Ijumaa, 01 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kusimamishwa kwa Khilafah Rashidah na Dori Yetu

(Imetafsiriwa)

Kuna mijadala mingi kuhusu kusimamishwa kwa Khilafah siku hizi katika Ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi. Kule ambako Khilafah itasimamishwa kwanza, iko Mikononi mwa Mwenyezi Mungu Peke Yake, kwani Yeye Pekee hupeana Nasr (ushindi). Bishara njema za Mtume (saw) zinatoa habari (khabar) juu ya jambo la uwezekano. Ama dori yetu ni kufuata njia ya Utume, kusimamisha Uislamu katika kutawala mambo yetu.

Tangu mtihani wa Gaza ulipoanza, ni dhahiri kwamba Mwenyezi Mungu (swt) anautayarisha ulimwengu kuhusiana na Dini ya Haki. Leo, Ulimwengu mzima wa Kiislamu unazungumza juu ya haja ya kuregea Uislamu, kutabikisha Shariah na kuungana kama Ummah mmoja. Baadhi ya mazungumzo haya yamepanuka hadi kwenye mjadala kuhusu Zama za Mwisho na kurudi kwa Khilafah. Ulimwengu mzima umeathirika pia. Tunaona sauti zinazowaunga mkono Waislamu miongoni mwa watu wenye mawazo ya adilifu katika nchi za Magharibi.

Bishara njema za Mtume (saw) zimesomwa kwa karne nyingi na maulamaa mahiri wasiohesabika. Kama wanafunzi, tunaweza kuona kwamba khabar (habari) hii inawashajiisha Waislamu kufanya matendo mema. Baadhi ya khabar (habari) huja kwa namna ya talab (amri) kutekeleza hukmu maalum, kama vile kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Ndiyo, tunaweza kutofautiana katika tafsiri, lakini licha ya tafsiri zetu, ni lazima tushikamane na amri za Kiislamu kuhusu hali yetu.

Kuhusu kile tunachopaswa kufanya, tunaregea kwenye Sira ya Mtume (saw):

a. Mtume (saw) aliwatayarisha jamaa na marafiki zake katika Dar ul Arqam. Nyumba zetu, familia, marafiki na jamii lazima ziwe mifano ya Dar ul Arqam. Ni lazima wawe vinara wa Dini na mwongozo wake wenye nuru, sehemu za kujifunzia na kuutekeleza Uislamu.

b. Mtume (saw) aliitayarisha jamii kwa ajili ya kuhukumu kwa Uislamu. Alizungumzia sheria zinazotawala mahusiano ya watu, kama vile kuamiliana na watoto wachanga wa kike, maskini, mayatima na udanganyifu katika biashara. Katika zama zetu hizi, ni lazima pia tuhutubie jamii, hadharani, tukishughulikia maovu yake na kuupeana Uislamu kama badali. Kwa hakika, Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume zinatoa mwongozo kamili wa uchumi, sera za kigeni, sera ya elimu na utawala.

c. Mtume (saw) pia aliwatayarisha watu wenye uwezo na nguvu ili kunusuru utawala kwa Uislamu. Yeye (saw) aliwaendea wapiganaji wa makabila na akawataka Nusrah (Msaada wao wa Kimada) kwa ajili ya kusimamisha Uislamu. Makabila ya Yathrib yaliitikia vyema, baada ya makabila mengi kukataa. Kupitia Kiapo cha Pili cha utiifu cha Aqabah, Nusrah ilipanuliwa hadi kuhukumu kwa Uislamu. Yathrib ikawa mamlaka ya Kiislamu kwa jina linalopendwa la Al-Madinah Al-Munawwarah, ambalo lilitoa mwanga mkali kwenye Bara Arabu. Kwa hivyo leo, lazima tuwaandae wana wetu, kaka na baba zetu katika jeshi ili kutoa Nusrah yao pia.

Kuhusu wapi tunapaswa kufanya kazi,

a. Inajulikana kuwa baadhi ya maeneo yanakubalika zaidi na mengine kidogo. Makka ndipo mahali ambapo Dawah kwa ujumbe wa Risaalah ya Mtume (saw) ulitokea kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, ilikuwa pizani kwa ujumbe huo, ikihisi kupendelewa na kufaidika na hali halisi ilivyo. Kinyume chake, Yathrib ilikuwa yeye kuupokea, ikikumbana na mitihani na matatizo mengi. Ulimwengu wa Kiislamu ni mahali pazuri pa kufanya kazi. Umejaa Waislamu wanaopenda Uislamu na wanapenda kujifunza kuhusu Uislamu. Umezama katika shida na kutafuta njia ya kujitoa.

b. Sisi tunaoishi katika Ulimwengu wa Kiislamu tuna ndugu na marafiki wengi. Ni mahali pa kimaumbile kwetu kuanza. Lazima sote tujifunze na sote lazima tufunze. Ni lazima sote tushughulikie jamii na kuwasilisha hukmu za Shariah za kutibu maovu yetu ya kijamii. Ni lazima sote tuwasiliane na jamaa na marafiki zetu katika majeshi.

c. Ndiyo, baadhi yetu tumelazimika kuhama nje ya Ulimwengu wa Kiislamu kutokana na matatizo. Hata hivyo, kama Waislamu walioondoka kwenda Abyssinia, nyoyo na matarajio yetu yanabakia kwa Ulimwengu wa Kiislamu. Sote tuna jamaa na marafiki katika Ulimwengu wa Kiislamu. Tunaweza kuanzisha miundo ya kidijitali ya Dar ul Arqam, kujifunza Uislamu na kufikisha Uislamu. Tunaweza hata kutembelea. Na pengine, baada ya Dua na maandalizi, tunaweza hata kutafuta njia ya kurudi.

Enyi Waislamu!

Ahmed amesimulia kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

Kisha kutakuwa na utawala wa kutenza nguvu, na atakuwepo apendapo Mwenyezi Mungu uwepo kisha Mwenyezi Mungu atauondoa apendapo kuuondoa. Na kisha kutakuwa na Khilafah kwa Njia ya Utume.” Na kisha (saw) akanyamaza. Kauli hii iliyobarikiwa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambayo si chochote isipokuwa Wahyi uliovuviwa na Mwenyezi Mungu (swt), sio tu ni bishara njema kwetu kuhusu kuregea kwa Khilafah kwa Njia ya Utume. Hapana, Hadith hii iliyobarikiwa pia ni habari (khabar) tuifanyie kazi, kwani ni wajibu juu yetu kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Imepita miaka mia tangu kuvunjwa kwa Khilafah enyi Waislamu, basi fanyeni kazi ya kuiregesha!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Ash-Sham ndio Nyumba ya Khilafah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu