- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:
Maoni ya Habari 21/06/2023
Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.
Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.
Ewe Mwenyezi Mungu, turegeshee ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahumma Ameen.
#BringBackKhilafah
Jumatano, 03 Dhu al-Hijjah 1444 H sawia na 21 Juni 2023 M
Watawala wa Waislamu ni Walinzi wa Umbile la Kiyahudi
Baada ya kitendo cha kishujaa cha mwanajeshi wa Misri, Muhammad Salah, hofu imetanda miongoni mwa wanajeshi wa Kiyahudi. Gazeti la "Jerusalem Post" liliripoti mnamo tarehe 10 Juni 2023, kwamba jeshi la Mayahudi limefupisha saa za zamu za kulinda mpaka wa Misri, baada ya askari wake kukataa vipindi virefu! Mayahudi ni waoga na wanawategemea watawala wa Waislamu kuzuia majeshi yao. Maafisa wa Kiislamu lazima wawaondoe watawala hawa, wasimamishe Khilafah na waandamane kwa ajili ya ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa.
26 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 15 Juni 2023 M
Khilafah Itaanzisha Ufadhili wa Viwanda bila ya Riba
Mkutano kati ya Balozi wa China na Waziri wa Fedha mnamo tarehe 12 Juni 2023 uliangazia utegemezi unaoendelea wa mikopo ya riba ya China. Uongozi wa sasa hufanya malipo ya riba, ambayo ni makubwa kuliko nakisi ya bajeti. Kisha unachukua mikopo zaidi kwa riba, na kuongeza deni. Khilafah itakomesha riba na kusimamia uchumi kwa mujibu wa Uislamu. Itazalisha mapato makubwa kutokana na kusimamia mali ya umma ya nishati na madini. Pia itatawala sekta kubwa inayohitaji mtaji mkubwa, ili iweze kushughulikia mahitaji ya umma ipasavyo.
27 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 16 Juni 2023 M
Khilafah Haitahitaji Mafuta na Gesi kutoka kwa Dola zanye kuupiga vita Uislamu
Mnamo tarehe 12 Juni 2023, Waziri wa Sheria alitangaza kwamba, "Pakistan inatarajia ushirikiano katika nishati na Urusi." Usalama wa nishati haupatikani kwa kupata nishati ya bei nafuu kutoka kwa dola zinazoupiga vita Uislamu. Pia haupatikani kwa kubadilishana dolari na rubles katika biashara ya kimataifa. Ulimwengu wa Kiislamu utakuwa na usalama wa nishati wakati Ardhi za Waislamu na rasilimali zao nyingi za nishati zitakapounganishwa chini ya dola moja ya Khilafah. Kisha Khalifa atatumia mapato yatokanayo na mauzo ya mafuta na gesi kwa ajili ya kuwachunga raia wote.
28 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 17 Juni 2023 M
Khilafah Itatafuta Ajira za Ndani kwa Vijana Wetu Waliosoma
Kulingana na shirika la utafiti Gallup Pakistan na PRIDE, 23.6% ya vijana wote wa mijini wasio na kazi katika mkoa wa Sindh wana digrii ya chuo kikuu. Ni wazi kuwa serikali haina ruwaza ya ukuzaji wa haraka wa viwanda, kutoa ajira kwa vijana waliosoma. Mfumo wa sasa wa uchumi wa kibepari wa kimataifa hauturuhusu kutimiza mahitaji yetu ya ndani kupitia uzalishaji wa ndani wa viwanda. Chini ya Khilafah, mfumo wa kiuchumi wa Uislamu utatoa sheria madhubuti za kiuchumi. Khilafah inatawala tu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ﷻ pekee, hivyo sheria hizi kamwe hazitafutwa.
29 Dhul Qa'adah 1444 H sawia na 18 Juni 2023 M
Marekani Inaunga Mkono Kuinuka kwa India, Licha ya Vita vyake dhidi ya Uislamu
Mnamo tarehe 15 Juni 2023, Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, alitangaza, "Kwa wale ambao wako tayari leo kufungua milango yao kwa Waziri Mkuu wa India, tunahimiza kwamba watoe wito wa kusitishwa kwa ukandamizaji na ukatili wa India." Marekani tayari imefungua milango ya kiuchumi na kijeshi kwa India, ili iweze kukabiliana na China na Waislamu. Ukuaji wa kiuchumi wa India sasa umeongezeka hadi asilimia 6.1 katika robo ya Januari hadi Machi. Khilafah inawatia nguvu Waislamu kwa kuutabikisha Uislamu na kuuunganisha Ummah kama dola moja. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:
[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]
“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surah An-Nisa'a 4:139].
01 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 19 Juni 2023 M
IMF Inataka Ushuru Uongezwe ili Pakistan Ilipe Riba kwa Mikopo
Mnamo tarehe 16 Juni 2023, Wizara ya Fedha ilishughulikia wasiwasi wa IMF kuhusu kupanua wigo wa kodi. IMF inataka kwamba ushuru uongezwe mara kwa mara, ili kulipa malipo ya riba. Ushuru ulikuwa zaidi ya trilioni 1 mnamo 2009, rupia trilioni 2 mnamo 2014, trilioni 4 mnamo 2019 na sasa, kwa 2024, ni zaidi ya trilioni 9. Suluhisho la mgogoro wa kifedha wa Pakistan ni kukomesha riba. Khilafah kwa Njia ya Utume itakataa matakwa ya IMF na kutumia katika majukumu ya Shariah. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ * فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ]
“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” [Surah al-Baqarah 2: 278 - 279]
02 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 20 Juni 2023 M
Chini ya Ubepari, Pakistan Kamwe Haitakwepa Mtego wa Madeni
Benki Kuu ya Pakistan (SBP) ilitangaza mnamo tarehe 16 Juni kwamba imepokea dolari bilioni 1 kutoka China. Mnamo 1971, deni la Pakistan lilikuwa rupia bilioni 30, lakini kufikia 1991, lilipanda hadi rupia bilioni 825. Kufikia 2011, deni la Pakistan lilikuwa rupia trilioni 10 na sasa linakaribia rupia trilioni 60. Malipo ya riba yanahakikisha Pakistan inatumbukia ndani zaidi kwenye mtego wa madeni. Khilafah itaondoa riba. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:
[الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا]
“Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.” [Surah al-Baqarah 2:275]. Khilafah itazalisha mapato makubwa kupitia kusimamia nishati na madini, pamoja na kuanzisha viwanda vizito.
03 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 21 Juni 2023 M