Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Muungano wa Ulaya Unang'ang'ana Kukabiliana na Janga la Kiuchumi la Covid-19

Na: Faiq Najah*

Akihutubia bunge la Ulaya Jumatano 27 Mei 2020, Rais wa Tume ya Ulaya Ursula Von der Leyen alipendekeza kwamba Muungano wa Ulaya uchukuwe deni la €750 Bilioni ilikupeana €500 Bilioni kama ruzuku na €250 Bilioni kama mikopo kwa nchi barani Ulaya zinazoteseka na kuharibikiwa kiuchumi kutokana na kufungwa kwa sababu ya Covid-19. Licha ya uhitaji wa haraka wa fedha hizi, inaweza kuchukua miezi mingi ya majadiliano kati ya nchi wanachama wa EU kabla makubaliano kufikiwa kiundani.

Wamagharibi wamelisimamia vibaya gonjwa la virusi vya Korona. Huku wakikaribia kupuuzia kabisa udhibiti wa maeneo ya kijiografia, Wamagharibi walitumia ubunifu wa kushangaza wa uwekaji masafa baina ya watu na kufunga miji kijumla, ikidhoofisha maisha jumla ya jamii. Uchumi wa Wamagharibi tayari ni tete kwa sababu ya nidhamu ya kiuchumi ya Kirasilimali iliyojengwa juu ya uhuru wa kumiliki unaosababisha kutekwa kwa mali na rasilimali na kikundi kidogo cha watu wasomi ambao hawana mwelekeo  wala uwezo wa kuzalisha shughuli za kutosha za kiuchumi kwa jamii nzima. Kikundi hiki cha wasomi wenye mali na nguvu kawaida hupendelea kuwekeza nguvu zao katika sekta ya fedha, ambayo yenyewe imekuwa kikwazo badala ya kufanya kazi kusaidia shughuli halisi za kiuchumi. Bila kuepukika, natija ya mfumo kama huu ni kwamba nchi za Kimagharibi kiujumla zinasumbuliwa na ugavi mbaya wa mali, ukosefu wa ajira na ongezeko la umaskini hata katika nyakati za kawaida.

Ulaya iko na shida za kipekee. Ilikuwa ni Uingereza na Amerika ambazo zilikuwa nyuma ya kubuniwa Jamii ya Ulaya kama njia ya kudibithi Ufaransa na, haswa Ujerumani dhidi ya kurudi kama dola zenye nguvu baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Hii ni kwa sababu nguvu zahitaji maamuzi, na kuunganisha Ujerumani na Ufaransa pamoja na nchi nyingine nyingi ndogo ndogo kutafanya maamuzi yao ya ufanisi kuwa magumu, kuzuilika na kuwa na vikwazo. Bado, uroho wa utaifa hauwezi kuzimwa na Ufaransa na Ujerumani, lakini licha ya ugumu, ziliweza kuenuka tena baada ya Vita vya Pili vya Dunia na zikawa ni nguvu kubwa. Zimefanya kwa bidii kujenga Muungano wa Ulaya kuwa jukwaa ambalo linaweza kuzalisha nguvu zao, hata wakati wanaendelea kupata taabu kutokana na uongozi mkuu dhaifu wa EU na kujitolea kugumu kufaulisha makubaliano yasiojulikana kutoka kwa serikali wanachama 27 wa EU kwa makubaliano muhimu. Wakati huo huo, inaonekana kwamba Ujerumani na Ufaransa zinataka kuchukua udhibiti utoaji maamuzi wa EU kwao wenyewe. Kwa mfano, mpango wa Benki Kuu ya Ulaya wa kupeana msaada wa kifedha kwa serikali kupitia upatikanaji dhamana ulipewa changamoto na mahakama ya juu ya Ujerumani mapema mwezi huu katika hatua ya kiajabu na isiyokuwa ya kawaida, kwa kuwa Benki hio Kuu haiko chini ya mamlaka ya mahakama za Ujerumani bali iko chini ya Mahakama ya Haki ya Ulaya. Inaonekana kwamba Ujerumani haikutaka Benki hiyo Kuu kufanya kazi ikiwa huru.

Hatimaye ufadhili kama huu ni muhimu kwa Ulaya na pengine kwa Ujerumani ni zaidi ya wote. Wiki hii pendekezo la €750 Bilioni  limefuatia moja kwa moja na tangazo la wiki kabla la Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Chansela wa Ujerumani Angela Markel, na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula van der Leyen ambaye hakika alikuwa waziri wa zamani katika serikali ya Merkel. Kinyume na nchi zingine za Kimagharibi, nguvu za kiuchumi za Ujerumani zimejengwa juu ya shughuli za kiuchumi za ndani na nguvu za utengenezaji, kwani Ujerumani inajulikana kwa idadi kubwa ya biashara ndogo ndogo na kiujumla imepinga tabia za Kirasilimali za kujenga viwanda vikubwa  vya kimataifa vyenye bajeti kubwa sawa na bajeti ya serikali kuu. Lakini hata hapa, mapato ya Ujerumani yanategema sana uuzaji wa mali nje ya nchi, haswa nchi za Ulaya Kusini, ambazo zinahitaji mwendelezo wa fedha kulipia bidhaa za ujerumani. Kivitendo, Ujerumani inafanyakazi kutumia mfumo wa kitambo wa kikoloni barani Ulaya, na utengenezaji unapewa thamani ya juu kuliko mali asili, kilimo, ama nguvu za kibinadamu, ikiiwacha Ulaya Kusini kwenye hasara ya kudumu ikilinganishwa na Ulaya Kazkazini. Ama kwa mfano huu wa kikoloni, njia pekee ya usanifu wa Kiuchumi wa Ulaya kufanyakazi ni kwa fedha kugurishwa mara kwa mara kwenda kusini, bila shaka na kwa kuambatanishwa na ‘masharti mingi’. Hivyo Ujerumani inajua kuimarisha fedha Ulaya ni muhimu si kwa nchi maskini za Ulaya pekee lakini muhimu hata kwa uchumi wa Ujerumani yenyewe.

Ugumu wa Ulaya ni natija ya dhana juu ya dola za kitaifa ambayo ilichipuka kutoka kwa makaazi ya Westphalian mnamo Karne ya 17 na, kabla hapo, upinzani kati ya Wafalme wa wanafamilia wa kifalme wa Kikristo barani Ulaya licha ya kuwa wote walijisalimisha kwa Papa mmoja. Kabla ya kubuniwa dola za kitaifa, nchi ziliweza kupanuka kiasili na kupungua kulingana na uwezo wa kutawala, nguvu za kijeshi na nguvu za kiuchumi. Lakini baada ya kuwekwa mipaka maalumu, nchi zenye nguvu hazina tena njia nyingine ila kuingililia na kunyonya nchi dhaifu ambazo haziwezi kujisimamia zenyewe. Njia sawa ya nguvu za Ujerumani ni kupanua maeneo ili kujumuisha, kwa mfano nchi maskini za Ulaya Mashariki ambazo zahitaji msaada na utawala bora. Hii italeta natija ya Ujerumani kuhuisha huduma na uangalizi wa mambo ya watu wake badala ya unyonyaji wa nchi zingine, kama ilivyotokea katika muda fulani kwa usimamizi wa yaliyokuwa maeneo ya Ujerumani Mashariki baada ya kuunganishwa tena. Muundo wa dola za kitaifa hauleti chochote ile kuendelea kulipa nguvu zaid taifa lenye nguvu na kulidhoofisha zaidi taifa dhaifu.

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ulimwengu karibuni utashuhudia kurudi kwa dola ya Khilafa Rashida itakayo simamishwa tena kupitia njia ya Mtume (saw) ambayo itaamua upanuzi wa eneo lake kulingana na nguvu zake, yenye kuwajibika na kuongoza kwa haki maeneo yake. Zaidi ya hayo, itaonesha kwa mara nyingine utukufu wa serikali moja yenye utawala mkuu, juu ya miundo ya dola za Kimagharibi zilizo gawanyika, zilizo vunjika na zilizo feli.

*Imeandikwa kwa Gazeti la Al-Rayah – Toleo 290

#Covid19    #Korona      كورونا#

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu