Jumamosi, 04 Rajab 1446 | 2025/01/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tawakkul (Kumtegemea) Mwenyezi Mungu:
Sababu nyuma ya Mafanikio Makubwa ya Umma wa Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Ukisoma historia ya Umma wa Kiislamu, mtu ataona ufunguzi mkubwa ambao ulipitia, ambao hakuna taifa jengine lililowahi kuupata. Waislamu walitoka Bara ya Arabu na kupigana na dola kubwa duniani kwa wakati mmoja, Dola ya Kirumi, Himaya ya Byzantine na Himaya ya Kifursi. Anapoangalia hili mwanzoni mtu atasema: watu hawa wenye kichaa ni kina nani? Waarabu wanatoka kupigana vifua wazi, hawajui silaha walizozijua himaya hizo, na hawana zana wala vifaa zinazomilikiwa na Wafursi na Warumi. Hawana uzoefu wa kupigana kama wa Warumi na Wafursi, walitoka kwa maelfu na kupigana na mamia ya maelfu ya wapiganaji. Basi je (Waislamu) walitegemea nini? Isitoshe, ujasiri wao ulitoka wapi? Walijawa na ujasiri mithili ya jabali imara; wakatoka huku wahakikishiwa na kujiaminisha kuwa Mwenyezi Mungu (swt) atawapa ushindi. Na hivyo hili liliendelea katika zama za Tabi'ina na wafuasi wao na hata katika historia za Kiislamu, kuna hadithi na matukio ambayo yaliwashangaza wasomaji, ambapo Waislamu walipigana kwa zana, vifaa na silaha chache sana kuliko maadui na wapinzani wao, wanagawanya safu, wakaingia ndani ya matatizo; Mwenyezi Mungu (swt) akawafanya washindi juu ya maadui. Maswahaba watukufu, katika miaka michache, waliiangamiza Himaya ya Kifursi, ambayo ilidumu kwa mamia ya miaka, kwa zama na kwa vizazi vingi. Waliishinda Himaya ya Kirumi kutoka Ash-Sham na Afrika Kaskazini, na wakaendelea kupigana nayo mpaka wakaishinda. Walipata wapi azma hii, kwa imani hii? Kuna jibu moja tu la swali hili; kwamba wana kitu katika itikadi yao (aqeedah) ambacho mataifa mengine hawana, yaani, “At-Tawakul ala Allah (Kumtegemea Mwenyezi Mungu),” Tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt) ni kitu spesheli kwa Ummah huu na manabii waliotangulia, wamepewa wao haswa, na mataifa mengine hayaijui. Mataifa yanapigana wao kwa wao kwa vifaa vyao, majeshi, idadi na vifaa. Mataifa yanashindana, watu wenye fikra ya kimada, wasiojua uhusiano na Mwenyezi Mungu, wanashindana tu katika maandalizi ya jeshi, na kwa hiyo mbio za silaha ndicho kitu pekee kinachozingatiwa katika vita vya mataifa hayo. Ama Umma wa Uislamu ni tofauti kabisa. Katika Umma wa Kiislamu, Waislamu wako tayari kupigana vita na wakijua kwamba silaha zao ni ndogo sana kuliko za adui zao. Lakini wanasonga mbele wakimtegemea Mwenyezi Mungu (swt), wamehifadhi maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [47:7].

Aidha, sio kupuuza umuhimu wa maandalizi. Ni wajibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kujiandaa.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَأَعِدُّوا۟ لَهُم مَّا ٱسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍۢ وَمِن رِّبَاطِ ٱلْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِۦ عَدُوَّ ٱللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَءَاخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ ٱللَّهُ يَعْلَمُهُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِن شَىْءٍۢ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ]

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.” [8:60].

[وَأَنفِقُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا تُلْقُوا۟ بِأَيْدِيكُمْ إِلَى ٱلتَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوٓا۟ ۛ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ]

“Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.” [2:195].

Maana ya “kutoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” yamaanisha kutoka katika kujiandaa kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Haya ni maandalizi ya kisilaha; hata hivyo, kinachowatofautisha Waislamu ni kwamba hawaweki maandalizi ya silaha kwanza. Yanakuja ya pili, maandalizi ya kwanza ni ya Iman, itikadi,  maandalizi ya kimaadili na kisaikolojia. Muumini anapokuwa amejizatiti kwa Imani yake, akiwa amejizatiti kwa kumtegemea kwake Mwenyezi Mungu, akiitamani Jannah ambayo ni upana kama mbingu na ardhi, akimtegemea Mola wake Mlezi, akiitumainia amri ya Mwenyezi Mungu, kwa njia hii amejitayarisha kwa hilo, huku adui yake hawezi kujiandaa hata kidogo. Muumini anachanganya maandalizi haya ya kisaikolojia ya imani ya maadili na maandalizi ya kimwili. Yameunganishwa ili kutupa msukumo wenye nguvu zaidi unaojulikana katika historia, nguvu ambazo zimebadilisha sura ya historia. Fahamu ya tawakkul ala Allah haihusiani tu na mada ya Jihad inayofanywa na Dawlat hul Islam (Dola ya Kiislamu), bali kumtegemea Mwenyezi Mungu huambatana na muumini, kama mtu binafsi na jamii, kama ummah na dola katika kila tendo katika kila hali. Ni lazima tumtegemee Mwenyezi Mungu katika kila nyanja ya maisha yetu. Tunaweza tusiwe na msaidizi katika maisha haya, tusiwe nyenzo, lakini tunatoka nje kusema neno la haki, tukiamini kuwa Mwenyezi Mungu atatulipa ujira. Ikiwa Yeye (swt) atatuokoa kutoka kwa adui yetu, basi tumepata ujira wa Mwenyezi Mungu katika ulimwengu huu, au tukutane na Mwenyezi Mungu kwa njia bora kabisa mtu anayoondokea kwenye ulimwengu huu. Tuna imani kwa Mwenyezi Mungu tunapotafuta rizq (riziki/ riziki). Tuna imani kwa Mwenyezi Mungu tunapotafuta ndoa. Tunamtegemea Mwenyezi Mungu tunapotafuta elimu. Tunamtegemea Mwenyezi Mungu tunapobeba Da’wah. Tunaandamana na tawakkul kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yetu yote; kabla ya kazi, wakati wa kazi na baada ya kazi.

Kumtegemea Mwenyezi Mungu ni jambo ambalo Waislamu wote wanaliamini. Hata hivyo, kuna tofauti kati ya wale ambao wana tawakkul kinadharia au wale wanaoamini tawakkul katika nadharia, na wale wanaojua tawakkul ya kweli, wanaifanya na kuitendea kazi. Leo Waislamu wote wanaamini wajibu wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwa sababu yeyote anayekataa kumtegemea Mwenyezi Mungu ni kafiri, kwa sababu anakanusha kipengele kilichokatikiwa katika Dini. “Kumtegemea Mwenyezi Mungu” kumeeleza katika dalili ya kukatikiwa. Qur’an ni dalili ya kukatikiwa, Aya zake zimetuamrisha tawakkul, na Aya hizi ni dalili za kukatikiwa. Lakini tatizo ni kwamba baadhi ya Waislamu hawakuelewa maana ya tawakkul na hivyo hawakumtegemea Mwenyezi Mungu kwa usahihi.

Dalili zinazotaja amri ya kuwa na tawakkul kwa Mwenyezi Mungu ni:

[ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ]

“Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Na juu ya Mwenyezi Mungu nawategemee Waumini.” [64:13]

[وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًۭا]

“Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.” [33:3]

[فَبِمَا رَحْمَةٍۢ مِّنَ ٱللَّهِ لِنتَ لَهُمْ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ ٱلْقَلْبِ لَٱنفَضُّوا۟ مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَٱعْفُ عَنْهُمْ وَٱسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِى ٱلْأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَوَكِّلِينَ . إِن يَنصُرْكُمُ اللهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا ٱلَّذِى يَنصُرُكُم مِّنۢ بَعْدِهِۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ]

“Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea. Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [3:159-160]

[إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتُهُۥ زَادَتْهُمْ إِيمَـٰنًۭا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ]

“Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.” [8:2]

[قُل لَّن يُصِيبَنَآ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوْلَىٰنَا ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ]

“Sema: Halitusibu ila alilo tuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu!” [9:51]

[فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُلْ حَسْبِىَ ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلْعَرْشِ ٱلْعَظِيمِ]

“Basi wakigeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi.” [9:129]

[قُلْ حَسْبِىَ ٱللَّهُ ۖ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ ٱلْمُتَوَكِّلُونَ]

“Sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye wategemee wanao tegemea.” [39:38]

[ٱلَّذِينَ قَالَ لَهُمُ ٱلنَّاسُ إِنَّ ٱلنَّاسَ قَدْ جَمَعُوا۟ لَكُمْ فَٱخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَـٰنًۭا وَقَالُوا۟ حَسْبُنَا ٱللَّهُ وَنِعْمَ ٱلْوَكِيلُ]

“Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa.” [3:173]

Umar (ra) alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akisema: ‏«لو أنكم تتوكلون على الله حق توكله لرزقكم كما يرزق الطير ، تغدو خماصاً وتروح بطاناً»‏‏ “Lau kama nyinyi mungemtegemea Mwenyezi Mungu haki ya kumtegemea, kwa yakini angewaruzuku kama anavyowaruzuku ndege, asubuhi wanatoka wakiwa na njaa jioni wanarudi wakiwa wameshiba”.

Hizi ni baadhi tu ya aya na hadith nyingi zinazoamrisha kuwa na tawakkul kwa Mwenyezi Mungu.

Je, Tawakkul ala Allah (Kumtegemea Mwenyezi Mungu) ni nini?

Katika maana ya kilugha, Tawakkul ni kujisalimisha. Wakati tumeweka utegemezi wetu kwa Mwenyezi Mungu, tumejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, tumemkabidhi suala letu, na tumeliwakilisha kwa Mwenyezi Mungu. Yeye (swt) ni Wakeel (Mlinzi), ambayo yamaanisha, Atasimamia mambo yetu.

Ni wakati gani muumini anakuwa na tawakkul?

Tawakkul ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kumkabidhi jambo na kumtegemea Yeye. Pindi Muislamu anapomfanya Mwenyezi Mungu kuwa Wakeel, Mwenyezi Mungu atasimamia mambo yake. Hii ina maana kwamba tawakkul haipo tu katika hali zote za muumini, bali ni wajib kwamba amtegemee Mwenyezi Mungu katika kila suala. Tawakkul yetu kwa Mwenyezi Mungu inaanza, mara tu tunapomwamini Mwenyezi Mungu na kumchukua kama Mola Mlezi wetu. Na kwa kuwa tumefuata mwongozo wake na kuuomba, hapa ndipo tunapo tunakuwa na tawakkul kwa Mwenyezi Mungu. Tunapofuata mwongozo, tutafanya matendo yetu kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu. Na tunapokuwa na subira kwa amri ya Mwenyezi Mungu licha ya dhiki, shida, na matatizo katika baadhi ya hali, basi utakuwa unamtegemea Mwenyezi Mungu (swt). Na tunapofanya kazi ya kutii amri za Mwenyezi Mungu kwa nia ya kufikia natija, tunaifanya kwa tawakkul kwa Mwenyezi Mungu Azza wa Jal. Tunapomwomba Mwenyezi Mungu atupe mafanikio na ushindi, basi tunategemea (tunakuwa na tawakkul) kwa Mwenyezi Mungu.

Pindi mkulima anapotafuta mbegu za kupanda na kukinai kuwa hazioti isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akipenda, huziotesha kwa sababu Mwenyezi Mungu ameagiza upanzi na upaliliaji, atazitunza na kuzimwagilia maji akiamini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye atupaye mafanikio. Na wakati wa kusubiri ukuaji wake, kwa kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Razzaq (Mtoaji), hivyo kuwa na tawakkul kwa Mwenyezi Mungu; na wakati wa mavuno yake ili kupata faida yake, anaweka tawakkul yake kwa Mwenyezi Mungu; anapopokea pesa na kuzitumia kwa utiifu kwa Mwenyezi Mungu na kumsifu Mwenyezi Mungu katika haya yote anamtegemea Mwenyezi Mungu. Tunapofuata amri za Mwenyezi Mungu na kufanyia kazi matokeo ambayo Mwenyezi Mungu aliamuru kwamba yanapaswa kupatikana, na watu husema, Je, unatarajia kwamba kutokana na juhudi zako kidogo, na nyenzo kufikia matokeo hayo unayotaka?! Anafanya hivyo kwa sababu Mwenyezi Mungu aliamuru hivi. Anakuwa na tawakkul kwa Mwenyezi Mungu. Je, ni waumini wangapi wanaotegemea Mwenyezi Mungu, wamepata matokeo makubwa ambayo watu hawakuyatarajia bila kujali kwamba walikosa rasilimali na ukosefu wa sababu za kimada? Lakini wamefanikisha mambo kwa tawfiq (mafanikio) ya Mwenyezi Mungu na kwa sababu walimtegemea Yeye (swt). Hivyo kumtegemea Mwenyezi Mungu sio maneno tu pekee, sio vile watu wanavyofikiri kwamba unafanya mambo bila kuandaa mbinu za kimada.

Ufahamu wa Tawakkul

Katika suala la tawakkul, watu wamegawanyika katika aina mbili. Baadhi yao wamesema tawakkul ni kwa kutotayarisha nyenzo. Na kumwachia Mwenyezi Mungu (swt), na sio kutafuta rizq (riziki) na sio kutafuta nusra. Mtu wa namna hii husubiri Mwenyezi Mungu ampe kile anachohitaji, kama anavyodai, akiwa na tawakkul kwa Mwenyezi Mungu. Kikundi hiki hakikuelewa tawakkul ipasavyo.

Kwa upande mwingine, kundi la pili lilielewa tawakkul kwa Mwenyezi Mungu kumaanisha kwamba wanachukua nyenzo. Maana ya ‘kumtegemea Mwenyezi Mungu’ ina maanisha, ‘kuchukua sababu za kimada’. Kwa hivyo kulingana na wao, tawakkul ni kuchukua mbinu. Hili pia ni kosa. Kwa nini? Kwa sababu Kumtegemea Mwenyezi Mungu ni ile hali ya Imani, isiyo ambatanishwa katika suala la kuchukua sababu au kwa kuacha sababu, bali ni kwenye kuendelea kabla ya kuchukua sababu, baada ya kuchukua sababu na wakati wa kuchukua sababu. Kuchukua sababu ni jambo ambalo Mwenyezi Mungu alilazimu, na ni njia ya kufikia matokeo na kufikia malengo. Ni njia ambayo Mwenyezi Mungu (swt) alitunga sheria kwa ajili ya mwanadamu; kuchukua sababu, kutafuta vitu, kufuata njia inayoongoza kwenye kufikia malengo. Lakini wajibu huu ni tofauti na tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt). Watu wengi wanachanganya Hadith ya Mtume (saw) ambayo anasema, Anas bin Malik amesimulia kwamba mtu mmoja alisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je, nimfunge (ngamia) na nimtegemee Mwenyezi Mungu?" au ni mwachilie na nimtegemee Mwenyezi Mungu?” Akasema:

«اعْقِلْهَا وَتَوَكَّلْ»

“Mfunge na utawakkal (kwa Mwenyezi Mungu).”

Wanasema Mtume (saw) amehusisha vitendo na tawakkul. Hadith hii inazungumza juu ya mtu mmoja ambaye alimuuliza Mtume (saw) alipokuwa karibu kuingia msikitini na ngamia wake, nini cha kufanya na ngamia? Alimuuliza Mtume (saw), “Je, nimuachilie na niwe na tawakkul? Au nimfunge na niwe na tawakkul? Katika riwaya nyingine, “Je, nimwachilie na niwe tawakkul? Au nimfunge na niwe na tawakkul? Mtume (saw) akasema: “Mfunge ngamia wako na ufanye Tawakkul”. Hadith hii ilikuwa ni jibu kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa yule mtu aliyemuuliza, je, kuamini kunamaanisha kwamba sichukui sababu? Au nichukue sababu pamoja na tawakkul? Mtume (saw) alieleza tawakkul kwa Mwenyezi Mungu haipingani na kuchukua sababu. Hadith hii haimaanishi tawakkul maana yake ni kuchukua sababu. Badala yake, hii inaeleza kwamba kuchukua sababu ni wajibu na kumtumaini Mwenyezi Mungu ni wajibu. Na pale jambo lilipochanganyikiwa, au pale mtu huyo alipochanganyikiwa na kufikiri au kukaribia kufikiri kwamba tawakkul maana yake ni kuacha sababu, Mtume (saw) alimuongoza. Wengine walielewa Hadith hiyo kuwa na maana ya kuchukua sababu, kwamba unafanya kazi kisha utawakkal. Wengine walijitenga na maana ya Hadith hii na wakasema kwamba tawakkul ni baada ya kazi. Hili ni kosa kubwa kwa sababu tawakkul ni hali inayoambatana na muumini katika kila hali.

Hii ndiyo maana ya tawakkul, ambayo huambatana na muumini kwani ameongozwa kwa utiifu wa Mwenyezi Mungu, kwa imani kwa Mwenyezi Mungu Azza wa Jal. Na kwa kuwa aliamua kutii amri za Mwenyezi Mungu (swt) na kufanya matendo yake yote kulingana na maagizo na makatazo ya Mwenyezi Mungu. Tawakkul itaonekana waziwazi kwa muumini, anapotekeleza utiifu kwa Mwenyezi Mungu licha ya matatizo, magumu, vitisho, idadi kubwa ya maadui, ukosefu wa nyenzo, muumini ana tawakkul mradi tu ni kuitikia amri za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametuamuru kuinusuru Dini yake, na akatuahidi kwamba tukiinusuru Dini yake, Yeye atatunusuru.

[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [47:7]

Katika uhalisia wetu, watu wengi huuliza au kutilia shaka kwamba, je Ummah huu utakuwa ni mshindi? Vipi hali ya Ummah itabadilika au tutaweza kuibadilisha, wakati mataifa ya ulimwengu yanapanga njama dhidi yake? Wanasema: Je, huoni yale ambayo dola kubwa za ulimwengu ziliyafanya, kuanzia Amerika hadi Urusi, Uingereza hadi China. Je, huoni walichowafanyia Waumini, Waislamu walipo waasi watawala wao! Angalieni Syria, Iraq n.k angalia jinsi muungano wa maadui ulivyoungana dhidi yetu kutoka kila upande ili kuzuia mwamko wetu, kuzuia ukombozi wetu, tunawezaje kubadili hili? Hali hii ya kukata tamaa, ya kuchanganyikiwa ambayo imewafanya watu wengi kusema kwamba hakuna matumaini kwa Ummah huu kuamka isipokuwa kwa kudhihiri Mahdi! Iwapo watu wote walifikiri hivi, basi vipi Mahdi angetokea! Kwa sababu Mahdi ni mmoja wa watu hawa. Yeye si mtume, wala si malaika anayeshuka kutoka mbinguni. Yeye ni mmoja wa wanadamu. Yeye ni mmoja wa viongozi wa waumini, fikra hii, ambayo haionyeshi tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt) hata kidogo inaongoza waumini kwenye hali ya kufazaika, hali ya kukata tamaa. Ilhali lau wangemtegemea Mwenyezi Mungu (swt) vyema na kuelewa maana ya tawakkul kwa Mwenyezi Mungu, wangekuwa na hakika kwamba ikiwa wangefanya yale waliyoamriwa kufanya, wangestahili ushindi wa Mwenyezi Mungu na Yeye (swt kisha atawapa ushindi na baada ya ushindi, Mwenyezi Mungu atawapa tamkini. Hii ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Ni nani angefikiri kwamba pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipo tumilizwa, mtu huyu angeweza kubadilisha sura ya historia kwa mpepeso kutoka siku hiyo? Wengine wanaweza hata kusema, Yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na manabii wanasaidiwa na miujiza. Hapana! Mtume (saw) hakusaidiwa na miujiza hiyo peke yake, bali alipambana, na kuumizwa, na kupigwa mawe na miguu yake mitukufu ikatoka damu. Alifukuzwa katika nchi, akapigwa vita, na watu wake hawakukubali ulinganizi wake isipokuwa wachache tu, lakini kwa sababu Mwenyezi Mungu anataka kutufundisha, alituonyesha jinsi watu wa Madina walivyosilimu kupitia swahaba mtukufu aitwaye Mus'ab ibn Umair (ra), ambaye alijifunza tawakkul juu ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Mwenyezi Mungu (swt) alileta nusra kupitia mikono yake. Kabla ya watu wa Madina kusilimu na kumpa Mtume (saw) mamlaka yao, Mtume (saw) na maswahaba zake walihamishwa katika ardhi na kuteswa kwa mateso makali zaidi; lakini tawakkul yao juu ya Mwenyezi Mungu iliwafikisha kwenye yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwaahidi

[وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ كَمَا ٱسْتَخْلَفَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ ٱلَّذِى ٱرْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّنۢ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًۭا ۚ يَعْبُدُونَنِى لَا يُشْرِكُونَ بِى شَيْـًۭٔا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [24:55]

Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Tunapotimiza wajibu wetu, tunafanya kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu, tukimtegemea Mwenyezi Mungu, tukifuata yale yote anayotuamuru kuyatii kupitia hukmu na kuchukua sababu, kusonga mbele, kwa kuwa na imani kwa Mwenyezi Mungu, tukimkabidhi yeye, hapo ahadi ya Mwenyezi Mungu itapatikana InshaAllah.

Nani angefikiri kwamba mtu (Mtume) anayetawala mji (Madina) angetuma ujumbe kwa wafalme wa ardhi hii: kwa Hiraqla, kiongozi mkuu wa Warumi; kwa Kisra, kiongozi mkuu wa Fursi; kwa Muqawqis, kiongozi wa Makubti? Je, mtu asiyejua maana ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, anaweza kutuma ujumbe kwa wafalme wa dunia, anapotawala mji? Kuwataka wafalme wa dunia, ««أَسلِمْ تَسلَمْ؛ يُؤْتِكَ اللهُ أجرَك مرَّتينِ؛ فإن تولَّيْتَ فإنَّ عليكَ إثمَ الأريسيِّينَ “Silimuni na mtaokoka, na Mwenyezi Mungu atakulipeni ujira mara mbili, musipofanya hivyo mutabeba dhambi ya watu wenu na taifa lenu.” Kiongozi wa mji wenye wafuasi wachache wa makabila ya Waarabu anatuma kwa wafalme wa ardhi, kabla hata ya ufunguzi wa Makka na Tai’f, kabla Uislamu haujaenezwa katika Bara Arabu. Ilikuwa ni tawakkul juu ya Mwenyezi Mungu iliyofanikisha hili. Vita vingi, sio tu wakati wa Mtume (saw), wakati wa Khulafah (makhalifa) walioongoka na zama za makhalifa baada yao wakati wa Bani Umayya, Abbas, Mamluk, Ayyubi, Seljuk na Uthmani, ambapo jeshi dogo linashinda majeshi makubwa. Ni kipi kilikuwa ndio nguvu ya kumsukumo huo? Ni kipi kiliwapa ushindi? Ni tawakkul kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Leo, tumeamrishwa kusimamisha dola ya Dini hii yenye kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha  Mwenyezi Mungu, kuregesha ubwana kwa Sheria ya Mwenyezi Mungu katika nchi na kuregesha mamlaka ya Umma, kuregesha umoja wa Ummah, kurudisha kubeba ulinganizi wa Uislamu kama ujumbe kwa ulimwengu mzima. Je, tunaweza kufanya hivyo? Ndiyo, mradi tu ni amri ya Mwenyezi Mungu, hii ina maana kwamba tunaweza kwa sababu Mwenyezi Mungu hatuamuru tusichoweza kukifanya. Hatuwezi kufikia hili sasa, lakini tunapaswa kujiandaa kulingana na yale ambayo Mwenyezi Mungu ameamuru, tukiwa na utegemezi (tawakkul) kwa Mwenyezi Mungu. Yeye (swt) ameuahidi Ummah huu tamkini. Sisi kama Waislamu tunapaswa kujua kwamba tukifuata agizo la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atatunusuru kwa kile tulichopungukiwa na nguvu za kimada. Je, Mwenyezi Mungu (swt) hakutuma kwa waumini wa Badr mamia ya Malaika safu baada ya safu? Malaika walipigana pamoja na waumini katika Badr, pia wanapigana na waumini dhidi ya maadui kila wakati waumini wanapofanya walichoamrishwa na hawavunji amri ya Mwenyezi Mungu na wakati muumini anafanya kazi ya kuifanya Dini ya Mwenyezi Mungu kuwa ya juu zaidi, kuimarisha Dini ya Mwenyezi Mungu duniani. Muumini anajua kwa yakini na ana utegemezi (tawakkul) kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwamba Yeye (swt) atatimiza yale ambayo Mwenyezi Mungu ameamuru ikiwa sio sasa, basi kesho, ikiwa sio kesho basi keshokutwa. Lakini Waumini wahuhesabu mambo kimada pekee, Mwenyezi Mungu hataleta ushindi na Umma hautafikia lengo lake. Umma haukupata ushindi katika historia kwa kuandaa zana na nyenzo pekee, bali ilikuwa ni kwa sababu ya Imani yake kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuwa na tawakkul kwake. Hii ndiyo maana ya kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt).

Wale wasio na tawakkul, waliosahau kumtegemea Mwenyezi Mungu walisema: ni lazima tuache kitu cha dini yetu; ni lazima tufuate baadhi ya sheria za jumuiya ya kimataifa na kutekeleza baadhi ya fikra na fahamu zake ili kuwaridhisha. Tunapaswa kukubali sheria ya kimataifa, katiba ya Umoja wa Mataifa. Tunakubali kuwa dola iliyo na mipaka. Tunakubali kufuata yale ambayo adui yetu anayataka kwa ajili yetu kwa sababu hatuwezi kuondoka kutoka kwa nguvu hii kubwa, hatuishi peke yetu katika ulimwengu huu. Kauli mbiu hizi zimekuwa kisingizio cha watu kuacha Dini yao. Wanasema: Hatuwezi kusimamisha Dola ya Kiislamu inayotawala kwa Uislamu wote, lazima tukubali maafikiano mwanzoni, na tutawale kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu hajayateremsha, tukubali kutabanni mfumo wa kibepari. Hii si njia sahihi ya kufikiri na kutenda. Sisi kama Umma wa Uislamu, tumeamrishwa kufuata mfano wa Mtume (saw):

[لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِى رَسُولِ ٱللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌۭ لِّمَن كَانَ يَرْجُوا۟ ٱللَّهَ وَٱلْيَوْمَ ٱلْـَٔاخِرَ وَذَكَرَ ٱللَّهَ كَثِيرًۭا]

“Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.” [33:21]

[قُلْ هَـٰذِهِۦ سَبِيلِىٓ أَدْعُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِى ۖ وَسُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ]

“Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.” [12:108]

Je, ni mfano wa Mtume (saw) kwamba viongozi wa Waislamu wanashirikiana na makafiri dhidi ya Waislamu? Je, ni mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba mtawala anadai kuwa yeye ni mcha Mungu lakini anatawala kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu hakuyateremsha, kutoa leseni za madanguro, kufungua fuo za watu kutembea uchi, na kuwa mwanachama wa muungano wa kimataifa unaopiga vita Waislamu kila mahali? Je, huu ndio mfano wa Mtume (saw)? Muumini anapataje ushindi kwa kutomtii Mwenyezi Mungu? Inakuwaje kufuata njia ya makafiri kupelekee kwenye ushindi wa Ummah?

Udhaifu wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, au kukosekana kwa maana ya tawakkul kwa Mwenyezi Mungu, au ufahamu wa makosa wa tawakkul kwa Mwenyezi Mungu imetutengenezea makundi ya wale wanaodai kwamba wanainusuru Dini ya Mwenyezi Mungu, lakini kupitia kukiuka sheria ya Mwenyezi Mungu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie kumtegemea Yeye kwa njia iliyo bora zaidi, aufundishe Ummah huu na atusaidie kuwasiliana na Ummah huu. Hii ndiyo maana na uhalisia wa utegemezi (tawakkul) kwa Mwenyezi Mungu ambayo itauwezesha Ummah kufuata njia iliyo sawa na kumchukua mtume wake kuwa mfano katika kuinusuru Dini hii na kuisimamia na kuitia nguvu duniani na kwa ajili ya ushindi wa Dini ya Mwenyezi Mungu na waja Wake. Tunaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na rehema na amani zimshukie bwana wetu Muhammad (saw) na jamaa zake na maswahaba zake na wale wanaofuata mwongozo wake hadi Siku ya Kiyama.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Hameed Bin Ahmad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu