Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jukumu Letu kama Waislamu kwa Majeraha ya Ummah Yanayochuruzika Damu

(Imefasiriwa)

Kiwango cha misiba na maafa yanayowakabili Waislamu kutokana na kukosekana Dola ya Khilafah, ambayo ni yenye kuuhifadhi Uislamu na kuukinga dhidi ya njama za maadui kutoka kwa Waislamu, kimekuwa wazi. Vita vinavyoanzishwa na maadui ni kutoka pande zote; wamehalalisha ukiukaji wa kumwaga damu ya Waislamu na kuwaacha Waislamu bila auni wala msaada.

Hakuna siku inayopita bila majanga mapya na maafa kuwakumba Waislamu, yakijumuisha yale yaliyopita, yakihuzunisha nyoyo, yakisababisha machozi kububujika, kuongeza maumivu na huzuni kubwa na kutonesha vidonda. Hivyo, maumivu yanarudi upya na kuongezeka kasi yake. Je, sisi kama Waislamu tufanye nini juu ya hili?

Waislamu wengi wanasukumwa kwenye programu mpya wanapoona hali za ndugu zao. Baadhi yao hutokwa na machozi wanapoona picha za miili ya Waislamu waliouliwa kule India, na baadhi huwaombea dua wakimbizi kutoka Syria, na baadhi yao hutoa misaada kwa watu wa Palestina, kutokana na huruma yao kwa maafa yanayowakuta, lakini je hili linatosheleza kwa Mwenyezi Mungu (swt)? Je, yule anayeyatenda haya atasalimika na jukumu mbele ya Mwenyezi Mungu, hasa kutokana na hali ya Ummah inayoelekea kubaya zaidi?

Mateso tunayoishi nayo kama Waislamu lazima yatuzindue hisia zetu na yatushajiishe kufanya kazi ya kubadilisha hali halisi ya maumivu na turejee katika nafasi yetu ya kuwa ni Ummah bora uliochaguliwa na Mwenyezi Mungu (swt).

Hisia za muda mfupi hazifikishi kwenye lengo linalotakiwa, hazifikishi kwenye mwisho unaotarajiwa, na hazimridhishi Mwenyezi Mungu (swt) pindi zikibaki pekee bila kuchanganywa na fikra makini na kazi yenye kutoa tija.

Tafakari ya makini kwetu kama Waislamu katika hali yetu na matokeo yake inatupeleka kwenye hitimisho la wazi na ukweli usiopingika kuwa sisi ni Ummah bila kiongozi; mataifa yamekusanyika dhidi yetu, na watawala wetu ni walinzi wa maadui zetu, wanayalinda maslahi yao, na sio yetu. Kile kitachoboresha hali yetu ni kufuata uongozi wa Mtume wetu Mtukufu na kuishika Dini barabara, ambayo huko nyuma ilikuwa ndio chanzo cha nguvu zetu na msingi wa Dola yetu. Hivyo, hali yetu haitotengemaa isipokuwa kwa kupitia kile kilichoiboresha hali ya Waislamu wa mwanzo waliokuwa kabla katika ujinga uliowasonga, zama walipoamka na kuchukizwa nao, na wakabeba fikra ya Uislamu kwa nguvu hadi Mwenyezi Mungu (swt) akawakirimu na wakasimamisha dola Madina ambayo katiba yake inachipuza kutokana na ya sheria za Mwenyezi Mungu.

Tafakari hii ya makini lazima ilenge juu ya suluhisho na tiba; yaani, mtazamo, njia, na mbinu zake ziwe ni za kutuongoza kwenye matokeo tunayoyategemea, ambayo ni kubadilisha hali yetu na kuunda umbo ambalo litatuhifadhi na kutufikisha kwenye maisha ya heshima na yalio bora kwetu.

Kwa matokeo hayo yenye matunda, fikra nyoofu, tutaweza kuwa na maamuzi muhimu kuhusu dori yetu kama Waislamu kuelekea Ummah wetu na hitajio la kufanya kazi kwa nguvu kuunasua kutokana na yale uliyonayo.

Ni muhimu kwetu kutumia fursa ya majanga tunayoyapitia kuamsha moto katika nyoyo zetu ambao utakuwa kichocheo cha kutushajiisha na kuongeza azma yetu. Muda wa maafa ni kipindi kizuri cha kufanya bidii ya kuuweka vyema utambuzi wa Waislamu na kuwafanya wafahamu njia wanayopaswa kuifuata na kueneza thaqafa ya kutoa na kujitolea muhanga kwa ajili ya Dini, na kuwa wao ni wabebaji wa ujumbe wa Mtume baada yake (saw).

Waislamu wote lazima wawe wenye kuwajibika, hata masheikh wakongwe, wavulana na wanawake wakongwe lazima wabebe hamu ya Ummah wao, na kujitahidi kuinusuru Dini yao.

Muislamu anawezaje kuishi raha mustarehe wakati Palestina inavuja damu, wakati Masra ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu inakiukwa utukufu na Mayahudi?!

Maelfu ya Waislamu wanauliwa na kudhalilishwa, Waislamu wa India, Afghanistan, Iraq na Syria wanalilia msaada bila majibu! Qur’an yetu inanajisiwa! Na mambo mengine yanatutoa mvi na kutufanya kama mayatima kwenye karamu ya watu waovu.

Tusipoteze muelekeo wa misiba ya Ummah wetu. Maumivu ndani ya nafsi zetu yatatusukuma kujadidisha ahadi yetu na Mwenyezi Mungu (swt) kila tunapokuwa dhaifu au tunapokumbwa na udhaifu na kukata tamaa. Picha ya kuogofya itakuwepo kwenye akili za ndugu zetu katika kisimamo cha kudhikisha mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Hukumu na kulalamika juu ya uzembe na utelekezaji wetu. Basi ni nani atakayetuokoa na ghadhabu za Mwenyezi Mungu (swt)?!

Mwenyezi Mungu (swt) ameweka wazi biashara itakayotuokoa kutokana na adhabu Yake Siku, hiyo wakati aliposema:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ * تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُون)

“Enyi mlioamini! Nikuonyesheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iliyo chungu? Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.” [As-Saff: 10- 11].

Kinachohitajika kwetu ni kufanya jihad ya nafsi zetu na kugombania kile kilicho cha tunu zaidi na thamani kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu, ili tuokoke, na kwamba hatuna chaguo isipokuwa kujitoa muhanga kwa fedha zetu na sisi wenyewe katika njia ya Haki na kuwa na bidii juu ya njia hiyo licha ya matatizo na ugumu wake, ili tupate sifa za waumini wa kweli watakaotekeleza masharti ya ushindi wa Mwenyezi Mungu na ahadi ya ukhalifa na tamkini baada ya udhaifu na udhalilifu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً)

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifah katika ardhi kama alivyowafanya makhalifah wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [An-Nur: 55].

Kila Muislamu lazima ajihisi kuwa yeye ni miongoni mwa Ummah uliochaguliwa na Mwenyezi Mungu (swt), ukiwa na historia inayobeba kurasa za kupendeza za utukufu na heshima, Ummah wa Quran na Uislamu uliyo mtukufu, Ummah usiostahiki kuvunjwa vipande vipande, udhalilifu na udhaifu uliofikia sasa. Ufunguo wa mwamko bado upo mikononi mwetu, shukran kwa Mwenyezi Mungu (swt). Tunao uwezo wa kuirejesha historia hii ya heshima ili iwe uhalisia wa hakika, na tuna uwezo wa kuhitimisha mateso ya Waislamu pindi tukiungana na kuisimamisha Khilafah itayohifadhi Uislamu na Waislam, ambayo itafukuza njama za wavamizi.

Basi ndugu zetu, njooni kwenye kile chenye utukufu wa dunia hii na Akhera.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Hajar Al-Ya’qoobi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu