Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mabadiliko Yanayokusudiwa
(Imetafsiriwa)

Tangu macheo ya Uislamu, mapambano kati ya Iman na ukafiri yamekuwa makali zaidi. Kwa hakika mapambano baina ya Haki na Batili yalianza na kushadidi tangu Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam, akamfundisha, akamuamrisha, na akamkataza. Kwa hiyo, amri ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake yalikuwa ndio haki, na kila kilichogongana au kuzikaidi ni batili.

Msingi ambao kwao watu wa imani na haki wanaegemea katika mapambano kati ya haki na batili ni ukweli wa ulimwengu, mwanadamu na uhai, na ukweli wa Dini ya Uislamu. Yeyote anayeufanya ukweli huu kuwa ndio msingi wa kufikiri kwake, na akajenga muundo mzuri juu ya hilo, Mwenyezi Mungu atamsaidia kuifikia haki. Wito wa haki unahusika na kubainisha mambo na ukweli jinsi yalivyo, huku wito wa batili unahusika na kuficha ukweli na kuleta uwongo kwao ili kufikiria batili kuwa haki na haki kuwa batili, kama ambavyo unahusika na kuirembesha batili na kuivutia ili ikubaliwe. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

(وَإِذْ زَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ)  

“Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao” [Al-Anfal: 48].

Kama matokeo ya mgongano huu kati ya haki na batili na kwa kile kinachohitajiwa kwa watu wa batili kupotosha ukweli na kuuharibu, njia nyingi za makosa za mabadiliko zinaonekana katika jamii zilizoamini upotovu, upuuzi na uchambuzi, na kufikia hali waliyonayo ya udhaifu na udhalilifu.

Miongoni mwa hadaa za watu wa batili ni yale wanayopendekeza na kuyaonyesha kuwa mabadiliko yako katika:

* Kwenda na kuwafikia Wamagharibi, kutabanni mielekeo yao katika fikra na thaqafa, na kutafuta msaada kutoka kwao ili kupanga mipango na kutoa ushauri, hivyo Wamagharibi wakoloni wanakuwa ndio mfano kwa waliokoloniwa, hasa kutokana na wito unaokua wa msaada wa Umoja wa Mataifa na mashirika yake mbalimbali na kuuonyesha kuwa ndio suluhisho pekee la matatizo yote ya binadamu. Hata hivyo, ukweli uliopo na wa wazi wa historia ya shirika hili tangu kuasisiwa kwake hadi sasa unaonyesha kuwa lilikuwa na lingali ni chombo cha unyanyasaji na ukandamizaji dhidi ya watu wote wanaodhulumiwa, hususan nchi za Kiislamu, kwa kuzipendelea dola kubwa na miradi yao Duniani. Inatosha kwamba lilitoa sehemu kubwa ya Palestina kwa Mayahudi wanyakuzi mnamo 1947, kwa azimio la kimataifa, na kulitambua umbile lao lemavu mnamo 1948.

* Kwa kuanzisha vikundi vinavyofanya kazi za hisani kama vile kujenga mashule na kuwasaidia maskini, mayatima na wahitaji. Ingawaje kazi za hisani ni miongoni mwa zile ambazo Uislamu unahimiza kuzifanya, vitendo hivi havina uhusiano wowote na kufikia mabadiliko yanayokusudiwa katika jamii. Ukweli ulio wazi ni kwamba viwango vya juu vya umaskini, ukosefu wa ajira, ujinga, na watu kujishughulisha na miaka pungufu ambayo inafichua uwongo wa njia hii ya mabadiliko kwetu, haswa kwa kuongezeka kwa idadi ya mashirika haya ya misaada, ambayo yamegeuza baada ya muda kuwa – vyama vyenye kutengeneza faida au vyama vinavyohusishwa na ajenda fisadi za kuwaweka mafukara na maskini katika msururu wa upotofu na mzoroto.

*Kwa kulingania akhlaqi na kumrekebisha mtu binafsi, kwani ijapokuwa wito huo ni kwa ajili ya kheri ambayo Mwenyezi Mungu aliwaamrisha Waislamu wailinganie, lakini miito kama hii haiwezi kuleta mabadiliko katika jamii au hata kuirekebisha, kwa sababu mageuzi ya jamii hutokea kwa kurekebisha fikra na hisia zinazotawala jamii na kurekebisha mfumo unaotabikishwa. Ukweli uliopo na wa wazi wa viwango vya juu vya uhalifu, ufisadi wa kimaadili na kuenea kwa ufuska unadhihirisha hali ya jamii ambazo zakaribia kukosa maadili ya kiakhlaqi, haswa baada ya majaribio makali ya miaka ya hivi karibuni ya kuhalalisha ushoga na mashirika hayo ya kimataifa ambayo hudai kulinda haki za binadamu.

* Kwa ushiriki wa kisiasa, ima kwa kuendesha au kupiga kura katika chaguzi za ubunge, pamoja na fatwa za kutabann uhalisia wa kifisadi kwa madai ya maslahi ya kitaifa, ulazima, kuishi kwa pamoja, amani ya raia, na madai mengine mengi ambayo husaidia kuweka kiraka uhalisia huu potovu kupitia kushiriki na kujihusisha ndani yake, na matokeo yake, kwa mujibu wa ukweli uliopo na ulio wazi, ni kuzorota kwa hali halisi kutoka kuwa mbaya hadi kuwa mbaya zaidi, na bila kufanya hata asilimia ndogo ya mabadiliko ambayo hayatakuja kwa ujio wa mwakilishi bungeni au kwa kurekebisha sheria hapa na kubadilisha mwanasiasa kule.

Miito hii yote ya mabadiliko na mengine ambayo watu wa batili wanailingania inatoka kwenye chimbuko moja, na hayana uhusiano wowote na mabadiliko yanayokusudiwa. Ni miito ya mabadiliko rasmi ndani ya mfumo wa tawala hizi zilizobuniwa na binadamu ambazo zimetawala tangu ukoloni hadi sasa, na hakuna jambo jipya ndani yake si katika misingi inayosimama juu yake wala katika masuluhisho yao. Yanatokana na itikadi yenyewe ya kirasilimali, yaani, itikadi ya kutenganisha dini na maisha, na juu ya masuluhisho yale yale yaliyofeli ambayo yalitekelezwa katika nchi yetu kwa miongo mingi hadi yakatufikisha kwenye ukingo wa shimo.

- Mabadiliko yanayokusudiwa ni kubadilisha hali za sasa zilizopo katika nchi za Kiislamu kutoka kwa tawala za kisekula, fikra na ladha mbovu za Magharibi, na watawala ambao ni vibaraka wa nchi za kikoloni za Kikafiri za Magharibi.

- Mabadiliko yanayokusudiwa ni kuuokoa Umma wa Kiislamu kutokana na hali ya mgawanyiko na udhalilifu uliowekwa juu yake na dola za kikoloni za kikafiri, na kutoka katika hali ya hasara, kutangatanga, na kuwa chini ya zile dola zinazowapiga vita Waislamu.

Mabadiliko yanayokusudiwa ni kurudisha utajiri wa Waislamu kwao badala ya kuporwa na nchi za kikoloni zinazofaidi bidhaa hizi na kuwaacha katika umasikini hohe hahe, wakiteseka chini ya mabilioni ya madeni kwa nchi hizi za kilafi.

Mabadiliko yanayokusudiwa ni kupitia kuhuisha Umma wa Kiislamu kwa msingi wa Uislamu, kukataa kila fikra isiyokuwa ya Kiislamu, na ni kwa kupitia kuondolewa mifumo ya ukafiri na kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume inayotawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na inaunganisha Umma wa Kiislamu na ardhi zake chini ya uongozi wa khalifa mmoja chini ya bendera moja na kubeba ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu.

Haya ndiyo mabadiliko yanayokusudiwa ambayo yanang'oa ushawishi wa makafiri wakoloni, kuanzisha maisha ya staha, na kukomesha machafuko haya ambayo yanaenea katika nchi zote na kuwaangamiza watu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Radio of Hizb ut Tahrir na
Rana Mustafa

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah #EstablishKhilafah
#ReturnTheKhilafah #TurudisheniKhilafah
#KhilafahBringsRealChange #بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي
أقيموا_الخلافة# كيف_تقام_الخلافة#
#YenidenHilafet #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu