Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Usaliti Kwenye Ardhi Tukufu ya Bara Arabu

Tukiwa tumeingia ndani ya mwezi mtukufu wa Dhul-Hijjah tuna kumbushwa juu ya kujitoa muhanga kwa Kipenzi cha Mwenyezi Mungu, Ibrahim (as) alipomuwacha mwanawe na mke wake katika jangwa baina ya Safa na Marwa. Tunakumbuka kwamba miaka kadhaa baadaye Yeye na mwanawe Ismael (as) walijenga Al-Ka’bah. Tunakumbuka namna Ibrahim (as) alivyompiga Shetani na ni katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuwa alikuwa tayari kumtoa muhanga mtoto wake bila kusita.

Ilikuwa ni katika ardhi hii hii tukufu ambayo ilishuhudia mapambano ya Haki na Batili katika Da’wah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akiwakabili Maquresh. Alifanya Da’wah hadi alipopata Nusrah na kufanya Hijra Yathrib ambayo ikawa ndio dola ya mwanzo ya Kiislamu, ikaitwa baadaye Madinah al Munawwara, mji wa Nuru. Mji wa dola ambao iliwatawala watu wake kwa yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Haukupita muda mrefu dola hii ikaenea eneo lote la Hijaz na Najd na kufika Yemen kwa upande wa kusini na mipaka ya Sham kwa upande wa kaskazini. Ardhi hii iliobarikiwa imeshuhudia Ufunguzi wa Makkah (Fathi Makkah) na kuvunjwa kwa masanamu yaliowekwa ndani ya Kaaba. Imeshuhudia mwaka wa wajumbe ambapo makabila ya Arabuni yalijisalimisha kwenye Uislamu. Ardhi hii iliobarikiwa imekuwa na hadhi maalum, ambapo Dini mbili hazikubaliwi, kama ilivyopokewa katika kitabu cha Muwatta cha Imam Malik, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,                   

«لاَ يَجْتَمِعُ دِينَانِ فِي جَزِيرَةِ الْعَرَبِ»

"Hazichanganyiki dini mbili ndani ya Bara Arabu"

Malik amesema kuwa Ibn Shihab amesema, “Umar ibn al-Khattab alitafiti juu ya habari hii hadi akapambanukiwa kwa uwazi kuwa Mtume (saw) amesema,

«لاَ يَجْتَمِعُ دِينَانِ فِي جَزِيرَةِ الْعَرَبِ»

"Hazichanganyiki dini mbili ndani ya Bara Arabu" Na hivyo akawafukuza Mayahudi kutoka Khaybar.”

Kutokana na ujumbe wake SAW kumalizika kwa ushindi wa Uislamu, ardhi hii takatifu imeshuhudia kuondoka kwa mbora wa viumbe SAW, ikiwa ni huzuni kwa Ummah wake SAW. Ardhi hii takatifu imeshuhudia Mitume waongo walioangamizwa na Khalifah Abubakar as-Siddiq (ra). Ilishuhudia Khilafah Rashida, na kufuatiwa na utawala wa Kiislamu kwa karne nyingi. Ardhi takatifu imeshuhudia mapenzi ya Ummah na kuwajibika kwa Makhalifah katika kusimamia utawala wa Kiislamu juu yao.

Usaliti wa mwanzo ulishuhudiwa wakati Sharif Hussein na Ibn Saud wote wakishirikiana na Uingereza kwa ahadi ya kupata mamlaka juu ya ardhi hizi takatifu. Walikula njama dhidi ya Ummah na Dini na wakasaidia kuiangusha Khilafah ya Uthmani na hivyo kumaliza utawala wa Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ardhi hii iliobarikiwa. Karne iliyopita ilishuhudia utiifu wa ufalme wa Saudia kwa Uingereza na baadaye maslahi ya Amerika, kwa kipindi chote wakiinajisi ardhi iliobarikiwa kwa kutabikisha ukafiri. Utawala saliti uliruhusu vikosi vya Amerika kuingia katika ardhi hizi tukufu “kuikomboa” Kuwait mwaka 1991 na kuivamia Iraq 2003. Waovu (hao) wameendeleza vitisho kwa watu wa Yemen, ambapo vita vikiwa katika mwaka wake wa 6, vimewaacha watu wa Yemen wakiwa katika hali mbaya zaidi isiowahi kushuhudiwa.

Kana kwamba haya hayatoshi, utawala wa Saudia umemkhini Mwenyezi Mungu kwa kuruhusu matamasha ya kipuuzi na uchafu wa wanamuziki wa kimagharibi na wachezaji densi kuwaharibu vijana. Kama hili halitoshi mapema mwezi huu, Vogue Arabia iliandaa shughuli ya upigaji picha kwa wingi (photoshoot) iliyojumuisha wanamitindo wakuu mashuhuri wa kimataifa, wakionyesha uchafu jirani na msikiti mtukufu wa Madinah. Nini kingetarajiwa kutoka kwa wasaliti hawa waliozuia Hijja kwa Ummah wa Kiislamu, licha ya utajiri mkubwa na vifaa walivyonavyo? Wanaojiita Watumishi wa Misikiti Miwili Mitukufu hawawezi na hawataki kuwezesha utekelezwaji wa nguzo ya Uislamu isipokuwa tu kwa Mahujaji wachache wenyeji, lakini wamehiyari kuwezesha uchafu kwa jina la maendeleo.

Enyi Ummah uliobarikiwa wa Mtume aliyebarikiwa (saw), tunashuhudia usaliti huu juu ya ardhi hii iliobarikiwa na moyo wenu unachuruzika damu, lakini bado mumebaki kimya kwa usaliti huu. Kumbuka kwamba Mwenyezi Mungu ametupa sisi ushindi juu ya mataifa mengine.

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya Ummah waliotolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Sura Al-Imran: 110].

Katika mwezi huu mtukufu ni lazima tutimize utukufu huu na jukumu hili. Na tutimize amri hii na tuwe sehemu ya chama kikubwa kabisa cha siasa cha Kiislamu ulimwenguni chenye kufanya kazi ya kuhuisha Dini ya Mwenyezi Mungu kupitia usimamishaji wa Khilafah, Hizb ut Tahrir. Sisi sote katika mwezi huu mtukufu tufanye kazi ya kusimamisha tena dola ya Khilafah kuwa miongoni mwa amali zetu njema kwa ajili ya Akhera yetu. Ni Khilafah pekee katika njia ya Utume itakayo safisha ardhi hii tukufu kutokana na uchafu wa ukafiri na kuikomboa na watu wake kutokana na wasaliti wanaotumikia Wamagharibi. Ni Khilafah ndio itakayoregesha Hijja katika njia yake ya sahihi na kukomesha ukandamizaji katika ardhi zilizobarikiwa za Sham na Yemen.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Maryam Ansari – Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu