Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Salamu kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kwa Wanaozuru Kurasa zake za Mtandaoni kwa Mnasaba wa
Idd ul-Adha Iliyobarikiwa ya Mwaka 1443 H sawia na 2022 M
(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na swala na salamu zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu na jamaa zake na wanaomfuata, na baada ya swala na salamu:

Kwa Umma wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu aliukirimu na kuusifu kama:

 (كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ)

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu. [Aali ‘Imraan: 110].

Kwa wabebaji wa Da’awah walio safi na wachamngu, na wala hatujaribu kumtakasa yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu, wale wanaozungumza maneno mazuri na wakatenda mema, kisha Mwenyezi Mungu akawasifu wale wenye sifa hizi:

 (وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ)

Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu? [Fussilat: 33].

Kwa wageni waheshimiwa wa ukurasa wa Facebook wanaouzuru kwa ajili ya haki na ukweli, wakitafuta kheri unaoibeba, basi Mwenyezi Mungu awalipe kheri ...

Nawapongeza wote kwa mnasaba wa sikukuu ya Eid ul-Adhaa na ninamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aikubali Hajj ya wale wanaoifanya na aifanye kuwa ni Hijja inayokubaliwa, juhudi inayopokelewa vyema na kusamehewa madhambi. Na pia namuomba Mwenyezi Mungu (swt) Ajaalie Tawfiq (kuafikiwa) kwa wale ambao hawakuhiji mwaka huu waifanye mwaka unaofuata kwa kheri juu ya kheri, na Mwenyezi Mungu (swt) ni Walii (Mlinzi) wa watu wema.

Kama ambavyo namuomba (swt) kwa Idd hii iwakilishe ufunguzi wa kheri na baraka kwa Waislamu, ili Idd ijayo ifike tukiwa chini ya kivuli cha Raayah (bendera) ya Khilafah Rashida. Rayah ya Laa Ilaaha Illa Allah Muhammadun Rasuulullah:

 (وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّـهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)

Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu [Ar-Rum: 4-5].

Kwa kutamatisha, nawatumia salamu zangu, nawaombea dua ya kheri, na kwamba Mwenyezi Mungu azikubali ibada zenu njema na utiifu wenu:

 (وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ)

na mwema mno ujira wa watendao [Aali ‘Imraan: 136].

Wasalaamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakaatuhu.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Amiri wa Hizb ut Tahrir

10 Dhul Hijjah 1443 H

Sawia na 09/07/2022 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu