Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wanawake wa Kiislamu nchini Iraq walio katika Mgomo wa Njaa Hawana Msaidizi Chini ya Sheria za Kibepari za Kiliberali

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 6 Mei 2023, BBC iliripoti kuwa mamia ya wanawake wamegoma kula katika gereza moja la Iraq katika mji mkuu wa Baghdad. Wanapinga kuzuiliwa kwao kwa kuwa sehemu ya kundi la Dola ya Kiislamu, baada ya kile wanachosema kuwa ni kesi zisizo za haki. Kundi hilo linasemekana kujumuisha raia wa kigeni kutoka Urusi, Uturuki, Azerbaijan, Ukraine, Syria, Ufaransa, Ujerumani na Marekani. "Inafikiriwa kuwa takriban watoto 100 pia wanazuiliwa katika kituo hicho".

Hofu za ile iliyokuwa Iraq zinazidi kuwa mbaya zaidi kwa wanawake na watoto katika eneo hilo. Mshtuko usio na kifani ambao ni lazima upitiwe na mtoto aliyefungwa gerezani ni jinamizi la kutisha. Kwa bahati mbaya, kwa sera za kikoloni za Kibepari kutawala ardhi zetu, hakuna njia ya kumaliza uhalisia huu wa kikatili. Wanawake na watoto wanatumiwa kama mifano ya kuwaadhibu na kuwafundisha Waislamu wengine kwamba kutakuwa na adhabu kubwa kwa wale watakao jaribu kupinga utawala wa Magharibi.

Hakuna Dola ya Kiislamu popote pale duniani. Ni ukweli ambao Magharibi inaujua waziwazi. Yale yanayotokea kwa mfano wa wanawake na watoto hawa ni ugaidi tu chini ya bendera ya kulinda uhuru. Kutia hofu katika akili za Waislamu endapo watataka kushikamana na kitambulisho chochote wa Kiislamu ndilo lengo la kweli hapa.

Waislamu wa ulimwengu wanaweza tu kutarajia aina hizi za unyanyasaji kurefushwa na kuharakishwa kadiri kazi kwa ajili ya Khilafah ya kweli kupitia Hizb sahihi kupatikana kwake inavyozidi kuwa karibu.

Tangu 2017, maelfu ya wanawake na watoto wamewekwa kizuizini. Baadhi waliregeshwa katika mataifa yao, lakini wengi wamesalia katika jela za Syria na Iraq. Haki za binadamu kama zilivyojadiliwa katika sheria za Umoja wa Mataifa hazitumiki katika kesi za Waislamu, lakini lengo lao la kindoto kama chombo cha kuweka udhibiti liko wazi katika kesi hii ya ukandamizaji.

Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt) yanapatikana tunapoonywa juu ya hatari kubwa tunazokabiliana nazo kama Umma wakati mambo yetu yapo mikononi mwa adui anayetaka kuiangamiza Quran na Sunnah kama marejeo katika siasa za dunia. يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ عَدُوِّى وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَآءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِٱلْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا۟ بِمَا جَآءَكُم مِّنَ ٱلْحَقِّ يُخْرِجُونَ ٱلرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَـٰدًۭا فِى سَبِيلِى وَٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِى ۚ تُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِٱلْمَوَدَّةِ وَأَنَا۠ أَعْلَمُ بِمَآ أَخْفَيْتُمْ وَمَآ أَعْلَنتُمْ ۚ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ﴿ Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni, wakamfukuza Mtume na nyinyi kwa sababu mnamuamini Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu, mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayo yaficha na mnayo dhihirisha. Na mwenye kufanya hayo kati yenu basi ameipotea njia ya sawa.” [Al-Mumtahina 60;1]

Video zilizotumwa kwa BBC ya Kiarabu kutoka ndani ya jela la Baghdad zinaonyesha wanawake waliodhoofika wakiwa wamelala kwenye sakafu ya mawe magumu. Inadhaniwa kundi hilo halijala tangu tarehe 24 Aprili.

BBC imeambiwa kwamba mwanzoni mwa mgomo huo wa njaa, washiriki walikuwa wakinywa nusu glasi ya maji kwa siku. Baadhi ya wanawake sasa wameacha kunywa kabisa.

Watoto wadogo pia wanaweza kuonekana kwenye kanda hiyo ya video - wengi wanaripotiwa kuzaliwa ndani ya jela hilo.

Mwenyezi Mungu (swt) airegeshe hadhi ya Ummah huu katika hali yake ya awali kabla ya kuvunjwa Khilafah, Amin!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Imrana Mohammad

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu