Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Utanuzi Mkubwa wa NATO Unaifanya iwe Tisho la Dunia

(Imetafsiriwa)

Tokea mwanzo ulipoanguka Umoja wa Kisovieti na kuvunjika kwa Muungano wa Warsaw, NATO ikawa ni chombo kinachoyumba, kisicho na usukani – lakini ilikuwa ni kwa muda tu. Marekani ikawa inasumbuka juu ya nini cha kufanya baada ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na kuwa ni mwisho usiopingika wa Vita Baridi.

Lakini NATO haikuwa mshirika mzuri kiasi hicho cha kuitupa. Sio kila siku unapata mataifa yenye nguvu yanayokubali kugharamia Utafiti na Maendeleo (R&D) kwa kiasi cha asilimia 2 ya Pato Ghafi la nchi (GDP) kwa ahadi ya kulindwa kutokana na maadui wanaoweza kupatikana.

Marekani imeibakisha NATO ili kuiweka Ulaya chini ya utawala wake wa kuendelea hata baada ya kumalizika kwa Vita Baridi - hasa kwa upande wa kuwa juu kijeshi. Ulaya kwa kiasi imenufaika na amani tokea mwishoni mwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ambapo kwa tukio la sasa la mzozo wa Ukraine limewashtua. Hata hivyo, mkakati wa muda mrefu wa Marekani wa dunia hauendi sambamba na amani ya kuazima ya Ulaya tangu kuwepo kwa upanuzi wa kuendelea wa NATO hadi kuwakasirisha Wamarekani na kuvunjwa kwa utulivu wa Ulaya.

Wakati Macron alipoielezea NATO mnamo Novemba 2019 kuwa ni maiti, na kutaka Ulaya ianzishe kikosi chake chenyewe, hili liliistua Marekani. Hili liliishawishi Marekani kusisitiza juu ya kuipa nguvu NATO. Vita vya Ukraine ikawa ni fursa adhimu ya kuiepusha Ulaya isitoke katika umiliki wake, ubwana na utawala wake. Na hii ilifanya kazi ya kipigo cha moja kwa moja kwa ndoto za Ulaya za kujitegemea kijeshi na uhuru, ikiongozwa na Ufaransa, kuikwepa Marekani. Kujumuishwa Finland na Sweden kwenye NATO katika mkutano wa Lithuania kulifanyika kwa lengo la kuzivunja ndoto za Ulaya! Marekani haina budi kuwa na furaha ya hali ya juu kwa kuwa imefanikiwa katika malengo mawili muhimu; kukomesha majaribio ya ukwepaji ya Ulaya na utanuzi wa NATO kuelekea mashariki.

Ama kwa Upande wa Ukraine…

Wakati Biden alipoeleza “viongozi wa NATO wamekubaliana kuwa Ukraine itakuwa mwanachama baada ya vita” (BBC, 12/7/2023), hii inaashria wazi ukataaji wa Marekani kwa Ukraine kwenye mashirikiano. Kwa hiyo ilikuwa haishangazi kuwa msimamo huu ulikuwa katika taarifa ya mwisho ya mkutano. Viongozi wa NATO hawakuja kuuachia mualiko kwa Kiev au kuweka ratiba kwa ajili ya kupata nafasi hiyo, ambayo inaihitaji, lakini wametengua takwa la kukamilisha kile kiitwacho Mpango wa Utekelezaji wa Uanachama (MAP), ambao huwa unaondoa kizuizi katika njia ya Ukraine ya kujiunga nayo. Mripuko wa hasira wa Zelensky kwenye twitter ulikuwa - bila kutia chumvi – ni wa masikitiko, lakini anajifunza somo gumu. Anajifunza kile ambacho ni gharama ya kinachohitaji ‘usaidizi’ wa Wamagharibi – udhalilifu na utumwa kwa thamani ya damu ya watu wako! Baada ya Ukraine kuchochewa na Marekani kuomba uanachama wa NATO, hivi sasa imekataliwa – wakati imeshachelewa, kwa sababu imeshamuweka dubu wa Urusi mwenye hasira juu yake!

Ama kwa Upande wa China…

Vita nchini Ukraine kwa kweli vimeipa NATO hamasa mpya. Kwa hakika, haikuwa nayo kabla. Katika hali ya ujasiri, Marekani inazingatia utanuzi wa NATO kuitisha China kana kwamba jukumu la NATO halitambui mipaka! Taarifa ya kikao imeitaja China katika vifungu hivi; 6, 23, 24, 25 na 55.

“Malengo yanayotajwa na sera za mabavu za Jamhuri ya Watu wa China (PRC) ni changamoto kwa maslahi yetu, usalama na maadili.”

“PRC inatumia uwanja mpana wa ala za kisiasa, kiuchumi, na kijeshi kuongeza nyayo zake kiulimwengu na uwezo wa kuelekeza nguvu za kijeshi, huku ikibakia yenye utata kuhusu mikakati yake, malengo na kujijenga kijeshi.”

“Tunajivunia utambuzi wetu wa pamoja, kuimarisha uimara wetu na utayari, na kujilinda dhidi ya mbinu za kulazimisha za PRC na juhudi za kuugawa Muungano wetu. Tutasimamia maadili yetu ya pamoja na mpango wa misingi ya kisheria ya kimataifa, ikiwemo uhuru wa safari baharini.”… na kadhalika.

China haikupoteza muda katika kuipinga hatua hii (China imerudisha mapigo kwa shutuma za NATO, ikaonya kuwa itahifadhi haki zake. (Reuters) https://www.reuters.com/world/china-opposes-natos-move-into-asia-pacific-region-warns-resolute-response-2023-07-12/

Macron aliliona hili mnamo mwezi wa Juni na akalipinga pia. Wakati Katibu Mkuu wa NATO Jenerali Jens Stoltenberg aliposema NATO inazingatia kufungua afisi ya uhusiano nchini Japan, Macron alijibu kwa haraka akisema: “Eneo la Indo Pasifiki sio sehemu ya Atlantiki ya Kaskazini, hivyo tusionyeshe kuwa NATO kwa kiasi fulani inajenga uhalali na inaanzisha uwepo wake katika maeneo mengine kijiografia.” Bila shaka Ufaransa ina sababu zake kwa uungaji mkono huu kwa China.

Ujumuishaji wa Japan, Australia na New Zealand na Korea Kusini kuwa waangalizi katika mikutano ya NATO una kichache cha kushawishi mashaka ya China. Hii huenda imekuwa sehemu ya sababu ya kushindwa ziara ya Blinken kutokana na China kukataa kukubali kufungua njia za mawasiliano baina ya majeshi yao mawili. Hivyo, Marekani hivi sasa inafanya kazi ya kuongeza mbinyo kwa China, na inaitumia NATO kufanya haya.

Kwa Maeneo mengine ya Dunia…  

Mkutano ulielea juu ya kauli za jumla za sera za dunia kutokea Mashariki ya Kati, “washirika wetu wa zamani katika Mjadala wa Mediterenia”, hadi Afrika na AU. Lakini hili linamaanisha tu kuwa Marekani inajaribu kuweka udhibiti wa utawala kupitia NATO juu ya maeneo haya kupitia na chini ya kivuli cha ‘kukuza mawasiliano na ushirikiano wa ndani katika maeneo hayo ambayo wanachama wa NATO kama Marekani, Uingereza na Ufaransa wanapambana baina yao kwa ajili ya ushawishi wa kieneo (kama inavyoonekana hivi sasa katika ugwe wa mapinduzi ya Afrika Magharibi).

Mashindano Mapya ya Silaha…

Utanuzi wa NATO kwenye maeneo ya Asia ya Pasifiki kukabiliana na uchokozi unao ongezeka wa China utapelekea tu kwenye mashindano ya silaha sawa au hata yenye kushtua zaidi ya Vita Baridi vya kwanza. Kauli ya Vilnius imeeleza katika kifungu cha 44 kuwa “vikosi vya mkakati wa nyuklia wa Muungano, hasa ule wa Marekani, ni wa uhakikisho wa juu zaidi wa usalama wa Muungano.” Kifungu cha 45 kinaendeleza dhamira ya kizuio cha nyuklia – bila ya kuitaja wazi Urusi (“Matumizi yoyote ya nyuklia dhidi ya muungano yatabadilisha kabisa hali ya mzozo (nchini Ukraine).”) au China bila shaka.

China haikukaa tu ikiangalia hili. Uimarishaji wa silaha wa China ni jambo lililo wazi likiwa na vipengele vya wazi kwa ajili ya usambazaji wa vikosi vya mashambulizi. Inatosha kusema, katika hali ya sasa ya mahusiano ya Marekani na China Vita Baridi tayari vinaendelea – au ‘Vita Baridi 2.0’ kama ilivyotungwa kwa majisifu na Niall Ferguson.

Hitimisho

NATO imejiweka kuwa ni mshurutishaji wa maslahi ya Marekani, ikipuuza kile kiitwacho mipaka ya kijiografia ya ‘Atlantiki ya Kaskazini’ na vizuizi vya mkataba. Vifungu vyovyote vilivyowekwa katika kuiunda NATO vimetupwa kwa maslahi ya ubwana wa dunia. Kama Marekani ingetaka, eneo la NATO lingefika mwezini! Ni uhakika, anga ni eneo linalofuatia la mapambano ya kugombea mamlaka, hivyo hii inaweza kuhakikisha kuwa ni zaidi ya kauli ya kejeli hivi karibuni (“China Inasisitiza ushirikiano wa ‘Amani’ huku Marekani iking’ang’ania Mjadala wa UFO [Unidentified Flying Objects]” Newsweek)

Hili ni funzo kwa Ummah wa Kiislamu katika kujihusisha na miungano na mashirika ya Magharibi. Wanaweza muda wowote kutafsiri upya vifungu au mikataba ya muungano wowote au makubaliano kukidhi maslahi yoyote wanaoyaona ni muhimu kwao. Makubaliano siku zote yanabaki kuwa yanayoweza kubadilika.

Hili linaonekana katika historia; Wamagharibi kila wanapoingia kwenye mikataba huwa ni kwa kubuni na kujenga mnyambuliko wa kiwango cha juu kwa ajili ya ujanja wa baadaye ambao tunaushuhudia hivi leo. Hili limeonekana wazi katika mikao mikubwa yote walioifanya kama Mkataba wa Westphalia (1648), Kongres ya Aix la Chapelle (1818) ya Ulaya, nk. Hali hii ni sawa na iliyokuwa wakati walipokuja kwenye nchi zetu kututawala, wakitengeneza mikataba na makubaliano na machifu wa makabila kwa ajili ya biashara (mwanzoni) ambayo ilikuwa wazi kwa mabadiliko yasio ya haki. Kampuni ya Royal Niger imekuwa hodari kwa hili.

Fikra ya NATO ya kuwa ni shirika lenye kushinda na kuendelea kutanuka kijeshi ni suala la hatari kwa maslahi na ustawi wa wanadamu kwa jumla. Ni muungano wa mataifa yenye nguvu, yakiongozwa na Marekani, yenye kumiliki uwezo wa nyuklia na silaha nyengine za uharibifu mkubwa. Kiongozi wa shirika hili adui na chokozi, Marekani, imeonyesha kutokuwa na aibu au kusitasita katika kulitumia ili kufikia maslahi yake binafsi ya dunia kwa hasara ya watu wa Ukraine. Nani atafuatia? Dunia haipaswi kuzubaa kwa kutulia kuona. Suluhisho kwa hili ni kupambana na kuidhoofisha fikra ya mashirika chokozi kama haya kwa kuunda rai jumla ya kilimwengu dhidi yake. Ni kwa kuisimamisha Dola ya Kiislamu Khilafah, ambayo muda wake umefika, ndipo hili litawezekana.

[وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ]

“Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehma kwa walimwengu wote.” [Al-Anbiya: 107]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Salim Muhammad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu