Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kauli Mbiu Tupu na Miito ya Faragha

(Imetafsiriwa)

Wakati wa simu ya faragha kati ya Benjamin Netanyahu na Joe Biden, Netanyahu alisisitiza maoni yake ya awali kuhusu kukataa wazo la kuunda dola ya Palestina. Netanyahu amesema hivi karibuni, “Sitalegeza msimamo juu ya udhibiti kamili wa usalama wa 'Israel' kwenye eneo lote la magharibi mwa Mto Jordan - na hili linaenda kinyume na dola ya Palestina.”

Vyombo vya habari viliripoti kwamba majadiliano yalihusu zaidi dola ya mustakbali ya Palestina ambayo haina uwezo wa kijeshi, wazo ambalo Biden aliliona kuwa la “kuvutia”. Mazungumzo hayo yalisifiwa kuwa mazito na ya kina, yakilenga sifa za dola ya baadaye ya Palestina ambayo itahitaji mazungumzo. Hata hivyo, Netanyahu amesema ‘Israel’ lazima ipigane hadi ipate “ushindi kamili”. Kwa hiyo, wakati huo huo, mauaji ya halaiki yataendelea.

Mazungumzo haya yalifanyika wiki moja baada ya makumi ya maelfu ya waandamanaji kukusanyika katikati mwa jiji la D.C. ili kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza na kusitisha msaada wa Marekani kwa umbile la Kizayuni. Waandamanaji walionesha bendera na kuimba miito kama “Iacheni Huru, iacheni huru Palestina”, wakiwa na mabango yanayoliita umbile la Kizayuni “Dola ya Ubaguzi wa Rangi” na Rais Biden, “Joe wa Mauaji ya Halaiki”. Tuhma kali zilirushiwa Marekani na wazungumzaji wengi waliita himaya ya kikoloni ya mauaji ya halaiki yenye historia ndefu ya kujihusisha na vitendo vya mauaji ya halaiki na ukoloni.Yote haya ni kutia shinikizo kwa utawala wa sasa ili kuokoa sura yake.

Sasa, utawala wa Biden unajiondoa kwenye tuhma za mauaji ya halaiki kwa kusema kwamba wako kwenye “mazungumzo”. Kutoelewana hadharani kati ya Biden na Netanyahu juu ya mustakabali wa Gaza na suluhisho la dola mbili sasa kunatokana na kuziba pengo kati ya maoni yao tofauti. Kwa hivyo, huku Gaza ikiteketea, mazungumzo na nyimbo zote zimezunguka pambizoni mwa mustakabali wa dola ya Palestina na usitishaji mapigano.

Hii ni fursa kwa Waislamu wa nchi za Magharibi kuwakumbusha wote kwamba, suluhisho la mauaji hayo ya halaiki linatokana tu na ukombozi kamili wa Palestina kutoka kwa uvamizi uliopo. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءَتْ مَصِيرًا]

“Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu!” [4:115].

Suluhisho la kweli kama ilivyoainishwa na Uislamu lipo katika kuhamasishwa majeshi ya Waislamu ili kutoa nusra kwa Palestina na watu wake. Huu ni wajibu kwa majeshi ya Waislamu. Biden wala Netanyahu hawana haki ya kujadili jinsi na ni hatua gani zinahitajika kumaliza mzozo huu. Masuluhisho ya kusitisha mapigano, dola moja au dola mbili ni mijadala inayokuzwa na wasiojua au wapinzani.

Ukombozi pekee wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ndio unaokubalika. Kuacha sehemu yoyote ya ardhi hii chini ya kukaliwa kimabavu ni haramu. Zaidi ya hayo, kuegemeza uzalendo uliolemaa katika ardhi iliyolowa damu ya mashahidi wasiohesabika ni usaliti kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na waumini. Ni muhimu kwamba sisi, kama jamii ya Kiislamu, tuwasilishe masuluhisho ya kweli na kukomesha mikono na ndimi zinazoingilia kati.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu