Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 28/06/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, turegeshee ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahumma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 10 Dhu al-Hijjah 1444 H sawia na 28 Juni 2023 M

300 Wazama Baharini, Huku Wakikimbia Mateso ya Maisha nchini Pakistan

Mnamo tarehe 18 Juni 2023, Mwenyekiti wa Seneti ya Pakistan aliomboleza hasara mbaya ya maisha ya zaidi ya Wapakistani 300, katika ajali ya mashua ya hivi majuzi kwenye pwani ya Ugiriki. Kuomboleza kifo cha Waislamu haitoshi. Wala kulaani walanguzi wa binadamu. Ni juu ya watawala kuzuia masaibu yanayowasukuma Waislamu kukimbia nchi, kuhatarisha maisha na viungo. Badala yake, watawala hutekeleza sera za IMF zinazoleta hali mbaya ya kiuchumi. Umefika wakati wa Waislamu kusimamisha tena Khilafah Rashida, ili hatimaye tuwe na watawala wanaotujali. Amesema Mtume (saw) مَا مِنْ أَمِيرٍ يَلِي أَمْرَ الْمُسْلِمِينَ ثُمَّ لاَ يَجْهَدُ لَهُمْ وَيَنْصَحُ إِلاَّ لَمُمْهَلَّ لَمْهَدُ لَهُمْ وَيَنْصَحُ إِلاَّ لَمُمْهَلَّ لَمُمْهَدُ لَهُمْ ‏ “Mtawala ambaye, baada ya kupata mamlaka juu ya mambo ya Waislamu, hafanyi juhudi kwa ajili ya kheri yao na wala hawatumikii kwa ikhlasi, hataingia Peponi pamoja nao.” [Muslim]

04 Dhul al-Hijjah 1444 H sawia na 22 Juni 2023 M

Majeshi ya Yote ya Ulimwengu wa Kiislamu kwa Pamoja Yanatosha Kukomboa Ardhi Zinazokaliwa kwa Mabavu

Raundi ya 12 ya Mashauriano ya Kisiasa baina ya Pakistan na Iran (BPC) ilifanyika jijini Tehran, mnamo tarehe 17-18 Juni 2023. Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan alishukuru uungaji mkono thabiti wa Iran kwa ajili ya Kashmir. Huku zikiwa zimegawanyika kwa dola za kitaifa, Ulimwengu wa Kiislamu umedhoofika mbele ya maadui zake. Pakistan ina wanajeshi 653,000, huku Iran ikiwa na wanajeshi 523,000, Misri ikiwa na wanajeshi 438,500, huku Uturuki ikiwa na wanajeshi 355,200. Saudi Arabia ina 227,000, huku Morocco ina 195,800. Chini ya Khilafah, ardhi hizi sita zitakuwa na jeshi la pamoja la watu 2,392,500. Jeshi kubwa kama hilo linatosha zaidi kukomboa Ardhi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu. Mwenyezi Mungu ﷻ ameamrisha,

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ]

Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” [Surah al-Baqarah 2:191].

05 Dhul al-Hijjah 1444 H sawia na 23 Juni 2023 M

Khilafah (Ukhalifa) juu ya Njia ya Utume Peke Yake Inaweza Kumaliza Mgogoro wa Kiuchumi

Mnamo tarehe 20 Juni 2023, mkuu wa jeshi aliwahakikishia watu wote kuunga mkono juhudi za Serikali za Mpango wa Kufufua Uchumi. Mpango wa Kufufua Uchumi utashindwa kwa sababu ni mpango wa kiuchumi wa kibepari, chini ya mfumo wa uchumi wa kilimwengu wa Marekani. Mpango unaohitajika ni ule wa mfumo wa uchumi wa Kiislamu. Khilafah itakomesha riba, na kuelekeza fedha kwenye uchumi halisi. Itanyakua mali iliyofujwa kutoka kwa watawala na maafisa wafisadi, ili kulipa madeni. Itatoa sarafu za dhahabu na fedha, na kukomesha mfumko wa bei. Itasimamia moja kwa moja nishati na madini, ikitoa mapato makubwa ya kushughulikia mambo ya watu. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Surah Taha: 124].

06 Dhul al-Hijjah 1444 H sawia na 24 Juni 2023 M

Mkolono Marekani Ametangaza Vita dhidi ya Uislamu na Kuleta Uharibifu wa Kiuchumi

Mnamo tarehe 21 Juni 2023, Waziri wa Fedha alimweleza Balozi wa Marekani kuhusu juhudi za kutimiza wajibu wa kifedha wa kimataifa. Mkutano huo ni mfano mmoja tu wa maana ya kuwa kibaraka wa wakoloni. Waziri wa Fedha anafungua maelezo ya kiuchumi kwa serikali ambayo inapigana na Uislamu, na kusaidia umbile la Kiyahudi na Dola ya Kibaniani katika kufanya hivyo. Marekani ni dola ambayo imeangamiza sehemu kubwa ya dunia kupitia mfumo wa kibepari ambao inautabikishaa. Khilafah ndiyo itakayomaliza mahusiano na mafungamano nayo. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah al-Mumtahina 60:9].

07 Dhul al-Hijjah 1444 H sawia na 25 Juni 2023 M

Kupitia Kusimamisha Khilafah, Ulimwengu wa Kiislamu Utakuwa Kitovu cha Nishati Ulimwenguni

Serikali inaziomba Ulaya na China kuweka njia za usambazaji wao wa gesi kutoka dola za Asia ya Kati, kupitia Gwadar ili kuhakikisha usalama wao wa nishati. Watawala wa Pakistan daima wanajionyesha kwa dola za kikoloni kama watumishi wao waaminifu. Hisa kubwa ya mradi huo ni ya makafiri, huku makombo yaliyobaki ndio ya Waislamu, kama vile Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC). Mbadilishaji mchezo halisi ni uunganishwaji wa Pakistan, Afghanistan na dola za Asia ya Kati kama dola moja ya Khilafah. Khilafah kwa Njia ya Utume itakuwa ni dola kuu, ambayo haiwezi kupuuzwa na dola yoyote duniani. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

[الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]

“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Surah An-Nisa'a 4:139].

08 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 26 Juni 2023 M

Muungano wa Pamoja wa Marekani na India Dhidi ya Pakistan Unaweza Kukabiliwa na Khilafah Rashida Pekee

Wizara ya Mambo ya Nje imelalamika, "Tunazingatia makusudio makhsusi ya Pakistan katika 'Taarifa ya Pamoja kutoka Marekani na India', iliyotolewa mnamo tarehe 22 Juni 2023, kama isiyo na msingi, ya upande mmoja na ya kupotosha." Baada ya vibaraka wa Amerika kuchukua mamlaka nchini India, dori ya Pakistan kuhusiana na Marekani ilikwisha, na Pakistan ilitupiliwa mbali. Wamarekani sasa wanaamuru kwamba dori yake iwe ni kupiga vita Uislamu na Waislamu. Hivi ndivyo Marekani inavyowachukulia vibaraka wake na hii ndio hatima yao. Njia pekee yenye ufanisi dhidi ya muungano wa Marekani na India ni kuunganishwa kwa Umma wa Kiislamu chini ya Khilafah kwa Njia ya Utume. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) هَذَا كِتَابٌ مِنْ مُحَمَّدٍ النَّبِىِّ ﷺ بَيْنَ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُعثتَثْمِنِينَ مِنْ قُرَيْبِينَ وَالْمُثْمِنِينَ مِنْ قُرَيْبِينَ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُثْمِنِينَ مِنْ قُرَيْبَشِيْرِينَ عَلَّى ُمْ فَلَحِقَ بِهِمْ وَجَاهَدَ مَعَهُمْ أَنَّهُمْ أُمَّةٌ وَاحِدَةٌ دُونَ النَّاسِ “Haya ni mapatano ya Mtume Muhammad baina ya Waislamu na Waumini kutoka makabila ya Maquraishi na Yathrib na waliokuwa chini yao wakipigana vita kwa pamoja. Hakika wao ni Ummah mmoja, tofauti na watu wengine wote.” [Bayhaqi]

09 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 27 Juni 2023 M

Pongezi Sana kwa Mnasaba wa Sikukuu ya Idd ul Adha

Kwa mnasaba wa sikukuu hii ya Idd ul Adha iliyobarikiwa, tunamuomba Mwenyezi Mungu ﷻ kwamba azikubali sadaka zetu na Hijja ya Mahujaji kutoka kote duniani. Hakika, Hijja na Idd ul Adha ni dhihirisho la Umma mkubwa, unaounganisha Waislamu wa rangi, lugha na makabila mengi. Katika wakati ambapo Waislamu wamegawanyika na kudhoofika katika vidola vidogo 57 mbele ya maadui zao, tunamuomba Mwenyezi Mungu ﷻ auunganishe Ulimwengu wa Kiislamu kuwa dola moja, Khilafah kwa Njia ya Utume. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema,

تَرَى الْمُؤْمِنِينَ فِي تَرَاحُمِهِمْ وَتَوَادِّهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ كَمَثَلِ الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى عُضْوًا تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ جَسَدِهِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى

Unawaona Waumini, katika rehema zao, na kuhurumiana, na wema wao, kama mwili mmoja. Ikiwa kiungo chochote cha mwili hakiko sawa, basi mwili wote hushiriki kutotulia na homa.” [Bukhari]

10 Dhul Hijjah 1444 H sawia na 28 Juni 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu