Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kutokomeza Giza la Demokrasia

(Imetafsiriwa)

[إِنِ الْحُكْمُ إِلاَّ لِلّهِ أَمَرَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لاَ يَعْلَمُونَ]

Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu.” [12:40]

Katika Uislamu, rai ya walio wengi haizingatiwi kuhusu uamuzi wa Mola Mlezi wa walimwengu wote, na kwamba sheria inapaswa kuwa ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee. Hivyo, katika mfumo wa Kiislamu neno la mwisho kabisa ni la Mwenyezi Mungu (swt). Amri, katazo, kuruhusu na kukataza ni kwa yule Aliye Juu zaidi, Mtukufu, Mjuzi, Muelewa na si kwa kiumbe chochote. Hakuna mtu au kundi lenye hisa hata kidogo katika sheria isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt).

Mwenyezi Mungu (swt) ndiye pekee anayetoa hukumu; [إِنِ الْحُكْمُ إِلاَّ لِلّهِ] Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu.” [12:40].

Tunachoshuhudia hata hivyo leo ni utawala wa kimataifa wa demokrasia ambao msingi wake ni fikra pinzani ya, 'hukmu ya watu, inayo endeshwa na watu na kwa ajili ya watu'. Kihistoria, Magharibi ndiyo iliyoanzisha fikra ya 'kutenganisha dini na maisha'. Demokrasia kama fikra na mfumo iliwafanya wanadamu kuwa bwana juu ya wao wenyewe badala ya kuufanya ubwana huo kuwa kwa Mwenyezi Mungu (swt). Akili badala yake ilikuwa na uhuru wa kuhukumu mambo ya maisha na watu binafsi walikuwa huru kufuata matakwa na matamanio yao kwa jina la maadili ya kiliberali ya kisekula. Uhuru wa imani, kumiliki, rai na uhuru wa kibinafsi unachukuliwa kuwa mtakatifu katika jamii za kidemokrasia.

Walakini, tunapozingatia utabikishwaji wa kivitendo wa fikra ya uhuru katika jamii kote ulimwenguni, tunaweza kuona giza jingi na kukata tamaa. Pindi mtu anapoangalia matokeo mabaya ya fikra ya uhuru wa kumiliki uliosababisha uharibifu mkubwa wa Ubepari, tunaweza tu kuona taabu, umaskini, unyonyaji, ukoloni, vita na ukiritimba unaozalishwa na mashirika tapeli ya kimataifa ya kibepari, nchi za kibepari na kipote cha mabepari.

Nchi za kibepari kama Amerika kihistoria zimeweka maslahi ya tabaka la Mabepari mbele na katikati, hata wakati kwa mfano wa kuandaa katiba ya kidemokrasia ya Marekani. Kwa maneno, ya Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter ambaye alisema, “Sababu ya Katiba ilikuwa kuwawezesha watu kwa mali juu ya watu wa kawaida. Hakika, ufafanuzi wetu wa serikali ya kujitawala wenyewe na uhuru vimeunganishwa, kama sio kufanywa sawa, na maslahi ya mashirika.”

Maneno haya kwa yakini yalisikika kwa sauti kubwa na wazi wakati wa janga la kimataifa la Covid-19 ambapo mabilionea waliuona utajiri wao ukiongezeka kwa muda wa miezi 24 kama walivyofanya katika miaka 23, kulingana na ripoti ya Oxfam ya “Kufaidika kutokana na Maumivu" iliyotolewa Mei 2022. Kila baada ya masaa 30, wakati COVID-19 na kupanda kwa bei ya vyakula vikisukuma karibu watu milioni moja zaidi katika umaskini uliokithiri, uchumi wa dunia pia ulizalisha bilionea mwengine mpya.”

Uislamu una falsafa tofauti kabisa ya uchumi ambayo matokeo yake ni jamii tofauti kabisa na ile ya Kibepari. Sera ya kiuchumi katika Uislamu au mwelekeo wa jumla wa mfumo wa uchumi wa Kiislamu ni kupata ushibishaji wa mahitaji yote ya kimsingi kwa kila mtu kikamilifu, na kuwawezesha kukidhi mahitaji yao ya ziada kadiri inavyowezekana. Hii ina maana sera za kiuchumi zitaangalia kuhudumia wote badala ya kuliachia sokoni pekee. Uislamu pia umefafanua jinsi wanadamu wanavyopata mali ili kuzuia watu wachache kutawala mali nyingi ili watu wengi wasinyimwe kukidhi baadhi ya mahitaji yao. Kupitia qiyas (uvuaji wa kimlinganisho) aya ifuatayo katika Qur’an inahakikisha hali hii kamwe haitokei:

[كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاء مِنكُمْ]

ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.[Al-Hashr: 7].

Ama kuhusu fikra ya uhuru wa kibinafsi, imezigeuza jamii katika nchi za kidemokrasia kuwa jamii za kinyama zilizo poromoka. Uhuru wa kibinafsi ni uhuru wa kuondoa vikwazo vyote. Mwenyezi Mungu (swt) amesema Kweli aliposema (swt):

[أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا * أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا]

Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe utakuwa ni wakili wake? Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao hawakuwa ila ni kama nyama hoa tu, bali wao wamepotea zaidi njia”. [Al-Furqan: 43-44].

Giza la mifumo iliyotungwa na mwanadamu kama vile demokrasia huria na ubepari imefanya maisha kuwa jehanamu isiyoweza kuvumilika kwa wanadamu. Mwanadamu ana kikomo na hana uwezo wa kutunga sheria kwa mafanikio kwa ajili yake na wengine. Ustawi wa kweli, utulivu, na maisha ya kuridhika yatapatikana tu kwa kuzingatia utekelezaji kamili wa mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Uislamu ndio mfumo pekee wenye uwezo wa kutatua matatizo ya watu kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiafya, unaotekelezwa ndani ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo inajenga taasisi zake, vyombo, nidhamu na katiba zake zote juu ya hukmu za Sharia zinazochipuza kutokana na Aqidah (itikadi) ya Kiislamu ambayo ni itikadi ya Ummah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Tsuroyya Amal Yasna
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara Zifuatazao za Kampeni:

#Time4Khilafah  #EstablishKhilafah 
 #ReturnTheKhilafah  #RealChange
 #KhilafahBringsRealChange  #بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي
 أقيموا_الخلافة#  كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

  #HakikiDeğişimHilafetle
 #TurudisheniKhilafah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu