Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Elimu ya Wanawake wa Kiislamu Inaingizwa Siasa ili Kuidharau Sharia

(Imetafsiriwa)

Januari 2023 inakamilisha mwaka mmoja tangu kupigwa marufuku kwa wanawake wa Kiislamu kuhudhuria Vyuo Vikuu katika eneo la Udupi nchini India. Masaibu ya elimu kwa wanawake wa Kiislamu katika ulimwengu wa kisasa, baada ya zama za Khilafah ambayo yamejirudia katika kipindi chote cha historia. Hizi hapa ni baadhi ya nukta muhimu:

Mnamo Januari 2023, utawala wa Taliban nchini Afghanistan ulipiga marufuku wanawake kuvaa burka na kuwakataza kupata elimu.

Mnamo mwaka wa 2019, serikali ya Denmark ilipitisha sheria ya kupiga marufuku uvaaji wa hijab katika maeneo ya umma, pamoja na burka na niqab.

Mnamo 2011, serikali ya Ufaransa ilipiga marufuku uvaaji wa hijab, pamoja na burka na niqab, katika maeneo ya umma. Sheria hii iliidhinishwa na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu mwaka wa 2014.

Mnamo 2010, Ubelgiji ilipitisha sheria kama hiyo, pia kupiga marufuku uvaaji niqab katika maeneo ya umma.

Miundo isiyo thabiti ya kijamii imesababisha kuvurugika kwa elimu ya wanawake na wasichana wa Kiislamu, mifano mashuhuri ni pamoja na;

Nigeria: Boko Haram, kundi la itikadi kali nchini Nigeria, limelenga shule na wanafunzi, hasa wasichana, kwa mashambulizi ya mabomu na utekaji nyara. Kutokana na hali hiyo, wasichana wengi katika eneo hilo wamenyimwa fursa ya kupata elimu.

Syria na Iraq: Vita vinavyoendelea na kukosekana kwa utulivu vimesababisha uharibifu wa shule nyingi na mamilioni ya watu kuhama makaazi yao, na hivyo kufanya kuwa vigumu kwa watoto, wakiwemo wasichana, kupata elimu.

Yemen: Mzozo wa sasa wa Yemen na njaa kubwa imesababisha watu wengi kuhama makaazi yao na uharibifu wa miundombinu, ikiwemo shule, na kusababisha ugumu kwa watoto, wakiwemo wasichana, kupata elimu.

‘Israel’ ina sera ya kibaguzi inayotenganisha wanawake wa Kiislamu na wanafunzi wa Kiyahudi katika mfumo wa elimu. Mfumo wa elimu wa Palestina ni duni zaidi na umevurugwa zaidi na vita na mamlaka zinazowaua, kuwaweka kizuizini na kuwateka nyara raia wa Kiislamu wapendavyo.

Hijabu, au kitambaa cha kichwa cha Kiislamu, ilipigwa marufuku nchini Iran mwaka wa 1936 chini ya utawala wa Reza Shah Pahlavi, mwanzilishi wa utawala wa nasaba ya Pahlavi. Reza Shah, ambaye alikuwa kiongozi wa kisekula, alitaka kuifanya Iran kuwa ya kisasa na kuiweka nchi mbali na mila zake za kidini. Kama sehemu ya juhudi hizo, alitekeleza sera zilizolenga kukandamiza mila na desturi za Kiislamu, ikiwemo kuvaa hijabu. Wanawake pia walitakiwa kuvaa mavazi ya Kimagharibi na walikatazwa kuvaa mavazi ya kitamaduni.

Marufuku hii ilianza kutumika hadi Mapinduzi ya Iran mwaka 1979, ambayo yalipelekea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuregeshwa kwa mila na desturi za jadi za Kiislamu. Baada ya mapinduzi, uvaaji wa hijab ukawa ni lazima nchini Iran, na wanawake ambao hawakufuata kanuni za mavazi wanaweza kukabiliwa na faini, kifungo, au adhabu zengine.

Mawimbi ya mzunguko wa mizozo ya kisiasa yanaendelea hadi leo huku wanawake nchini Iran wakipinga uvaaji wa lazima wa hijab.

Mnamo Disemba 2021, Chuo cha Serikali cha Awali kabla ya Chuo Kikuu, huko Udupi, kilipiga marufuku wanafunzi Waislamu kuvaa hijab ndani ya darasa. Wanafunzi sita walipinga hatua hii. Utawala ulikataa kubadili sheria yake mpya, na kusababisha maandamano zaidi kutoka kwa wanafunzi Waislamu. Baadaye, mnamo Januari, mamia ya wanafunzi wa Kibaniani walifika katika vyuo vyao wakiwa na mitandio ya zafarani shingoni mwao, wakitaka wanafunzi wenye hijab wakataliwe kuingia katika vyuo vikuu. Walisema kuwa hijab ilikiuka sheria za taasisi zao kuhusu sare. Watu wengi wenye itikadi kali za mrengo wa kulia waliwanyanyasa na kuwahangaisha wanawake wa Kiislamu kwa kujitokeza madarasani wakiwa na mavazi ya Kiislamu. Walimu na wahadhiri hawakuwa tofauti katika kuwatisha kina dada.

Video kadhaa ziliibuka kwenye mitandao ya kijamii za wanafunzi wa kike wa Kiislamu wakizuiliwa kwenye lango la chuo, wakilazimishwa kuvua vazi lao la burka na hijab nje, wakidhalilishwa na walimu na makundi ya wanafunzi wa mrengo wa kulia. Katika baadhi ya matukio, wanawake wa Kiislamu walikuwa wakirudishwa nyumbani ikiwa walikataa kuvua hijab zao.

Mnamo Februari 5, 2022, serikali ya Karnataka ilitoa agizo ikisema kwamba vyuo vinapaswa kuzingatia sheria za sare na kwamba hakuna mapendeleo yatakayofanywa kwa hijab.

Mashirika kadhaa ya Kiislamu na wanafunzi waliwasilisha maombi dhidi ya amri hii. Mnamo Februari 10, 2022, Mahakama Kuu ya Karnataka ilitoa amri ya muda ya kuwazuia wanafunzi kuvaa "shali za zafarani, skafu, hijab, bendera za kidini au mithili ya hizo ndani ya madarasa".

Machi 2022, wakati Mahakama Kuu ya Karnataka ilipotoa uamuzi katika suala hilo, ikiafiki haki za vyuo kuwakataza wanafunzi kuvaa hijab - vyuo vingi katika jimbo zima vilianza kutekeleza marufuku ya hijab, katika kile ambacho kilianza kujulikana kama "marufuku ya hijab." Mahakama ilisema, "Wakataji rufaa wameshindwa kwa kiasi kikubwa kutimiza matakwa ya kizingiti cha maombi na uthibitisho kwamba kuvaa hijab ni desturi ya kidini isiyoweza kukiukwa katika Uislamu na sio sehemu ya 'amali muhimu ya kidini'."

Mahakama pia ilidai kwamba maagizo ya kanuni za mavazi yatakuwa ni "hatua katika mwelekeo wa ukombozi". Hukumu hiyo ilisomeka, "Ni vigumu kueleza kwamba hii hainyang'anyi uhuru wa wanawake au haki yao ya elimu kwa kadri wanavyoweza kuvaa mavazi yoyote wanayopenda nje ya darasa." Walalamikaji walikata rufaa kwa Mahakama ya Upeo mnamo Oktoba 2022, benchi la majaji wawili lilitoa uamuzi wa mgawanyiko, baada ya kesi hiyo kupelekwa kwa Jaji Mkuu wa India. Kwa ufanisi, tangu wakati wa uamuzi wa mahakama ya upeo hadi sasa, wakati walalamishi wakisubiri katiba ya benchi jipya kusikiliza suala hilo, marufuku ya hijabu imebakia.

Tunachokiona hapa ni uingizaji siasa za kimataifa kwa Sharia kwamba inawakandamiza wanawake wa Kiislamu, na hata katika yale mataifa yanayojiita ya kidemokrasia ambayo yanatafuta "kuwaokoa" na "kuwalinda" wanawake dhidi ya sharia, wanakataa hiari ya wanawake wanaochagua. hijab.

Hijab au mtandio wa kichwa sio ukiukaji halisi hapa. Hebu na tuwe wazi; kosa kubwa ni kwamba wanawake wanakubali kuishi maisha ambapo wanachagua kuupa kisogo “uhuru’ wa thaqafa huria. Changamoto hii ya wazi ndiyo inayofichua upungufu wa maadili ya kisekula. Mifumo iliyopo haiwezi kukidhi mahitaji ya wanawake. Hii inajenga ukosefu wa usalama katika miundo ya kipote cha wachache ya dunia. Tishio halisi ni upinzani wa kijamii na kisiasa na kukiri kwamba kunaweza kuwa na njia mbadala ya utawala wa kibepari.

Mwandishi wa habari Johanna Deeksha amenukuliwa katika makala ya Januari 11, 2023, akisema; “Wakati Waislamu kote nchini India kwa muda mrefu wamekuwa na upataji mdogo wa elimu, wale wa Karnataka wamejitahidi sana kwa ajili yake. Utafiti wa serikali uliotolewa mwaka wa 2013 uligundua kuwa kati ya majimbo yote, Karnataka ilikuwa na kiwango cha juu zaidi cha wanafunzi wa shule wa Kiislamu kuacha shule kati ya darasa la 1 na 8, kwa asilimia 6.3. Utafiti huo pia uligundua kuwa kati ya wanafunzi wote Waislamu nchini India katika hatua ya juu ya shule ya msingi ambao waliacha shule mwaka huo, 73.9% walikuwa kutoka Karnataka.”

Kinachoweza kusomwa kutokana na mitindo hii tofauti inayotia hatiani na kukemea kanuni za mavazi za wanawake wa Kiislamu ni kwamba katika hali zote, mada kuu ni "Uislamu ndiye adui".

Iwapo waliberali wanakemea kujitolea kwa wanawake wa Kiislamu kwa Mwenyezi Mungu (swt), wanawatenga na kuwaadhibu wanawake wa Kiislamu sawasawa na Taliban au Boko Haram. Mfumo pekee ambao kwa dhati kabisa utawapa wanawake haki ni Sheria za Kiislamu, jambo ambalo viongozi wa Magharibi wanataka kuweka kikomo kutokana na usambazaji wa habari kwa kutumia mbinu za uzushi na kupotosha ufahamu wa vitisho halisi kwa wanadamu.

[إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْهِمْ ءَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ * خَتَمَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ وَعَلَىٰٓ أَبْصَـٰرِهِمْ غِشَـٰوَةٌۭ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌۭ * وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ * يُخَـٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ * فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌۭ فَزَادَهُمُ ٱللَّهُ مَرَضًۭا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْذِبُونَ]

“Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawaamini. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini. Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo.” [Al-Baqara: 6-10]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu