Ijumaa, 29 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sasa Je? Je, tunaweza kufanya nini ili kuleta mabadiliko?

(Imetafsiriwa)

Nchini Pakistan, chaguzi za hivi majuzi chini ya Demokrasia zilithibitisha kuwa hazileti mabadiliko. Dola za Magharibi na vibaraka wao hawataki mabadiliko. Watakwenda urefu wowote ili kuyazuia. Watu wamechanganyikiwa na wana hasira.

Kwa hiyo, sasa, je? Je, tunaweza kufanya nini ili kuleta mabadiliko?

Ni lazima tufuate njia ya Mtume (saw) kuleta mabadiliko. Ndiyo njia pekee ya mafanikio Duniani na Akhera. Kuna hatua tatu kutoka katika Sunnah yake (saw) ambazo ni lazima tuzihuishe.

Hatua ya Kwanza: Kufuwandisha Jamaa na Marafiki zetu kuhusu Mabadiliko ya Kiislamu

Mwenyezi Mungu ﷻ  amesema,

[وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ]

“Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.” [Surah ash-Shu’ara 26:214].

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alimlingania mkewe Bibi Khadija (ra) na akamuamini (saw). Kisha (saw) akamlingania binamu yake Ali (ra) na akamuamini (saw). Yeye (saw) akamlingania rafiki yake Abu Bakr (ra) ambaye pia alimwamini (saw). Aliendelea (saw) kuwalingania watu kwenye Uislamu. Wengine waliamini na wengine walikataa. Aliwakusanya wale walioamini katika Dar ul-Arqam, au yeye (saw) angemtuma mtu fulani awafunze katika halaqa majumbani mwao, au kwenye mabonde ya milima. Ujumbe ulikita mizizi ndani ya nyoyo zao na katika akili zao. Uislamu ukawa kama damu kwenye mishipa yao. Wakawa mifano inayotembea ya Uislamu.

Kwa hivyo, je, tumewaendea watoto wetu wa kiume na wa kike, kaka na dada zetu, waume na wake zetu, mama na baba zetu, ili kuwafundisha kuhusu mabadiliko ya Kiislamu? Je, nyumba zetu ni kama Dar ul-Arqam? Je, tuna halaqa majumbani mwetu?

Hatua ya Pili: Kutangaza Ujumbe wa Mabadiliko ya Kiislamu Hadharani

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[فَاصْدَعْ بِمَا تُؤمَرُ وَ أَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِکِیْنَ]

“Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina.” [Surah Al-Hijr 15: 94]. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitokeza kutoka Dar ul Arqam na kundi lake la Maswahaba (ra), katika maandamano ya hadhara. Kwa namna ambayo haijashuhudiwa kabla na Waarabu, walifanya Twawaf kuzunguka Ka’aba wakitangaza Ujumbe. Yeye (saw) aliwapinga madhalimu, Maquraishi, miungu yao, itikadi zao na fikra zao kwa kuonyesha ubatili wao, ufisadi na upotovu wao. Aya za Quran ziliteremshwa kwa Mtume (saw) zikishambulia vitendo vyao vyote vya ufisadi ikiwa ni pamoja na ulaji riba, kuua watoto wao wa kike, kulaghai katika mizani na kuzini. Aya hizo pia ziliwashambulia viongozi wa Maquraishi, zikikashifu babu zao na akili zao. Aya zilifichua njama zao dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na Maswahaba zake (ra).

Kwa hivyo, je, tunaandaa masomo ya Kiislamu katika misikiti, makongamano, mihadhara na bayani katika maeneo ya umma? Je, tunaeneza ujumbe wa mabadiliko ya Kiislamu kwenye mitandao ya kijamii? Je, tunafichua jinai na njama za madhalimu dhidi ya Dini yetu? Je, tunaongeza ufahamu wa umma kuhusu mfumo wa Kiislamu ni nini? Je, tunatoa maelezo ya jinsi Uislamu utakavyobadilisha Ulimwengu wa Kiislamu, pamoja na ulimwengu mzima?

Hatua ya Tatu: Kuhakikisha Wanajeshi Wenye Nguvu Wanatoa Nusrah (Msaada wao wa Nyenzo) kwa Mfumo wa Kiislamu

Katika Bay’ah ya pili ya Aqabah, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema, «أُبَايِعُكُمْ عَلَى أَنْ تَمْنَعُونِي مِمَّا تَمْنَعُونَ مِنْهُ نِسَاءَكُمْ وَأَبْنَاءَكُمْ»  “Nawapa Bay’ah kwa msingi kuwa mtanilinda kama mnavyolinda wake zenu na watoto wenu.” [Musnad Ahmad] Al-Bara’ alichukua mkono wake kutoa bay’ah na akasema, فَبَايِعْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَنَحْنُ أَهْلُ الْحُرُوبِ وَأَهْلُ الْحَلْقَةِ وَرِثْنَاهَا كَابِرًا عَنْ كَابِرٍ “Tunatoa Bay’ah yetu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sisi ni watu wa vita na silaha ambazo tumerithi kutoka kwa baba hadi mtoto.” Hivyo, walikuwa ni makamanda wa jeshi wa Ansar (ra) waliotoa Nussrah yao (Msaada wa Nyenzo) ili kuhakikisha Uislamu unatabikishwa kivitendo.

Kwa hivyo, je, tumewafahamisha watoto, kaka na baba zetu katika jeshi kuhusu wajibu wao wa kuunga mkono mabadiliko ya Kiislamu? Je, wanawatazama Ansari (ra) kama vielelezo vyao? Je, wako tayari kuchukua hatua kukomesha utawala wa madhalimu?

Haya ndiyo matendo ambayo Hizb ut Tahrir inayafanya ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Jiunge na Hizb ut Tahrir. Jifunze kuhusu mabadiliko ya kweli. Fanya kazi kwa ajili ya mabadiliko ya kweli.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[لَقَدْ کَانَ لَکُمْ فِیْ رَسُوْلِ اللّٰہِ اُسْوَۃٌ حَسَنَۃٌ لِّمَنْ کَانَ یَرْجُوْا اللّٰہَ وَالْیَوْمَ الاٰخِرَ وَذَکَرَ اللّٰہَ کَثِیْراً]

“Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.” [Surah Al-Ahzab 33: 21].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu