Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Urusi: Tafsiri ya Quran

Ilitambuliwa Tena Kuwa ni Kitabu Cha Misimamo Mikali

Mnamo Agosti 19, Krasnoglinsky, Mahakama ya Wilaya ya Samara ilitangaza kuwa juzuu ya kwanza kati ya juzuu tatu ya toleo la tafsiri ya Quran kwa lugha ya Kirusi ya Abd ar-Rahman al-Saadi kuwa ni yenye misimamo mikali.

Mwendesha mashtaka wa Samara ametaka kupigwa marufuku kwa juzuu ya kwanza na ya tatu ya toleo hilo, pamoja na vitabu kadhaa vya dini hapo Juni 2018. Afisi ya Mashtaka imedokeza kuwa maafisa wa FSB wameviona vitabu hivi vikiwa na vilipuzi katika chumba cha ibada katika Kijiji cha Krasny Pakhar wakati wa upekuzi mwaka 2016 katika kesi inayoitwa “chumba cha Masalafi”.

Uchunguzi wa kimaandishi uliofanywa na Idara ya FSB ya Samara mwezi wa Machi mwaka 2018 imeona katika vitabu “maelezo ya sura ya misimamo mikali inaodhamiria kuchochea chuki, uadui au ugomvi juu ya msingi wa mitazamo ya dini (yenye kuhusiana na makundi “Mayahudi”, “Wakristo”, Wasioamini dini”). Japokuwa, katika maoni ya wanasheria, njia hii inayoitwa uchunguzi inaonekana kama kuwa dondoo nyingi kutoka katika Biblia huweza kirahisi kutambuliwa kuwa zenye misimamo mikali, ambapo kuna maelezo kama hayo kuhusiana na wasio Wakristo, pamoja na kauli kama “haikuja kuleta amani kwenu bali upanga” nk. Yayo hayo yanaweza kusemwa kuhusiana na nususi za uchunguzi, mashtaka na hukumu zenyewe, ambapo kuna maelezo yenye muundo wa msimamo mkali yanayodhamiriwa kuchochea chuki, uadui, ugomvi na hofu kwa msingi wa mitazamo ya usekula (kuhusiana na makundi ya “Waislamu wenye siasa kali” ambao “hawatambui utawala wa sheria za kisekula”. Yayo hayo yanaweza kusemwa kwa kujiamini kuhusu maudhui yote yenye kupinga Uislamu ya vyombo rasmi vya Habari.

Kumbuka kuwa hili sio jaribio la kwanza la kukipiga marufuku kitabu hichi – juzuu tatu. Mwaka 2017, Afisi ya Mashtaka ya Usafiri ya Volga ilipeleka mashtaka mahakamani, kutaka kuvipiga marufuku vitabu sita:

1. Juzuu tatu za Tafsiri ya Quran Tukufu. (Mtunzi – Abd ar-Rahman al-Saadi, iliofasiriwa na E.Quliyev).

2. Mkusanyiko wa maneno na matendo ya Mtume Muhammad (saw) – Sahih al-Bukhari (mukhtasari) iliofasiriwa kutoka lugha ya Kiarabu na A. Nirsch).

3. Bustani za Waja wema [Riyadh as-Salihiin] (Imam an-Nawawi Moscow, 2008)

4.”Bulugh al-Maram. Kufikiwa lengo la ufahamu wa misingi ya Sheria” (Mtunzi – Ibn Hajar al-Asqalani, imefasiriwa kutoka lugha ya kiarabu na E. Quliyev, Moscow, 2008).    

Hata hivyo, mnamo tarehe 7 Agosti 2018, Mahakama ya Laishevsky ya Wilaya ya Tatarstan kwa kuhofia kilio cha ummah - kama inavyoonekana kwa nje - ilikataa dai la Afisi ya Mashtaka ya Usafiri ya Tatarstan kuitambua tafsiri ya Quran Tukufu na mkusanyiko wa hadith sahihi kuwa ni nyenzo zenye misimamo mikali.

Desturi ya kupiga marufuku fasihi ya Kiislamu ncini Urusi chini ya kingizio cha kuwa na kuwa na taarifa zenye misimamo mikali ndani yake, kwa muda mrefu imekuwa ni ya kawaida. Ikumbukwe kuwa orodha ya serikali ya fasihi yenye misimamo mikali kwa kiasi kikubwa inakusanya fasihi ya Kiislamu na daima hujadidiwa kwayo. Hesabu inakwenda kwa maelfu ya nukta katika orodha. Fasihi msingi ya Kiislamu, ambayo ni chanzo cha ufahamu wa Uislamu kwa ujumla, kwa muda mrefu imepigwa marufuku: tafsiri ya Quran, matoleo mbali mbali ya Sera ya Mtume Muhammad (saw), mkusanyiko wa maneno ya Mtume Muhammad (saw), mkusanyiko wa Ibada za Swala, nk.

Wataalamu huru wanaeleza kuwa zaidi ya asilimia 80 ya vitabu vikuu vya Kiislamu, ambavyo Waislamu kote duniani hupata elimu ya dini ya Kiislamu, vimepigwa marufuku Urusi. Marufuku hii ni muendelezo wa “kukaza nati” dhidi ya Waislamu.

Mapambano ya Urusi na Uislamu ni ya kihistoria na ni jambo la karne nyingi nyuma. Napenda kukukumbusha kuwa hasara kama hiyo na hata kubwa zaidi kwa herufi za Watatar na Wabashkir zenye misingi ya herufi za Kilatini (Yanalif) ziliwekwa, na baadaye mwaka 1940 wakati Waislamu walipolazimishwa kutumia herufi za Cyrillic. Matukio haya yamekuwa ni moja ya mambo muhimu katika kuwatenga Watatar na Wabashkir kutokana na fasihi na historia ya Uislamu iliyoandikwa kwa herufi za Kiarabu, na ndio sababu ya kutojua kwao dini na kutengana kwa kizazi kipya na mizizi ya kidini, utamaduni, na kihistoria. Yote haya ni yalikuwa ni sehemu sera ya wakoloni ya kuwaoanisha. Hivi leo tunaona kurejea kwa jamii kubwa ya Waislamu wa Urusi kwenye dini yao, ambapo inawalazimisha watawala kupambana na hali hii kwa namna zote. Hivyo kupigwa marufuku kwa vitabu vya Kiislamu, kuzuliwa kwa kesi za jinai dhidi ya Waislamu wachangamfu wanaolingania Uislamu, propaganda kubwa dhidi ya Uislamu chini ya kauli mbiu ya “kupigana na misimamo mikali na ugaidi”.

Lakini licha ya jitihada zote za jeshi la shetani miongoni mwa majini na wanaadamu, hawakuweza kuzuia mwangaza wa haki na kuwaweka vijana wema wa ummah wetu katika kiza cha ukafiri.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema ukweli huu: 

[يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia”.  [9:32].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shaikhutdin Abdullah

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 06 Septemba 2020 14:24

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu