].

Tukiwa ni wafuasi wa Mtume wa mwisho (saw), majukumu yetu kwa ujumbe huu una maeneo mengi, ima kwa mama anayewalilia watoto wake waliofukuzwa majumbani mwao, au kwa baba anayepambana kumtoa mtoto wake kutokana na (fikra za) uhuru na utumiaji ambao Ubepari umezibuni. Uislamu umekuja kutatua matatizo ya wanaadamu wote. Hivyo kwa namna gani tunaweza kuridhika kwa Uislamu kuwa ni wenye kuonekana kama ni mjumuiko wa imani za kiroho tu au matendo ya kujaza uwazi wa kiroho.

Kwa hakika, ni kwa kuurejesha tena Mfumo wa Kiislamu wa Khilafah tu ndipo tutapoweza kuishi kwa Uislamu na kuueneza duniani ukiwa ni njia iliokamilika ya maisha. Ni kwa kupitia Khilafah tu Waislamu wanaweza kufurahia kiukweli matukufu na amani ambayo ni yao kwa haki na kwa ajili ya kujiegemeza kwa Mwenyezi Mungu (swt). Ni njia ya maisha ya Uislamu tu inayoweza kuonyeshwa kuwa ni njia mbadala ya kikweli na dawa kwa hali ya kutokuwepo chochote cha maana ilioletwa na mfumo wa kiulimwengu wa kisekula.

Hapana budi kuwa Ummah kwa pamoja uhitajie kile kilicho chake na kufanya kazi bila kuchoka kuleta mabadiliko ambayo hatimaye unayahitajia. Tunapaswa kufahamu kuwa hili ni suala la kufa na kupona, ambalo jukumu lake linamlazimu kila Muislamu.

Mtume (saw) amesema: «وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً “Yeyote anayekufa hali ya kuwa hana bay’ah shingoni mwake amekufa kifo cha kijahiliya.” (Muslim).

Ni jukumu la kila Muislamu kuhakikisha wanafanya kila kitu kilicho chini ya uwezo wao kuufanya wito wa Khilafah kuvuma kiasi cha kuvitingisha viti vya enzi vya madhalimu na kubiruliwa na watu wenye nguvu na ushawishi wanaomuogopa Mwenyezi Mungu (swt) na kutamani kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) aliposema:

 (وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema ya kwamba atawafanya Makhalifah katika ardhi kama alivyowafanya Makhalifah wa kabla yao.”  [TMQ An-Nur 24:55].

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Wali

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu