Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuibuka kwa Eneo la Kusini mwa Dunia

(Imetafsiriwa)

Eneo la Kusini mwa Dunia liko katika fesheni; Kila mmoja hatosheki. China na Urusi zinasema kuwa wao ndio mustakbali na wanaomba msaada wao na Magharibi ambao kwa muda mrefu waliwapuuza sasa wanawaona kama muhimu ili kudumisha mustakabali huria. Huku mizani ya nguvu za kilimwengu ikiyumba muundo wa mustakbali wa uchumi wa kilimwengu kwa mujibu wa wengi utahitaji kulizingatia Eneo la Kusini mwa dunia.

Siasa za jadi za Kijiografia zimeuangalia ulimwengu kihistoria kutoka kwa dhana ya Mashariki-Magharibi. Mataifa tajiri zaidi duniani, majeshi makubwa  zaidi na mataifa yaliyofanikiwa zaidi yako huko. Hii kawaida kimsingi ilitokana na njia yao ya kuivinjari mito ambapo iliruhusu biashara na mawasiliano. Mataifa ambayo yanaishi katika eneo la Kusini mwa Dunia yaliona mahusiano yao muhimu na ushindani kuwa katika eneo la kaskazini na hii ndio sababu yalikuwa na mtazamo wa mashariki-magharibi.

Eneo la Kaskazini mwa Dunia hivyo basi linakusudia mataifa yaliyo endelea kiviwanda na tajiri huku eneol la Kusini likikusudia mataifa yanayoendelea ambayo tofauti na Kaskazini yana uchumi wa kibidhaa badala ya uchumi wa kiviwanda na huduma. Uchumi wa ulimwengu kwa miaka 500 iliyopita unapendelea eneo la Kaskazini na ulijengwa nalo, huku kihistoria eneo la Kusini mwa Dunia limekuwa na sifa ya kiwango cha juu cha tofauti ya kiuchumi.

Mataifa ya Kusini mwa Dunia ndio ambayo yamezingatiwa kwa muda mrefu kuwa pembeni ya mfumo wa siasa za kijiografia. Wao hujibu matukio badala ya kuyaendesha. Wakati ulimwengu wa ncha mbili (bi-polar) ulipoibuka baada ya WW2 ulimwengu ukawa uwanja wa vita kati ya Umoja wa Soviet na Marekani ambao wote walitaka kupanua ushawishi wao na kuingiza ulimwengu katika kambi zao. Mataifa mengi ya ulimwengu yalikuja kuona vita hivi kama tishio kwa uhuru wao wa kujitawala. Huku wakiziona dola zote mbili kuwa muhimu kwa fedha na silaha, hawakuweza kufanya chochote nje ya mfumo wa kilimwengu au hata kubaki bila kuwa upande wowote.

Katika muktadha huu harakati zisizoegemea upande wowote ziliibuka, na G-77 iliibuka kushughulikia changamoto za kiuchumi. Wote hawakufanikiwa sana kwani walikuwa na ushawishi mdogo juu ya matukio ya kilimwengu. Kudumaa, ukosefu wa ajira na mgogoro wa kifedha katika miaka ya sabiini ilisababisha wengi kukusanya deni mnamo miaka ya sabiini na wakati Vita Baridi vilipomalizika eneo la Kusini mwa Dunia lilibaki kutengwa katika mfumo wa siasa za kijiografia wa baada ya Vita Baridi.

Pamoja na mfumo huria wa kilimwengu kudhoofika na mfumo wa uchumi wa ulimwengu ukitumikia tu eneo la Kaskazini mwa Dunia mataifa kadhaa kutoka eneo la Kusini mwa Dunia na uchumi wao wa bidhaa yanataka kuchukua njia tofauti. Brazil na India zimeibuka kama viongozi kwenye uwanja. India ni muhimu kwa Urusi kutoka kwa mtazamo wa kiuchumi na muhimu kwa Marekani kisiasa. Uchumi wa unaoegemea bidhaa wa Brazil umekuwa muhimu kwa China na vile vile Ulaya. Wakati huo huo, mataifa ya Asia ya Kati yanachumbiwa na Urusi, Uturuki, China, Marekani na Ulaya.

Ushindani unaoibuka kati ya eneo la Kusini mwa Dunia ni kuona ushindani kati yao ukipendelea eneo la Kusini mwa Dunia. Kwa zaidi ya miaka 500 iliyopita Kaskazini mwa Dunia ilitawala siasa za ulimwengu na uchumi na kuweka sheria za kushirikiana na Kusini mwa Dunia. Kwa kuendelea mbele Kaskazini mwa Dunia inakabiliwa na changamoto za idadi ya watu na kiuchumi kaskazini itategemea zaidi Kusini mwa Dunia. Uhalisia huu wa siasa za kijiografia uliifanya Ufaransa kutoa pendekezo la kuhudhuria mkutano wa kilele wa BRICS mnamo Agosti 2023, lakini Xi Jinping akakataa ofa hiyo.

Japan ilichapisha hati mnamo 2023 ambayo ilionyesha umuhimu unaokua wa eneo la Kusini mwa Dunia kwa mfumo wa kimataifa. Karatasi yake nyeupe juu ya uchumi wa kimataifa na biashara iligawanya uchumi wa ulimwengu katika kambi tatu: Magharibi, ikiongozwa na Marekani, Mashariki, ikiongozwa na China na Urusi; na mataifa yasiyo upande wowote. Ilisema kwamba ujenzi na kuimarisha ushirikiano na Kusini mwa Dunia Global ilikuwa ni kipaumbele, kwa msisitizo fulani juu ya India.

Je! Eneo la Kusini mwa Dunia linaweza kuwa mlingoti mpya ulimwenguni? Kusini mwa Dunia inakabiliwa na changamoto kadhaa katika kufanikisha hili. "Kusini mwa Dunia" haina uhalisia wa kisheria au wa kisiasa, ni urahisishaji tu. Maingiliano mengi ya eneo la Kusini mwa Dunia hufanyika katika kiwango cha nchi mbili. Mataifa mengi ya Kusini  mwa Dunia yanakabiliwa na ukosefu wa utulivu wa ndani, ambapo ni kikwazo kikubwa katika kupatiliza fursa ya mitindo inayoibuka. Ikiwa Kusini mwa Dunia ingeanza kuchukua hatua kwa ulimwengu badala ya kuishi kwa huruma ya Kaskazini, hii ingeashiria mabadiliko makubwa katika karne ya 21.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdurrahman Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu