Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Rambirambi kutoka Hizb ut Tahrir, kwenda kwa Mashahidi wa Matetemeko ya Ardhi, yaliyoikumba Uturuki na Syria
(Imetafsiriwa)

(الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ * أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ)

“Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.” [Surah 2:156-157]

Kwa ndugu na dada wapendwa, kwa wabebaji wa Da’wah nchini Uturuki na Syria, na kwa wabebaji Da’wah kwa jumla...

Kwa familia zenye subira na kujikaza nchini Uturuki na Syria, na kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla...

Hizb ut Tahrir inatoa rambirambi kwa mashahidi wa matetemeko ya ardhi yaliyozikumba Uturuki na Syria. Hizb ut-Tahrir inamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awarekodi, pamoja Naye, kama mashahidi wa Akhera, wakithibitisha Hadith iliyopokewa na Bukhari na Muslim, kutoka kwa Abu Hurairah (ra), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«الشُّهَدَاءُ خَمْسَةٌ الْمَطْعُونُ وَالْمَبْطُونُ وَالْغَرِقُ وَصَاحِبُ الْهَدْمِ وَالشَّهِيدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ»

“... Mashahidi wapo aina tano: Mwenye kufa kwa ugonjwa wa tauni, mwenye kufa kwa maradhi ya tumbo, mwenye kufa maji, mwenye kufa chini ya kifusi, na anayekufa katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.” [Bukhari na Muslim]. Aliyepondwa maana yake ni yule anayekufa chini ya kifusi cha ubomozi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Mtukufu na Aliye juu zaidi, awajaalie nafuu ya haraka waliojeruhiwa na walioathirika, kiasi ya kuwa kupona kwao kuwe kwa haraka kikamilifu, ambako hakutaacha nyuma alama yoyote ya majeraha au maradhi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba wale walionusurika kwenye mkasa huu waendelee na maisha mema, wayatumie katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na katika kumtii Mtume wake (saw), kutokana na neema na fadhila za Mwenyezi Mungu.

Mkasa wa tetemeko hili la ardhi ulidhihirisha kwamba Uislamu umedumu kwa kina ndani ya Waislamu. Walipokuwa wakiwaokoa ndugu zao kutoka chini ya vifusi, Waislamu walipiga takbira. Takbira hizi hazikukoma katika ndimi zao, hasa walipokuwa wakimuokoa mtoto mchanga, ambaye mama yake alimzaa, kisha akafa chini ya vifusi, huko Gaziantep, katika Wilaya ya Afrin ... au walipokuwa wakijaribu kumtoa mwanamke kutoka chini ya jengo lililobomoka huko Jindires, mwanamke huyo aliomba afinikwe kichwa chake, kabla ya kutolewa nje, ili nywele zake zisiwe wazi ... au wakati yule aliyeita akiwa chini ya vifusi katika jiji la Kahramanmaraş ili kumtoa nje, aliomba kwanza maji ili atawadhe kabla ya Swalah, ili wakati wa swala usije ukampita... Na wakati wote huo takbira zilisikika, Allahu Akbar... Allahu Akbar...

Muumini si kama watu wengine, kwa kuwa anajua kwamba Qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt) ni ya mwisho na anajua Qadhaa hiyo ilikuja kwa sababu ya hekima ambayo Mwenyezi Mungu (swt) Peke Yake ndiye Anayejua. Kwa hiyo, Muumini huvumilia kwa yale yanayomsibu, akitafuta Radhi (Ridwaan) ya Mola wake Mlezi (swt), kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kutoka kwa Suhaib (ra),

«عَجَباً لِأَمْرِ الْمُؤْمِنِ إِنَّ أَمْرَهُ كُلَّهُ خَيْرٌ وَلَيْسَ ذَاكَ لِأَحَدٍ إِلَّا لِلْمُؤْمِنِ إِنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فَكَانَ خَيْراً لَهُ وَإِنْ أَصَابَتْهُ ضَرَّاءُ صَبَرَ فَكَانَ خَيْراً لَهُ»

“Ajabu ni kwa jambo la muumini hakika kila jambo lake huwa ni kheri na hilo halipatikani isipokuwa kwa muumini; akisibiwa na jambo la kufurahisha akishukuru huwa ni kheri kwake na akisibiwa na jambo la madhara akisubiri huwa ni kheri kwake.” [Muslim]

Maafa yanatokea na kuzisibu nchi za Kiislamu. Hakuna nchi yetu yoyote isiyo na misiba: matetemeko ya ardhi na mafuriko, ukame na ukosefu wa mazao, vita na mapigano, umasikini na njaa... Ingawa majanga ya kimaumbile yanayojulikana yako ndani ya mzunguko wa Al-Qadhaa, kuchukua tahadhari zinazohitajika na kuwajali Waislamu, bila ya uzembe, ni faradhi kwa dola inayosimamia mambo yao. Lau Waislamu wangekuwa na dola ya Khilafah, ingewaunganisha wao na mambo yao. Ingewafariji katika misiba yao. Ingewaondolea mizigo na kushughulikia mambo yao. Ingeipeleka mikono yao kwenye kila lililo jema. Ingetekeleza wajibu wake, pasi na haja ya msaada wa wengine isipokuwa Waislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) awarehemu wafu wetu. Mwenyezi Mungu (swt) awaponye majeruhi wetu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awe Mlinzi wa manusura wa janga hili. Tunamalizia kwa tuliyo anza nayo... Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ * أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ)

“Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.” [Surah 2:156-157]. Hakika, sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Amiri wa Hizb ut Tahrir

18 Rajab 1444 H

9 Februari 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu