Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mafunzo Makubwa Kutoka kwa Abu Ayyub Al-Ansari kwa Waislamu Jumla na Hasa kwa Majeshi ya Waislamu Juu ya Kumbukumbu ya 99!

Katika kumbukumbu ya 99 ya kuvunjwa kwa Khilafah huko Istanbul, ni juu yetu kumkumbuka mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtume (saw), Abu Ayyub Al-Ansari, alikuwa ni miongoni mwa watiaji hamasa wakubwa kwa jeshi la Sultan Fatih kuhakikisha kufikiwa bishara ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika kuiteka Konstantinopoli (ambayo baadaye ikawa Istanbul). Abu Ayyub Al-Ansari alikuwa ni sahaba aliyemnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake hadi kifo chake. Baada ya kutoa bay’ah kwa Mtume (saw) katika Aqaba, alitekeleza ahadi yake hadi kifo chake, sio tu kwa kufikia katika kuikomboa Makkah wala kwa kufikia kifo cha Mtume (saw). Alishiriki takribani katika vita vyote kuanzia Vita vya Badr hadi katika jaribio la jeshi la Waislamu la Kuifungua Konstantinopoli. Kuna mafunzo makubwa kutoka katika maisha yake, hasa katika uthabiti wake katika vita vya mwanzo dhidi ya Konstantinopoli kwa Waislamu jumla na hasa kwa jeshi la Waislamu. Baadhi yake ni:

1) Mbali ya kuwa ni vizito au vyepesi, ni juu ya Waislamu kwa ujumla kubeba da’wah ya Uislamu kwa ulimwengu na kukomboa ardhi zilizovamiwa. Abu Ayyub Al-Ansari alikuwa na umri wa miaka 80 wakati jeshi la Waislamu lilipoizingira Konstantinopoli mwanzoni. Umri wake haukumpunguzia ari kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, akiwa ni mkweli kwa aya ya Mwenyezi Mungu,

(انْفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ)

“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua.” (TMQ 9:41). Wakati umri ikiwa ni moja ya jambo kubwa zaidi lenye kutia uzito katika kusonga mbele kwenye njia ya Mwenyezi Mungu wakati huo huo ugumu, uchache wa idadi ni miongoni mwa mambo mengine.

2) Ni juu yetu kubeba mzigo wa kufanikisha bishara za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kuwa na hima ni sehemu yake bila kuiwacha kwa wengine kama kina Imam Mahdi, licha ya majukumu yetu wenyewe yanayojumuisha kuirejesha tena njia ya maisha ya Kiislamu na kuieneza ulimwenguni.  Abu Ayyub Al Ansari, licha ya umri wake, hakuwaachia wengine kuzikamilisha bishara za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuhusiana na kukombolewa Konstantinopoli. Bali, alishiriki katika msafara wa mwanzo wa kivita wa Konstantinopoli, hadi alipofariki na kuwa shahidi kutokana na maradhi na kulitaka jeshi la Waislamu kumzika jirani na kuta za Konstantinopoli, na kuonesha msimamo wake wa kufanikisha bishara hadi kuwa ni miongoni mwa wale ambao Mtume (saw) aliwatolea bishara ya msamaha kwao. Mtume (saw) alisema:

    «أول جيش من أمتي يغزون مدينة قيصر مغفور لهم» “Litasamehewa jeshi la mwanzo la Ummah wangu litakalopigana katika mji wa Qaysar yaani Konstantinopoli.” (Bukhari)

3) Ni juu ya Waislamu jumla na majeshi ya Waislamu khassa kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake bila kujali ima ushindi umepatikana ama la. Kile kinachotakiwa na shariah ni kwenda sambamba katika kufanikisha majukumu wakati huo huo kuwa na Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu juu ya ushindi. Abu Ayyub Al-Ansari akiwa pamoja na Ansar wengine (ra) hawakuifunga pekee nusra ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) hadi ukombozi umepatikana na Uislamu umekuwa wenye kutawala wakati wa kuikomboa Makkah. Bali, waliendelea na kutoa nusra hadi kifo chao, wakiwa wakweli kwa kauli ya Mwenyezi Mungu (swt),

(مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا)

“Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” (TMQ 33:23)

عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ أَسْلَمَ أَبِي عِمْرَانَ التُّجِيبِيِّ، قَالَ كُنَّا بِمَدِينَةِ الرُّومِ فَأَخْرَجُوا إِلَيْنَا صَفًّا عَظِيمًا مِنَ الرُّومِ فَخَرَجَ إِلَيْهِمْ مِنَ الْمُسْلِمِينَ مِثْلُهُمْ أَوْ أَكْثَرُ وَعَلَى أَهْلِ مِصْرَ عُقْبَةُ بْنُ عَامِرٍ وَعَلَى الْجَمَاعَةِ فَضَالَةُ بْنُ عُبَيْدٍ فَحَمَلَ رَجُلٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ عَلَى صَفِّ الرُّومِ حَتَّى دَخَلَ فِيهِمْ فَصَاحَ النَّاسُ وَقَالُوا سُبْحَانَ اللَّهِ يُلْقِي بِيَدَيْهِ إِلَى التَّهْلُكَةِ فَقَامَ أَبُو أَيُّوبَ الأَنْصَارِيُّ فَقَالَ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّكُمْ تَتَأَوَّلُونَ هَذِهِ الآيَةَ هَذَا التَّأْوِيلَ وَإِنَّمَا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ فِينَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ لَمَّا أَعَزَّ اللَّهُ الإِسْلاَمَ وَكَثُرَ نَاصِرُوهُ فَقَالَ بَعْضُنَا لِبَعْضٍ سِرًّا دُونَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِنَّ أَمْوَالَنَا قَدْ ضَاعَتْ وَإِنَّ اللَّهَ قَدْ أَعَزَّ الإِسْلاَمَ وَكَثُرَ نَاصِرُوهُ فَلَوْ أَقَمْنَا فِي أَمْوَالِنَا فَأَصْلَحْنَا مَا ضَاعَ مِنْهَا ‏.‏ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّهِ صلى الله عليه وسلم يَرُدُّ عَلَيْنَا مَا قُلْنَا‏:‏ ‏﴿‏وَأَنْفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلاَ تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ﴾‏‏ فَكَانَتِ التَّهْلُكَةُ الإِقَامَةَ عَلَى الأَمْوَالِ وَإِصْلاَحَهَا وَتَرَكْنَا الْغَزْوَ فَمَا زَالَ أَبُو أَيُّوبَ شَاخِصًا فِي سَبِيلِ اللَّهِ حَتَّى دُفِنَ بِأَرْضِ الرُّومِ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ.

Ukombozi haukumshawishi kuzuia nusra yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw). Wakati mtu mmoja katika jeshi la Waislamu katika msafara wa mwanzo wa Konstantinopoli alipojitupa mwenyewe ndani ya safu za jeshi la Roma, Waislamu wakapiga mayowe, “SubhanAllah, amejitupa mwenyewe kwenye maangamizi”, wakitolea maelezo kwa aya ya Mwenyezi Mungu: “Msijitie wenyewe kwenye maangamizi” (TMQ: 2:195), Abu Ayyub Al-Ansari akajibu kwa kusema maangamizi ni kuwacha Jihadi na kujiepusha kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw). Abu Ayyub Al-Ansari aliwaambia, “Enyi watu! Mmetoa tafsiri hii kwa ajili ya ayah, wakati ayah hii imeteremshwa kutuhusu sisi, watu katika Ansar, wakati Mwenyezi Mungu ameufanya Uislamu kuwa na nguvu, na kuongezeka wenye kuunusuru. Baadhi yetu kimya kimya tukaambizana, mbali ya uwepo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): “Mali yetu imeangamia, na Mwenyezi Mungu ameutia nguvu Uislamu, na kuongezeka wenye kuunusuru, hivyo ikiwa tunazielekea mali zetu basi kile tulichokipoteza katika hicho kimehuishwa tena kwa ajili yetu.” Hivyo, Mwenyezi Mungu, Mtukufu na Aliye Mkuu, ameteremsha kwa Mtume wake (saw), amekaripia kile tulichokisema: ‘Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, na msijiingize katika maangamizi.’ (TMQ: 2:195). Hivyo maangamizi ni kuielekea mali na kushughulika nayo.” Kukombolewa Makkah hakukumfanya kuacha Jihadi hadi kufikia kwenda Konstantinopoli katika kipindi cha umauti wake ambapo mbegu ya ushindi ilipandwa kwa ajili ya jeshi lililobarikiwa la Sultan Fatih na kuweza kuvunwa miaka 800 baadaye.

Inaweza kutokea kwa Waislamu, hasa wabebaji da’wah, wakati Nusra (ushindi) imecheleweshwa huku wakitumia sehemu au maisha yao yote katika da’wah. Mtu anaweza kuwa na hisia ‘kwa nini tusilenge kwenye shughuli zetu au biashara angalau, ili kujihakikishia riziki zetu?’, au mtu anaweza kufikiria juu ya hasara zake katika shughuli au biashara kwa ajili ya da’wah, au watu wake wa karibu wanaweza kumfanya afikiri juu ya hasara kama hiyo. Inaweza kutokea kwa jeshi la Waislamu khassa kufikiria juu ya matokeo wakati wakimnusuru Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake kuwa ni maangamizi. Mwenyezi Mungu (swt) ameweka wazi yale yote yaliyo maangamizi ambayo ni kuwacha Jihadi baada ya Uislamu kufanywa wenye kutawala chini ya mikono ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw). Maangamizi yetu mabaya yaliyoje, wakati Uislamu umeshindwa kutawala hivi leo, wakati Waislamu kiujumla hufikiria kurudia katika mambo ya kidunia, wakiiwacha da’wah nyuma na hasa majeshi ya Waislamu kufikiria matokeo ya kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kuwacha majukumu yao wakiwa wao ni watu waliomiliki nguvu! 

Hivyo, kuna masomo muhimu kutoka kwa Abu Ayyub Al-Ansari kwa Waislamu kwa ujumla na hasa kwa majeshi ya Waislamu. Miaka 99 imepita tokea kuvunjwa kwa Khilafah, 28 Rajab 1441 H. Ni juu ya Waislamu kufanya kazi bila kuchoka katika kuendeleza mpango wa Khilafah kwa haraka kadri inavyowezekana, kama Abu Ayyub Al-Ansari aliyejaribu kuwa karibu kwa kadri inavyowezekana katika kuikomboa Konstantinopoli kukamilisha bishara za Mtume (saw). Na juu ya majeshi ya Waislam, hasa, kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, katika hali ya kutokuwepo Mtume (saw), kutomuogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu ili kufanikisha bishara zilizobakia ikiwemo ya kutoa Nusra kwa kusimamisha Khilafah.

(لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ)

“Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili wazi wazi, na tukateremsha kitabu pamoja nao na mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anayemnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.” (TMQ 57:25)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammad bin Farooq

#TurudisheniKhilafah

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu