Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipi Khilafah Itakavyo Kuwa Dola Inayo Ongoza Katika Sayansi na Teknolojia

Mapinduzi ya kiviwanda 4.0 yalitangazwa kama ajenda ya kiulimwengu katika Kongamano la Kiuchumi la Kiulimwengu la mwaka 2016, yaliwasili kama mafuriko makubwa katika biladi nyingi za Waislamu. Kuanzia mapinduzi ya kiviwanda 1.0 ambayo yalijiri katikati mwa karne ya 18 ambapo kuzuka kwa mitambo ya kutumia bukhari yalibadilisha (matumizi ya) wanyama wakati huo na kufanya mabadiliko ya kimsingi, hususan kwa uchumi wa kiulimwengu. Yakaendelea kwa kuja mapinduzi ya kiviwanda 2.0 yaliyojitokeza kwa kuja mitambo ya nguvu za umeme na magari ya utumizi wa nguvu za mafuta. Uvumbuzi huu ulichochea kuzuka kwa simu, magari, ndege, nk. vilivyo badilisha pakubwa sura ya ulimwengu. Katikati mwa miaka ya 80 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 ikawa ndio kudhihiri kwa mapinduzi ya kiviwanda ya tatu, hadi sasa yanapo ingia mapinduzi ya kiviwanda 4.0 ambapo maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano ya tovuti na hata uhodari wa kubuniwa yamekuwa ni kitu ambacho sio ndoto tena.  

Lakini maendeleo yote haya ya kiteknolojia kwa bahati mbaya yanadhibitiwa kikamilifu na wageni ambao msukumo wao mkubwa ni kaida ya kirasilimali, kwa jina KBE (uchumi uliojengwa kwa msingi wa elimu). Ulimwengu wa Kiislamu umekuwa tu ni bidhaa na masoko. Tafiti za vyuo vikuu katika biladi za Waislamu pia zinafanywa kuvitumikia viwanda vya kigeni ambavyo kihakika vinamilikiwa na warasilimali makafiri.  

Matunda ya utafiti daima huenda sambamba na mahitaji ya viwanda yanayo hitaji ubunifu mkubwa. Hivyo, ndio maana kuwa ni vigumu kwa vyuo vikuu katika ulimwengu wa Kiislamu kuweza kupenya na kuingia katika orodha ya vyuo vikuu 100 vya kwanza ulimwenguni kwa kuwa karibu biladi zote za Waislamu zimekuwa zikikabiliwa na KUPOROMOKA KIVIWANDA kwa kiasi kikubwa, huku Wamagharibi wakiwa katika hatua ya maendeleo ya kiviwanda kwa zaidi ya miaka 150 iliyopita. Huku mojawapo ya mambo yanayo hitajika kwa dola kusemwa kuwa inaweza kumudu sayansi na teknolojia ni ikiwa ina uwezo wa kuunda nguvu ya utafiti inayo pelekea utatuzi wa matatizo yanayo kabiliwa na dola hiyo, pamoja na uwezo wa kuunda nidhamu ya viwanda yenye kutekeleza natija za utafiti huo.

Huku kinaya kikiwa, tangu kuvunjwa Khilafah, ulimwengu wa Kiislamu uliridhika kwa kiasi fulani na wadhifa wa “wafanyi kazi” na “watumizi” wa bidhaa nyingi na huduma za teknolojia zinazo nadiwa masokoni, zinazo miminika katika biladi za Waislamu. Makala haya yatajadili jinsi ruwaza ya Uislamu inavyo tekelezwa katika dola ya Khilafah katika kumudu sayansi na teknolojia katika zama za leo za kidijitali. Ruwaza na mpangilio ambao umesahauliwa na Waislamu wenyewe kwa muda mrefu. 

RUWAZA NA MKAKATI WA DOLA YA KHILAFAH

Dhati ya dola katika Uislamu ni kulinda na kudumisha roho, akili, dini, mali, izza, usalama na dola. Hivyo basi, siasa zote za kielimu na kiviwanda zitashirikishwa pamoja ili kupata yale yanayoitwa malego ya sheria (Maqaasid ul-Shari’ah), kama ilivyo fafanuliwa chini:

  1. A. Mkakati katika Kuunda Uwezo wa Dola katika Kuimudu Elimu na Teknolojia

Mkakati wa kwanza umefungamanishwa na uundaji wa nidhamu saidizi tatu (3) zinazo saidia uwezo wa dola wa kumudu elimu ya juu kabisa.

  1. Uundaji wa nidhamu ya elimu yenye maono kuanzia kiwango cha msingi, upili hadi cha elimu ya juu ambapo filosofia na utamaduni wa kisayansi hutafutwa kutoka katika Itikadi ya Kiislamu pekee, hivyo kizazi chenye sifa ya fikra ya uongozi na uaminifu kitazaliwa, kikiwa na ujuzi na nyanja za taaluma tofauti tofauti.
  2. Uundaji wa nidhamu ya utafiti na maendeleo (R&D), ambayo ni uwezo wa kujumuisha utafiti kutoka kwa taasisi za utafiti za dola, vitengo, pamoja na kutoka kwa vyuo vikuu; ambapo zote zinadhibitiwa, kushajiishwa, na kufadhiliwa kikamilifu na dola.
  3. Uundaji wa nidhamu ya mkakati wa kiviwanda inayo milikiwa na kusimamiwa huru na dola na kujengwa kwa msingi wa mahitaji ya kijeshi ya kisasa na ushibishaji wa mahitaji msingi ya watu. Uhuru wa viwanda ikiwemo uwezo wa kudhibiti, kusimamia na kuhakikisha usalama wa mahitaji ya vipengee muhimu vya viwanda, kwa majina: mali ghafi, teknolojia, ujuzi, uhandisi, fedha, uwezo wa kuunda silsila kamili ya kiviwanda, pamoja na sera.

Kuhusu elimu, Khilafah ya Kiislamu pamoja na upande wa siasa zake za kigeni na mkakati wa diplomasia itashirikiana kwa uchangamfu na nchi nyenginezo zisizo maadui. Yaweza kuwa ni katika ubadilishanaji walimu na wajumbe baina ya nchi hizi mbili katika kueneza thaqafa na lugha ya kila mojawapo. Kaida za makubaliano ya kimataifa ya Khilafah katika Elimu ni kama zifuatazo:

1. Khilafah hutabikisha mtaala wa elimu kwa sera maalumu ili kuunda shakhsiya ya Kiislamu (shakhsiyyah Islamiyah)

2. Sheria ya Kiislamu huwezesha amali za ufundishaji na usomaji ndani ya muundo wa kuimarisha elimu inayo nufaisha Ummah na ulimwengu. 

3. Khilafah huenda ikafanya makubaliano ili kuleta walimu na wahadhiri katika nyanja ya sayansi za kiutafiti kutoka ng’ambo kwa sababu mwalimu amefungwa na mtaala wa dola na hapaswi kupotoka kutokana nao.

4. Imeharamishwa kufanya makubaliano ambayo ndani yake yanaruhusu nchi nyenginezo kueneza fikra na mfumo potofu, au kufungua shule za kibinafsi miongoni mwa Ummah wa Kiislamu.

5. Imeharamishwa kujifunga na makubaliano ambayo ndani yake yanaitaka Khilafah kujifunga na mpango wowote ambao hawendi sambamba na sera za elimu ambazo ni lazima zishikiliwe imara.

Kuhusu nidhamu ya kiviwanda, viwanda huelekezwa ili kuweza kutimiza mahitaji yote ya watu, Waislamu na wasio kuwa Waislamu, pia kuweza kukidhi mahitaji nyeti ya Dola, na kuweza kuunda uhuru wa nchi kwa kaida zifuatazo: 

1. Nidhamu za viwanda zenye kuenda juu ya msingi wa nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu katika kaida za uwekezaji na umilikaji. Uislamu umefafanua kuwa baadhi ya rasilimali asili haziwezi kumilikiwa na watu binafsi, wanajeshi, sembuse wageni. Umilikaji ni wa Ummah mzima. Dola inakuwa msimamizi tu ili kutoa manufaa kamili kwa watu.

2. Sekta nyeti ya viwanda ni lazima idhibitiwe na dola, kama vile ukulima, madawa, kawi, usafiri, miundo msingi, na kadhalika. Maendeleo yote ya kiviwanda ni lazima yajengewe muundo huru. Hapapaswi kuwa na fursa hata ndogo itakayo tufanya kuwategemea makafiri, katika teknolojia (kupitia kanuni za utoaji leseni), uchumi (kupitia mikopo au usafirishaji- uagizaji bidhaa) na siasa. وَلَن يَجْعَلَ اللّهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً] ] “… na wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini. (TMQ An Nisa: 141)

3. Viwanda haviko kwa ajili ya usafirishaji bidhaa, isipokuwa wakati huo huo kwa ajili ya mahitaji msingi tofauti tofauti ya watu ni lazima kuagizwe. 

4. Viwanda pia vinajengwa juu ya msingi wa mikakati ya da’wah na jihad, ya kujihami pamoja na kufungua, ya kimwili na isiyo ya kimwili. Viwanda vyote vilivyoko ni lazima viwe na uwezo wa kutoa mahitaji kwa ajili ya jihad vinapo hitajika. Viwanda vya vifaa vizito ambavyo katika wakati wa amani vitatengeza magari moshi au vyombo vya jikoni, wakati wa vita ni lazima viweze kubadilishwa kwa haraka kuwa viwanda vya vifaru na bunduki za otamatiki. 

B. Mkakati katika Kuchukua Elimu kutoka kwa Hadhara nyenginezo

i. Ushirikiano wa kielimu, sayansi, na teknolojia pamoja na Dola za Kikafiri zilizo katika mkataba (Mu’ahid)

Makubaliano katika uwanja wa sayansi na teknolojia yanaruhusiwa kikamilifu, kwa sababu sheria ya Kiislamu inayaruhusu kwa hilo. Hivyo basi, ushirikiano kama huo unaruhusiwa kulingana na aina ya ushirikiano, huku mandhari ya siasa za kimataifa ikiendelea kuzingatiwa.  

ii. Dola Husalimisha Makundi ya Wanasayansi ili Kutafuta Elimu katika Nchi Maalumu.

Ni dola pamoja na upande wake wa kisiasa ndio itakayo yatuma makundi ya wanasayansi ili kusoma ng’ambo kwa ajili ya maslahi ya kistratejia ya Dola ya Khilafah. Hivyo pindi Khalifah alipoona kuwa ili kuboresha jihad dhidi ya dola kuu ya Kirumi yahitaji majeshi imara ya majini, alituma wajumbe wa Ummah wa Kiislamu ili kujifunza mbinu za ujenzi wa meli, usafiri pamoja na unajimu na mwelekeo wa maeneo, unga wa bunduki, na kadhalika. Na kwa haya ni lazima wajifunze kwa China – ambayo ni ya kwanza kujua kuhusu mwelekeo wa maeneo au unga wa bunduki – kisha wakaenda huko, ingawa safari ilikuwa ngumu, na ni lazima wajifunze lugha kadha wa kadha za kigeni.   

iii. Kuwaajiri Wanasayansi wa Kigeni ili Kuufunza Ummah wa Kiislamu

katika hali fulani ya kisiasa, hatua za kijasusi huenda zikachukuliwa, hususan wakati wa kupambana na nchi maadui wa Khilafah ya Kiislamu, kama katika zama za Sultan Muhammad al-Fatih (1453 M) ambapo majaribio yalifanywa kumwacha huru mfungwa Orban, mjuzi, mhandisi, mtengezaji bunduki, kutoka gereza la Kostantiniya. Alifungwa na Mfalme Costantine ili kumzuia kuajiriwa na jeshi la Uthmaniya. Kufupisha hadithi, kwa hatua za umakini Orban aliachwa huru na kuja mbele ya Sultan Al-Fatih. Kisha aliajiriwa kwa mshahara wa juu zaidi ya mara kumi kuliko alipokuwa akifanya kazi mjini Kostantiniya. Hatimaye, bunduki kubwa ilitengezwa, ambayo ilikuwa mpya zaidi kwa wakati ule. 

Kuunda upya izza ya Uislamu inawezekana kufanywa na ulimwengu wa Kiislamu endapo watakuwa na umoja kama hadhara ili iwe “nguvu mpya” katika mandhari ya kisiasa ya kiulimwengu. Ummah wa Kiislamu karibuni utaregea kuongoza hadhara ya kiulimwengu na maendeleo ya kiteknolojia, endapo ubora wa kizazi chao mara moja kitaelekezwa upya kuwa kizazi cha viongozi. Kwa sababu biladi za Waislamu zina nguvu kubwa mno za rasilimali watu na rasilimali za kiasili, ambazo, ikiwa zitaungana chini ya kivuli cha Khilafah, hakuna nchi au taifa litalingana nayo.

Hili kwa yakini linajibu utegemeaji wa Ummah wa Kiislamu juu ya teknolojia kutoka nchi za Magharibi. Siasa za ukiritimba wa elimu zinazo fanywa na Magharibi zitakabiliwa na Ummah wa Kiislamu kwa uhuru na mtazamo imara wa mfumo wao. Na polepole lakini kwa uhakika, msimamo utabadilika. Magharibi ndiyo itakayoitegemea Khilafah ya Kiislamu. InshaAllah.

Wallahu A’lam bi-Suwab

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 10:38

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu