Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mzozo wa Gaza Wafichua Viwango Maradufu vya Wamagharibi

Mzozo wa Gaza unaoendelea ndani ya Ardhi ya Baraka ya Palestina ni baraka iliyojificha. Wamagharibi wakoloni wakiongozwa na Amerika na washirika wake wamefichuliwa kikamilifu. Hakika, upatilizaji wa matumizi ya viwango maradufu uko juu mno. Matukio yafuatayo ni baadhi tu yanayothibitisha hilo:

Kwanza, mnamo Machi 27, 2023, Baraza la Pili la Kabla-Kesi la Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa Rais wa Urusi, Vladmir Putin na Kamishna wa Urusi wa Haki za Watoto, Maria Alekseyevna Lvova-Belova. Msingi wa maamuzi yao ni ripoti iliyoandaliwa na watafiti wa Chuo Kikuu cha Yale waliodhaminiwa na Kitengo cha Wizara ya Kigeni cha Amerika, iliyodai kwamba Urusi iliwahamisha kinyume cha sheria watoto zaidi ya 6,000 na kuwapeleka katika mtandao wa kambi ndani ya mipaka ya Urusi. Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu anaendelea kuua zaidi ya watoto 10,000 ndani ya Ardhi ya Baraka ya Palestina. Hakujatolewa hati za kukamatwa kwake!

Pili, mnamo Juni 17, 2020, Rais wa Amerika, Donald Trump alisaini kuwa sheria Kifungu cha 2020 cha Sera za Haki za Kibinadamu kwa Uyghur. Sheria hiyo iliwawekea vikwazo maafisa wa Uchina wanaohusika na sera dhidi ya Uyghur. Kwa upande mwingine, Amerika na washirika wake hivi sasa wanatoa silaha na ulinzi kwa Umbile la Kiyahudi ‘Israeli’ dhidi ya Uislamu na Waislamu!

Tatu, ile inayojiita jamii ya kimataifa inailani Urusi kwa kukalia mipaka ya Ukraine. Ikidai kwamba Urusi haiheshimu sheria ya kimataifa ambayo yatambua mipaka ya Ukraine. Kwa upande mwingine, Amerika hivi sasa inahifadhi Azimio la Balfour la Uingereza ambalo ndio msingi unaotumiwa na Umbile la Kiyahudi ‘Israeli’ kuvamia na kumwaga damu za Waislamu na kunajisi matukufu ya Uislamu. Wakati huo huo, Mazayuni wanadai suluhisho la dola-moja. Amerika inawaunga mkono kwa kisingizio cha suluhisho la dola-mbili!

Nne, mnamo Disemba 5, 2023, kasuku ‘vyombo vya habari’ wa Kimagharibi wakiongozwa na muendeshaji kipindi kinachojiita Piers Morgan Uncensored, walikitumia kudhilalisha na kukejeli Uislamu na Waislamu. Hiyo ni kuhusiana na kuwa Waislamu duniani kote ikijumuisha Uingereza wakiongozwa na Hizb ut Tahrir waliandaa maandamano wakitaka kuunganishwa kwa majeshi ya Waislamu ili kuikomboa Gaza na Ardhi ya Baraka ya Palestina yote! Walimbandikizia mgeni katika kipindi hicho, kaka yetu Dkt. Abdul Wahid, Mwenyekiti wa sasa, Kamati ya Hizb ut Tahrir Uingereza kuwa ana msimamo mkali na anapigia debe Ugaidi! Badala ya muendeshaji kipindi, kukemea na kumshambulia mvamizi na muuaji, Umbile la Kiyahudi ‘Israeli’!

Tano, mnamo Disemba 8, 2023, Amerika ilipiga kura ya turufu dhidi ya pendekezo la Umoja wa Mataifa kwamba mzozo usitishwe ndani ya Gaza!

Sita, mnamo Disemba 13, 2023, watawala Waislamu vibaraka wa wakoloni waliamrishwa na mabwana zao wakoloni Wamagharibi kufanya mkutano wa pili mjini Riyadh, Saudi Arabia kuwaleta pamoja Waislamu wakuu wa majeshi chini ya mwamvuli wa Muungano wa Kiislamu wa Kijeshi wa Kupambana na Ugaidi (IMCTC) uliobuniwa mnano Disemba 2015 na utawala wa Saudi uliolaaniwa na uliojaa hila ukiongozwa na Mohamed bin Salman. Ajenda kuu ilikuwa ni kutathmini mkakati na kufaulu kwa muungano kuhusiana na kutatua masuala ya kimfumo, kimawasiliano, kifedha na oparesheni za kijeshi za makundi ya kigaidi kwa mujibu wa maamrisho ya Wamagharibi ambayo yanajumuisha Hamas!

Saba, mnamo Disemba 19, 2023, Amerika ilitangaza muungano wa mataifa 10 unaoitwa Oparesheni ya Ulinzi wa Ustawi, ili kuweza kulinda meli zinazotumia Bahari Nyekundu kutokamana na mashambulizi ya Houth yanayolenga vyombo vinavyomilikiwa na Umbile la Kiyahudi ‘Israeli’ au kutoka nchi zinazoliunga mkono kwa njia ya moja kwa moja au isiyokuwa hiyo! Hakika, kuna ustawi katika kulinda muuaji wa Waislamu!

Nane, kuwashika na kuwanyamazisha Waislamu wakijumuisha wanachuoni ndani ya ulimwengu wa Waislamu. Mfano wa hivi majuzi ni ule wa utawala wa Saudi Arabia, kumshika Muislamu mwanamume katika Msikiti wa Mtume ndani ya Madinah, kwa kosa tu la kuomba dua kwa ajili ya ukombozi wa Qiblah cha Kwanza cha Waislamu, Masjid al-Aqsa na Ardhi ya Baraka ya Palestina yote! Wanachuoni waovu ndani ya Saudi Arabia na nchi nyingine za Waislamu wako kimya kabisa kama ambaye yanayotokea Gaza hayawahusu. Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, wanashughulika nyuma ya pazia kuhalalisha mahusiano na muuaji wa Waislamu na kunajisi matukufu ya Uislamu! Aibu iliyoje!

Hayo hapo juu ni baadhi tu ya mifano inayothibitisha kuanguka kwa mfumo wa Kimagharibi uliofeli na uliojaa uhadaifu na wafuasi wake popote walipo. Kwa mara nyingine Wamagharibi wakoloni wamefichuliwa na hawana popote pakuficha sura zao. Walikuwa wakijipiga kifua kuwa wao ndio ngome ya demokrasia, walinzi wa haki za kibinadamu, wanaoheshimu sheria za kimataifa nk. Hakika, wao sio chochote, bali ni mabwana katika udanganyifu wa kisiasa, kijamii na kiuchumi!

Wamagharibi na wapambe wao wamepanua upatilizaji wa watu kwa sharti itawafikisha katika maslahi yao ima ya kindani au ng’ambo. Mfano mzuri ni Kenya, katika miaka ya 1950 Waingereza waliwabandikiza wapiganaji wa Mau Mau wakweli kuwa ni magaidi na yeyote aliyewahurumia yuko pamoja nao. Hivyo basi, wakawashika, wakawatesa na kuwaua kwa kudai uhuru! Hivi majuzi, Amerika chini ya utawala wa Biden, waliwabandikiza wale wanaojiita Weupe watukufu kuwa ni magaidi! Kwa kuongezea, polisi nchini India mnamo Novemba 28, 2023 waliwabandikiza wanafunzi saba kutoka Kashmir kuwa magaidi na kuwashika, kwa kosa tu la kusherehekea Australia kuishinda timu ya kriketi ya India!

Kila kitu sasa kiko wazi kama ilivyo nyeusi na nyeupe. Kila mtu anaweza kujionea mwenyewe na kuwa hakimu. Matukio ya kimataifa yanawafungua macho wale ambao wameisoma historia kwa makini na kuweza kuunganisha vitone. Ubwana wa Amerika unakaribia kutangazwa kuwa umekufa na nafasi yake kuchukuliwa SIO na Uchina au ule unaoitwa muungano wa BRICS+ kwa sura ya ulimwengu wa wenye usemi wengi! Badala yake ni kuwa nafasi yake itakaliwa na kurudishwa tena maisha ya Kiislamu kupitia kuisimamisha Serikali ya Kiislamu, Khilafah kwa njia ya Utume. Njama zote ovu dhidi ya kuchelewesha kuchipuza Khilafah, zimefeli, kuanzia na ile ya kubuni kijidude kwa jina ISIS, kuubandikiza Uislamu kuwa ni mfumo wa siasa kali na Waislamu kuwa watu wenye misimamo mikali!

Wakati ni ndio huu kwa Waislamu hususan walioko ndani ya majeshi ya Waislamu kuweza kunyanyuka na kuitikia mwito kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt): ﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ “Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]. Kwa kuongezea, jamaa za wanajeshi lazima wapatilize fursa kuwakumbusha jamaa zao kwamba kutoa msaada (nusrah) kwa maana kuitikia mwito wa Mwenyezi Mungu (swt) ni wajibu ambao kwamba lau Hautatekelezwa utawapelekea kulaaniwa na Mwenyezi Mungu (swt)! Njia ni mbili, ima ni wanajeshi kujibu mwito wa Mwenyezi Mungu (swt) au kuendelea kubakia wametiwa minyororo ndani ya kambi zao za kijeshi. Wakisubiri maagizo kutoka kwa watawala Waislamu vibaraka wa wakoloni, ambao wao wenyewe wanasubiri maagizo kutoka Washington, London, Paris, Berlin, Beijing na Moscow!

Ama kuhusu Waislamu waliobakia ndani ya Ummah hususan wale walioko ndani ya nchi za Waislamu, lazima wayaelekeze maandamano yao na hasira zao katika nyumba (ikulu) za watawala Waislamu vibaraka wa wakoloni. Fauka ya hayo, wamtake ajifunge na atekeleze kwa ukamilifu Shari’ah ya Kiislamu. Agizo lake la kwanza liwe ni kwa majeshi kuikomboa Ardhi ya Baraka ya Palestina. Kukosa kufanya hivyo, wampindue na nafasi yake kuchukuliwa na mwanamume Muislamu muadilifu, Khalifah. Inaonekana kuwa ni kazi ngumu mno kwa wale waliotekwa na fikra za kisekula za kirasilimali, lakini ni rahisi kutekeleza unapotekwa na uchajimungu (taqwa) na ukweli (ikhlass). Mwenyezi Mungu (swt) alisema:

وَيَوۡمَٮِٕذٍ۬ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ﴿ “Na siku hiyo Waumini watafurahi.” [30. Ar-Rum: 4]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro (Abu Taqiuddin)

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu