Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mafunzo kutoka kwa Maafa ya Vita vya Bosnia

Mwezi huu wa Julai unafikisha mwaka wa 25 tangu mauwaji na halaiki ya Waislamu wa Bosnia eneo la Srebrenica ambayo ni uhalifu uliotekelezwa na Jeshi la Kibosnia la Waserbia, likiongozwa na 'Mchinjaji wa Bosnia', mhalifu wa kivita Ratko Mladic. Ilikuwa ni miaka 25 iliyopita Julai hii ambapo ulimwengu ulisimama kando na kuwatazama wanaume, wanawake na watoto wa Kibosnia wakichinjwa, kunajisiwa, kuteswa na kufurushwa majumbani, vijijini na mijini mwao eneo la Mashariki mwa Bosnia katika ile iliyoitwa kampeni ya 'mauwaji ya kimbari' iliyo ongozwa na mhalifu wa kivita wa Bosnia wa Kiserbia Radovan Karadzic.

Dola za kimataifa kama Amerika, Uingereza na Ufaransa pamoja na mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa pasi na kutaharaki na kwa ushirikiano walitazama au kujitia upofu huku Jeshi la Kibosnia la Waserbia likitekeleza mauwaji makubwa zaidi ya halaiki ya raia barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia. Katika hatua ya kumaliza vita vya Bosnia ambayo iliendelea tangu 1992 hadi 1995 kufuatia kuvunjika kwa dola ya Kikomunisti ya Yugoslavia, Amerika ilitaka amani kwa gharama yoyote kwa Wabalkan na hii ilikuwa ijumuishe gharama isiyo sameheka ya njama ya kisasi maarufu cha Waserbia wa Bosnia cha kuwauwa vilivyo maelfu ya wavulana na wanaume wa Kiislamu wa Kibosnia ambao ima walikuwa wakijihifadhi katika 'Maeneo Salama' yaliyo dhibitiwa na Waholanzi yaliyo telekezwa na Umoja wa Mataifa ya Potocari na Srebrenica au walikamatwa au kuuwawa wakijaribu kukimbilia milimani kuelekea mji wa Bosnia wa Tuzla. 

Orodha ya uhalifu wa Vita vya Kiserbia vilivyo ongozwa na Ratko Mladic na kutekelezwa na Jeshi la Kibosnia la Waserbia dhidi ya Waislamu wa Bosnia wakati wa vita hivyo inajumusha kuwafungia kikamilifu na uzingiraji wa siku 1452 wa mji wa Sarajevo – uzingiraji mrefu zaidi wa mji katika vita vya kileo baada ya uzingiraji wa Ghouta, Syria – kwa umiminaji mabomu na risasi za walenga shabaha za kuendelea kwa mji huo ambapo kwa pamoja ilichukua miaka mitatu na kuua Wasarajevo 14,000, ubakaji wa halaiki wa zaidi ya wanawake na wasichana 50,000 majumbani mwao, hotelini, kambini na hadharani uliofanywa na vikosi vya kijeshi vya Kiserbia kwa dhulma hizi chungu na msongo wa mawazo yaliyofanywa kwa watoto wao wasio na hatia na mateso, unyimaji chakula na mauwaji ya Waislamu katika kambi za mateso kama Omarska yote yalikuwa dhahiri kabisa ambapo viongozi wa ulimwengu walijua kuhusu uovu huu wa utaifa wa Kiserbia uliovuka mipaka ukiongozwa na Mladic na Karadzic na kwamba mauwaji haya ya halaiki ya Srebrenica yangeuweka uovu kama huo katika jiwe la Kihistoria.

Licha ya hatua bandia kutoka kwa viongozi wa dunia wakati huo kama aliyekuwa Waziri Msaidizi wa Kigeni Richard Holbrooke aliyekiri kwamba Vita vya Bosnia vilikuwa ni, "kufeli kukubwa zaidi kwa Magharibi tangu miaka ya thalathini."

Waislamu hawakuwa wajinga juu ya chuki kamili ambazo Dola za Kimagharibi barani Ulaya zilikuwa nazo kwa Waislamu wa Bosnia wakati wa vita hivyo. Maneno ya mpatanishi wa Muungano wa Ulaya Lord Owen kwa yakini yanafichua hili pindi aliposema kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu waliokuwa wamezingirwa Sarajevo, "Katu, katu, katu msiishi chini ya ndoto hii kwamba Magharibi itakuja na kutatua tatizo hili." Au pindi aliyekuwa waziri wa kigeni wa Ufaransa, Alain Juppe aliposema katika moja ya mahojiano akikusudia mauwaji ya halaiki ya Srebrenica, "Sote tulijuwa watu ambao wangeuwawa, au angaa kwamba Waserbia hawatasaza maisha ya  Wafungwa."  

Hakukuwa na lolote la kushangaza juu ya utekeleza uhalifu wa utaifa uliopitiliza wenye kiu ya damu ya Jeshi la Bosnia la Waserbia katika hamu yao ya kulipiza kisasi dhidi ya wavulana na wanaume wa Kiislamu wasiokuwa na silaha mashariki mwa Bosnia! Ratko Mladic alichukuliwa filamu huku akitazama kwa ujasiri kamera ya Kiserbia baada ya kuiteka Srebrenica akisema, "Mji huu tunaupatia taifa la Kiserbia kama zaidi. Wakati umewadia sasa wa kulipiza kisasi juu ya Waislamu."   

Baadaye ilifuatia, kwamba wavulana na wanaume 8,000 wasiokuwa na silaha, waliofungwa na kuzibwa macho wenye umri kati ya miaka 12 na 77 baada ya "kuhojiwa kwa kushukiwa uhalifu wa kivita" na kutenganishwa na mama, wake na binti zao ambao kwa maelfu walifurushwa hadi eneo la Bosnia, wangechinjwa kwa kipindi cha siku nne na kuzikwa katika makaburi ambayo yalitangulia kuchimbwa ambapo yalinaswa na picha za setilaiti wakati wa vitendo hivi vya mauwaji ya halaiki.

Kuna mafunzo mengi ambayo Waislamu wanaweza kuchukua kutoka katika mwaka huu wa kumbukumbu ya 25 ya Mauwaji ya Halaiki ya Waislamu eneo la Srebrenica. Kwanza, uchinjaji na uovu wa mauwaji ya halaiki yaliotekelezwa juu ya Waislamu tangu 1995 nchini Bosnia sio wa kipekee bali umeendelea hadi leo juu ya Waislamu nchini Syria, Myanmar, Turkestan Mashariki, Afghanistan, Somalia, Kusini mwa Thailand na Ufilipino, Iraq, Libya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Palestina na Yemen. Hadhara ya kimgambo ya Kirasilimali inayo ongozwa na Amerika baada ya Vita Baridi inaendelea hadi leo kudumisha vita vyake vya kiulimwengu dhidi ya Uislamu, kulinda maslahi yake ya kiulimwengu kupitia vita na uvamizi katika ulimwengu wa Kiislamu, kupitia vita vya wakala vya watawala vikaragosi wa Waislamu kama Mfalme Mtarajiwa wa Saudia Mohammed bin Salman nchini Yemen na kutoka kwa ushirika wa serikali za utaifa na mashirika ya kimataifa na ya kieneo kote duniani ambao wametabikisha sera za kupambana na ugaidi na misimamo mikali zinazo walenga raia Waislamu.

Pili, kuibuka kwa mrengo wa kulia wa vyama na mavuguvugu ya utaifa yaliovuka mipaka mithili ya vyama na mavuguvugu ya utaifa yaliovuka mipaka ya Kiserbia yanayo walenga na kuwatoa kafara Waislamu kwa kufeli kokote katika mujtamaa, yakiwaunganisha na kuwahamasisha wanaume na wanawake ambao hawakuathirika  kama muuwaji mkubwa wa Kiaustralia Brendon Tarrant aliyewaua Waislamu 51 wakati wa swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Noor katika eneo la Christchurch nchini New Zealand mnamo 2019. Kufikia hadi kwamba Tarrant alicheza wimbo wa utaifa wa Kiserbia "Iondoe Kababu" ndani ya gari alilokuwa anaendesha njia kuelekea Msikiti wa Al-Noor inayo muenzi Radovan Karadzic iliyoimbwa na majeshi ya Serbia wakati wa vita vya Bosnia.    

Tatu, Ummah wa Kiislamu pia unaweza kutambua barabara jinsi gani uovu wa "maslahi" ya Kiamerika unavyojua kuchochea mgogoro kwa Wabalkan kupitia kumuunga mkono Milosevic na kuyadumisha kupitia kulazimisha vikazo vya silaha juu ya Bosnia, ili kuunda hitajio kwa Amerika na eneo la Ulaya kupitia kuionyesha Ulaya kwamba wanaweza kwenda bila ya "uongozi" wa Amerika.

Nne, Bosnia pia ilikuwa ni ukumbusho wa wazi kwamba hata baada ya miaka ya uoanishwaji, Wabosnia wenye macho ya samawati bado hawakukubaliwa na Ulaya, kwa sababu walikuwa ni Waislamu. Hili ni somo kwa Waislamu wanaoishi Magharibi wanastahili kujifunza kwalo, namna yatakavyo telekezwa maadili na mila zetu katika jaribio la kuwa watu mambosasa na kuwa sehemu ya mujtamaa mpana, daima kutabakia shauku. Jamii ya Waislamu yahitaji kutatua hofu yoyote iliyo undwa kupitia sera za serikali na majaribio yanayo endelea ya kutaka kuuchakachua Uislamu, kupitia kushikamana imara na maadili yetu na muhimu zaidi kupitia kuamiliana na mujtamaa mpana na raia wa kawaida.

Tano, mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa kwa yakini sio marafiki wa Waislamu. Kutelekezwa kwa Waislamu wa Bosnia katika yale yanayoitwa 'Maeneo Salama' ambapo nyuma yaliwahadaa Waislamu kudhani kuwa Jeshi la Ulinzi la Umoja wa Mataifa (UNPROFOR) lingewalinda hatimaye ilikuwa wazi kwa Ummah. Umoja wa Maitafa hata ilisaidia kuwapa majeshi ya Serbia zaidi ya lita 30,000 za petrol ili kuwasafirisha wavulana na wanaume wa Kiislamu hadi makaburi yao ya halaiki!

Hivyo basi, Enyi Waislamu, ni lazima tujifunze kutokana na Historia ya Kiislamu kutoka kwa mfano wa kama Khalifah al-Mu'tasim billah pindi aliposikia ripoti za mwanamke wa Kiislamu kushambuliwa na Warumi katika mji wa Kirumi wa Ammuriyah. Khalifah huyu alisema, "Ripoti imenifikia mimi kwamba mmoja katika dada wa Kiislamu ameshambuliwa katika mji wa Kirumi. Wallahi, nitalituma jeshi ambalo ni kubwa kiasi ambacho likiwafikiwa wao mwanzo wake ungali unaondoka kambini mwetu. Na niambieni mji wa Warumi hawa ulio na nguvu zaidi na nitatuma jeshi katika mji huo." Hivyo basi, usalama unaweza kupatikana pekee chini ya Khilafah.

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakina, Iman (Kiongozi wa Waislamu) ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo.” [Muslim]

Ummah wa Kiislamu unahitaji uongozi wenye ikhlasi na utambuzi ulio na ari ya kukabili tishio lolote kwa Ummah huu, ngao kama ilivyo sifiwa na hadith nyingi ni kulinda maisha na heshima ya Ummah huu. Hivyo mfano wa kama aliyekuwa kiongozi wa Bosnia wa Kiserbia Radovan Karadzic anayewauliza kwa kejeli Waislamu nchini Bosnia huku akiwaua, "Yuko wapi Allah wenu?" atapokea majibu makali anayostahiki.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Tsuroyya Amal Yasna
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#Srebrenica25YearsOn    #Srebrenitsa25Yıl  #SrebrenicaMiaka25Baadaye   سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل#

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu