Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Serikali ya Kyrgyz ni Adui wa Wanawake, Adui wa Uislamu
(Imetafsiriwa)

Watu wa Asia ya Kati wamepitia mateso chini ya utawala wa Tsar, na baada yao Utawala wa Wakomunisti chini ya Muungano wa Kisovieti, walio watawala kwa mkono wa chuma, wakivunja misikiti na kuigeuza kuwa vilabu au mabanda ya farasi. Waislamu wa huko hawakuvuta kuvuta pumzi za afueni baada ya kuporomoka kwa Muungano wa Kisovieti na kuanguka kwa utawala wake, kabla ya watawala wa vibaraka waovu kuwajia; na utawala wao haukutofautiana na wa wale walio watangulia kwa chochote kile, kwani wote waliafikiana katika vita dhidi ya Uislamu huku uadui wao kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) na waumini ukiwa sawa.

Serikali eneo la Asia ya Kati bila kuisaza hata moja hutumia upanga wao pasi na aibu katika vita visivyo na mwisho kwa chochote kinachohusiana na Uislamu. Watawala wake wanajua fika kwamba Waislamu huko kamwe hawatasita kurudi katika dini yao pindi fursa yoyote utakapoibuka kwao. Na wanajua kwa yakini kuwa kurudi kwa Waislamu katika dini yao na kuwazuia baina yao na hili litamaanisha kuporomoka kwa serikali zao na kuangamia kwa viti vyao vya enzi.

Vyama vya kidini vimepigwa marufuku bila ya kukisaza hata kimoja. Hakuna chama chochote kilicho na mwelekeo rasmi wa Kiislamu ambacho kimesajiliwa katika nchi yoyote ya Asia ya Kati isipokuwa Chama cha Mwamko cha Kiislamu nchini Tajikistan. Serikali pia zinafanya kazi kukausha chemichemi za kifikra zinazo nawirisha vijana wa Kiislamu na kuliimarisha fungamano lao na imani yao. Sheria dhidi ya ugaidi zilizopitishwa na serikali hizi, kama vile Sheria ya Uhuru wa Imani na Vitendo vya Kidini iliyopitishwa na Tajikistan mnamo 2009, imepelekea kufungwa kwa maelfu ya misikiti na shule za kidini zilizo asisiwa baada ya kuporomoka Muungano wa Kisovieti. Mnamo 2011, serikali hii ilipitisha sheria ya "majukumu ya wazazi", ambayo kwayo iliharamisha vijana wa kiume na wa kike walio chini ya umri wa miaka 18 kuhudhuria misikitini, na familia za wanaokiuka hutozwa faini na adhabu chini ya sheria hii ya kidhalimu. Kwa kuzingatia serikali hizi kandamizi zinazolenga sio tu vyama vya kisiasa na maabadi pekee, bali muonekano wa Uislamu wa aina yoyote unalengwa, unapigwa vita na wahusika wake wanaadhibiwa kana kwamba ni wahalifu!" Na maneno ya serikali hizi ni mithili ya watu wa Lut waliposema: "Wafukuzeni nje ya mji wenu, hakika hawa ni watu wanaotaka kuwa watakatifu (kutokana na madhambi)!" Ndevu zinapigwa vita, wanaume wanaofuga ndevu kuadhibiwa, na uvaaji wa mtandio, yaani hijab, umepigwa marufuku katika vitengo vya serikali, masokoni, usafiri wa umma, na makazini, na maafisa wa polisi huzivua hijab vichwani mwa wale wanaozivaa mabarabarani. Ama niqab, imepotea kwa kudumu miaka kadhaa iliyopita. Bali, uhalifu wa serikali, ikiwemo serikali ya Kyrgyz, umewafanya kukipiga vita Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kana kwamba hawajui matokeo ya vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Kitabu Chake Kitukufu. Yeyote anayethibitishwa kuwa na nakala ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu anaadhibiwa kwa kufungwa gerezani na hata kuteswa kunako pelekea kupata shahada. Wanataka kuvitenganisha vizazi vya Waislamu na Quran, kama walivyovitenganisha na lugha ya Kiarabu, baada ya kupiga marufuku usambazaji wa herufi za Kiarabu na kulazimisha alama za Latin na lugha ya Kirusi kama lugha ya kwanza.     

Uhalifu huu dhidi ya Waislamu unafanywa chini ya macho ya Umoja wa Mataifa na nchi kuu ambazo huficha uhalifu wa vibaraka wao na kusaidia ushawishi wao unaotumikia maslahi yao, ambapo mithili yake ni kama mlaji sanafu wa tende aliyemtengeza jana, kwani uhalifu wote huu wa kimya unafichua madai ya kirongo ya haki za kibinadamu na uhuru.

Magharibi, ambayo imetangaza vita kwa uzito wake wote visivyo na mwisho ili kupitisha miradi chini ya majina ya kuvutia kama vile ukombozi wa wanawake, uwezeshaji wa wanawake, na ulinzi kwa familia, na serikali zote zilizoko katika nchi za Waislamu huitumikia, imenyamazia kimya kukamatwa kwa wanawake sita wa Kiislamu wanaozikimu familia zao, na baadhi yao kuwachunga wazazi wao dhaifu, na wale wanaochunga mjukuu wao mlemavu, na wanaochunga watoto wao wadogo.

Magharibi imejitia upofu kwa uhalifu wa serikali nchini Kyrgyzstan, baada ya kuwakamata wanawake hawa, kama ilivyojitia upofu kukamatwa kwa Zulfiyya Amonova, na kuuwawa kwa babake shujaa, na kujitia upofu kukamatwa kwa Aafia Siddiqui… Wanawake hawa wasafi na watakatifu sio miradi ya kutafutia masoko ya serikali za kihalifu, na hili linaongeza utukufu wao na cheo chao, wala wao sio sehemu ya ajenda duni za Kimagharibi za kuwanyanyasa wanawake na kukiuka hadhi yao mikononi mwa wanawake, na hili linawanyanyua juu ya nyota.

Serikali nchini Kyrgyzstan haitadumu milele, na dhulma haisahauliki, na Mwenyezi Mungu Yupo Milele na wala hafi, na siku itakuja ambapo Ummah utalipizia kisasi dini yake na binti zake.

 [وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ]

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [ash-Shu'araa: 227]

Imeandikwa kwa Ajili ya Idhaa ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bayan Jamal
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

مسلمات_قرغيزستان#   

#KırgızistanlıMüslümanKadınlaraÖzgürlük     

#FreeMuslimahsKyrgyzstan

#WaacheniHuruWanawakeWaKiislamuKyrgyzstan 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 30 Agosti 2020 11:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu