Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

“Umma Mmoja… Khilafah Moja”

Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan imeandaa kampeni kwa kichwa, “Umma Mmoja… Khilafah Moja” katika mitandao ya kijamii.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, turegeshee ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahumma Ameen.

#1Ulema1Khilafah

Ijumaa, 26 Dhu al-Hijjah 1444 H sawia na 14 Julai 2023 M

Khilafah ya Kiislamu ina bendera za kipekee, "Liwaa" na "Raya." Ushahidi unatokana na dola ya kwanza ya Kiislamu, ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliisimamisha. Bendera ya Liwaa ni nyeupe. “La Ilaha illa Allah, Muhammadun RasulAllah ﷺ,” imeandikwa juu yake kwa maandishi meusi. Imefungamanishwa na mkuu (amir) wa jeshi. Inatumika kama bendera (‘alam) kwa ajili yake peke yake. Ushahidi wa hili ni ule uliopokewa na Ibn Majah, “Kwamba Mtume ﷺ aliingia Makka siku ya ufunguzi wake. Bendera yake ya Liwaa ilikuwa nyeupe.”

Bendera ya Rayah ni nyeusi. “La Ilaha illa Allah, Muhammadun Rasul Allah ﷺ” imeandikwa juu yake kwa maandishi meupe. Inabebwa na makamanda wa kijeshi wa vitengo, bataliani, vikosi, na vitengo vyengine, vya jeshi la Khilafah. Ushahidi wa hili ni kwamba Mtume ﷺ alipokuwa mkuu wa jeshi huko Khaybar alisema: “Nitampa bendera ya Raya kesho mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Na akampa Ali (ra).” (Bukhari na Muslim)

Mtume ﷺ amesema: “Hakuna Mtume baada yangu. Kutakuwa na Makhalifa na watakuwa wengi.” Maswahaba zake wakasema: Unatuamrisha tufanye nini? Akasema, “Mpeni bay’ah mmoja tu, kwa wakati mmoja.” Imam An-Nawawi amesema katika Sharh yake kwamba, “Iwapo Khalifa atapewa bay’ah baada ya Khalifa mwengine kuteuliwa, basi uteuzi wa kwanza ndio sahihi. Ni lazima utimizwe. Wa pili ni batili. Ni haramu kuutimiza. Ni haramu kwake kudai utimizo huo. Hii ni bila kujali kama Waislamu walimjua Khalifa wa kwanza au la. Haijalishi kama walikuwa katika nchi moja au tofauti, au mmoja wao alikuwa katika nchi iliyotengwa kabisa na nyingine.”

Mtume ﷺ amesema: “Inapochukuliwa Bayah kwa ajili ya Makhalifa wawili, muueni wa mwisho wao.” [Muslim] Imam an-Nawawi alisema katika maelezo yake, kwamba, “Maulamaa wameafikiana kwamba haijuzu kwa Makhalifa wawili kuteuliwa, kwa wakati mmoja. Hii ni bila kujali kama dola ya Kiislamu imepanuka sana au la. Imam al-Haramain (al-Juwaini) alisema katika kitabu chake “al-Irshad,” kwamba, “Rai za wanachuoni wa zama zetu ni kwamba hairuhusiwi kwa watu wawili kuteuliwa kwa wakati mmoja (kama Khalifa). Rai yangu ni kwamba hairuhusiwi kuteuwa makhalifa wawili katika ardhi moja. Rai hii imekubaliwa na wote.”

Ibn Ishaq anasimulia, kwamba katika Khutba yake, Abu Bakr (ra) alisema, “Hakika, hairuhusiwi kwa Waislamu kuwa na amiri wawili. Laiti hilo lingetokea, kungekuwa na hitilafu juu ya mambo na sheria zao, umma wa Waislamu ungefarakana na kubishana wao kwa wao. Hilo lingesababisha kuachwa kwa Sunnah. Uzushi (bid’ah) ungeonekana, mifarakano (fitnah) ingekuwa imeenea, ambapo hakuna chochote kati ya hayo kingekuwa haki kwa yeyote.”

Katika “Sunan” yake, ad-Darimi, ambaye alifariki mwaka 255 H, alisimulia kutoka kwa Umar (ra) ambaye alisema, “Hakuna Uislamu, bila ya jamaa moja. Hakuna jamaa, bila ya Imarah moja. Hakuna Imarah bila ya utiifu.”

 

Imam Mawardi, ambaye alifariki mwaka 450 H, alisema katika kitabu chake, “al-Ahkam as-Sultaniyyah,” kwamba, “Ikiwa Maimamu wawili watateuliwa katika ardhi tofauti, uongozi wao wa pamoja hauwi na mkataba. Hairuhusiwi kwa Ummah kuwa na Maimamu wawili (Khalifa) kwa wakati mmoja.”

Ibn Hazm, aliyefariki mwaka 458 H, alisema katika “Maraatib al-Ijmaa’a” kwamba, “Kuna Ijma’a (Itifaki) kwamba hairuhusiwi kwa Waislamu kuwa na Maimamu wawili (Khalifa), popote pale duniani, kwa wakati huo huo mmoja. Hii ni iwe Maimamu wawili wamekubaliana juu ya jambo hili, au wamekhitilafiana. Pia hairuhusiwi kuwa na Maimamu wawili ima wawe mahali pamoja, au katika sehemu mbili tofauti.”

Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ: “Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu”. [Surah al-Anfaal 8:46]. Ibn Kathir amesema katika Tafsiir yake, “Na nguvu zenu zitaondoka, yaani, nguvu zenu, umoja wenu, na chochote kilichomo ndani yenu cha ustawi.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: “Haya ni mapatano ya Mtume Muhammad baina ya Waislamu na Waumini wa makabila ya Quraishi na Yathrib na walio chini yao wakipigana vita pamoja na wao. Hakika wao ni Ummah mmoja, tofauti na watu wengine wote.” Imesimuliwa na Al-Bayhaqi katika Al-Sunan Al-Kubra. Umma wa Kiislamu ni Ummah mmoja na umoja wa Kiislamu lazima upatikane kivitendo ndani yake. Ama umoja huu wa kisiasa unafumbatwa katika kusimamisha Khilafah.

Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: “Waumini katika kupendana, kuhurumiana kwao, upole wao, ni kama mwili mmoja. Ikiwa kiungo chochote cha mwili hakiko sawa, basi mwili mzima hushiriki kwa kukosa usingizi na homa.” Hili ni agizo kwa Waislamu kuwa na umoja, katika mambo yao yote. Umoja wa kisiasa chini ya Khilafah moja ni matokeo ya kimaumbile ya umoja huu wa kifikra na kihisia.

 

Imam Shafi’i, ambaye alifariki mwaka 204 H, alisema katika “Ar-Risaalah” kwamba, “Waislamu wana Makubaliano ya Pamoja kwamba kunaweza kuwa na Khalifah mmoja tu. Mwenye kuhukumu ni mmoja (katika mzozo), Amiri ni mmoja (katika mambo) na Imam ni mmoja (katika Dini).

Imam Al-Qurtubi, aliyefariki mwaka 671 H, alisema katika tafsiri yake kwamba, “Ayah hii (al-Baqarah: 30) ni msingi wa kuweka Imam mmoja na Khalifa, anayesikilizwa na kutiiwa. Mambo yanaunganishwa kupitia yeye.”

 

Ibn Hajar Al Asqalani, aliyefariki mwaka 852 H, alisema katika “Fath al-Bari,” kwamba, “Al-Nawawi na wengineo walisema, wao (Maulamaa) walikubaliana kwa kauli moja kwamba ni lazima ateuliwe Khalifa mmoja baada ya mwengine. Uteuzi wake lazima ufanywe na wale waliopewa mamlaka (ahl ul hal wal ‘aqd). Lazima kuwe na Khalifa mmoja tu, na hakuna mwengine anayeteuliwa zaidi yake.”

Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ: “Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Sura Aali Imran 3:103]. Ibn Kathir amesema katika Tafsir yake kwamba, “Anaamrisha Waislamu kuwa umma mmoja na Yeye ﷻ anawakataza kugawanyika.” Aya hii ni ushahidi kwamba Waislamu wanalazimika kukusanya, kuungana, ndani ya umbile moja.

Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: “Yeyote anayejaribu kugawanya mambo ya Ummah huu na hali umeshikamana, basi lazima mumpige kwa upanga, yeyote awaye.” [Muslim]. An-Nawawi amesema katika Sharh yake, “Ndani ya hii kuna amri ya kupigana na yeyote anayemuasi Imam (Khalifa), au anataka kugawanya mambo ya Waislamu na yanayofanana na hayo. Amekatazwa kufanya hivyo. Ikiwa uovu wake haungeweza kuzuiliwa isipokuwa kwa kumuua, basi atauawa.” Asili, Umma huu wa Kiislamu unapaswa kuunganishwa, chini ya mamlaka moja, Khilafah. Adhabu ya kisheria kwa yeyote anayetaka kuigawanya na kuigawanya katika viumbo vidogo na majimbo, ni kuuliwa.

Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ: “Hakika Waumini ni ndugu.” [Surah al-Hujurat 49:10]. Imam Qurtubi alisema katika Tafsir yake, “Yaani katika Dini na utakatifu, sio katika rangi. Kwa sababu hii, ilisemwa, ‘Udugu katika Dini ni wa kudumu zaidi kuliko udugu kwa rangi. Udugu kwa rangi hukatwa kwa kukiuka Dini, wakati udugu katika Dini haukatiki kamwe na tofauti za rangi.

Mtume ﷺ amesema: “Enyi wanadamu, hakika Mola wenu ni Mmoja, na baba yenu wa mwanzo ni mmoja. Hakika Mwarabu hana ubora juu ya asiye Mwarabu, wala asiye Mwarabu juu ya Mwarabu, wala mweupe juu ya mweusi, wala mweusi juu ya mweupe, isipokuwa kwa uchamungu.” [Ahmad]

Ni dhambi kubwa kuitisha mafungamano kwa misingi yoyote ile isipokuwa udugu wa Uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: “Mwenye kuuawa chini ya bendera ya ujahiliya, akilingania uaswabiya au kuunga mkono uaswabiya, basi amekufa kifo cha kijahiliya.” [Muslim]. Imam an-Nawawi amesema katika Sharh yake, “Hakika yeye hukasirika kwa ajili ya uaswabiya na hainusuru Dini. Uaswabiya ni kulisaidia taifa lake katika kudhulumu.” Hivyo basi, Waislamu wakatae miito yoyote ya ukabila au utaifa na washike kamba ya Mwenyezi Mungu ﷻ kwa uthabiti, kwani huu ndio ufunguo wa nguvu zetu.

Vijana wawili, mmoja kutoka kwa Muhajirina na mwengine kutoka kwa Ansari, walikuwa wakipigana. Muhajir aliwaita Muhajirina wenzake, huku Ansari wakiwaita Ansari wenzake. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akatoka na kusema: “Kunani mwito huu wa Kijahiliya?” [Muslim]. Imam An-Nawawi amesema katika “Sharh” yake, “Ama kuuita kwake mwito huu kuwa ni ujahiliya, ni kuuchukia kwake. Ni sehemu ya mila ya Jahiliyah kusaidia kulingana na makabila, katika mambo yanayohusiana na ulimwengu. Ni kutokana na ujinga kuchukua haki kwa misingi ya rangi na makabila. Uislamu ulifuta hilo, na ukaamua kesi kwa hukmu za Shariah.”

 

Kilichounganisha makabila yanayoshindana kwenye Bara Arabu haikuwa rangi, bali Uislamu mkuu pekee. Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: “Mwenye kujinasibisha na sifa ya Ujahiliyyah, basi mwambie aume uume wa baba yake, na wala usiseme kwa mfano.” Imepokewa na Ahmad. Mulla Ali al-Qari amesema katika Sharh yake, “Mtu anayejisifia nafsi yake ina maana kwamba anajisifu kwa nasaba, kama ilivyonasibishwa katika Jahilliyah (ujinga). Kuna sauti ya vokali ya Fat’ha kwenye ‘ayn. Inamaanisha jamii ya familia yake, kwa kujisifu juu ya baba zake na babu zake.”

Mtume ﷺ alipoondoka Makka alisema: “Ninakuacha nikijua kwamba wewe ni ardhi inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu na mtukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Lau kama watu wako hawakunifukuza kwako, nisingeondoka.” (Musnad Al-Harith, nyongeza ya Al-Haythami). Maandiko yote yanaelekeza kwenye ukweli kwamba Mtume ﷺ aliipenda Makka kwa sababu ilikuwa ni ardhi inayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu, kwani ndani yake ilikuwa na Nyumba Yake Tukufu, Ka’aba. Upendo huu haukuwa kwa sababu ya ukabila, au uzalendo, au utaifa.

Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ: “Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [Sura an-Nisaa 4:139]. At-Tabari amesema katika Tafsir yake, “Wale waliochukua washirika kutoka miongoni mwa makafiri, hutafuta heshima pamoja nao. Hao ndio watu waliofedheheka zaidi na watu duni zaidi. Basi, kwa nini hawakuchukua washirika miongoni mwa Waumini ili wapate utukufu, ulinzi na msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ana heshima na ulinzi?

Imam Shafi’i amesema: “Yeyote anayedhihirisha ukabila au ubaguzi wa rangi kwa kauli, kwa kuungana na kwa kuitana, hata kama hakupata umaarufu kwa kuupigania, basi ushahidi wake unakataliwa. Alifanya jambo lililokatazwa. Hakuna tofauti ya rai miongoni mwa Maulamaa wa Kiislamu, kwa mujibu wa nijuavyo mimi. Dalili ni kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ: “Hakika Waumini ni udugu” na pia kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) “Na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu kama ndugu.” [Imepokewa na Bayhaqi katika As-Sunan As. -Saghir]

Mwenyezi Mungu ﷻ amesema: “Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.” [Sura Aali-Imran 3:28]. Imam Qurtubi amesema katika Tafsir yake, “Ibn Abbas (ra) amesema: “Mwenyezi Mungu amekataza waumini kuridhika na makafiri, na kuwachukua kama washirika. Vile vile, msichukue wasiri wa karibu nje ya nafsi zenu. Kwa hivyo, unakuja ufafanuzi wa maana hii.”

Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ: “Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha.” [Sura Aali Imran 3:102]. Ibn Abbas (ra) ameeleza, “kwamba wanajitahidi katika njia Yake jinsi Anavyostahiki juhudi Yake. Ni lazima wasiogope lawama ya mwenye kulaumu, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ﷻ. Ni lazima watende uadilifu, hata kama ni kinyume na nafsi zao, mababu zao na vizazi vyao.” [Imepokewa na Ibn Kathir katika Tafsiir yake]

Mtume ﷺ amesema: “Mwenye kujitenga na Ummah wa Kiislamu kiasi cha shubiri moja, basi amepotoka kutokana na Uislamu isipokuwa aregee kwenye ummah. Yeyote anayelingania ukabila wa ujahilia ni miongoni mwa watu wa Jahannam, hata akifunga, akaswali na kudai kuwa yeye ni Muislamu.” [Imepokewa na At-Tirmidhi na Ahmad]. Moja ya dfahamu kuu za Umma wa Kiislamu ni uaminifu na huruma ya pande zote kwa Waislamu, na kukataliwa kwa kila fungamano jengine. Hakuna msaada, hakuna mapigano na hakuna chuki kwa ajili ya kabila, familia, nchi au watu.

Mtume ﷺ amesema: “Mwenyezi Mungu amekuondoleeni fahari ya zama za ujahilia, na kujifakhirisha na mababu. Mtu ima ni muumini mchamungu au mtenda dhambi muovu. Nyinyi nyote ni wana wa Adam (as), na Adam (as) anatokana na udongo. Watu waache kujifakhiri kwa mababu zao. Hao ni kuni tu katika Jahannam, au bila shaka watakuwa chini ya hisabu mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko mdudu anayeviringisha kinyesi kwa pua yake.” [Abu Daud]

Abdullah ibn Mas’ud (ra) amesema: “Yeyote anayeunga mkono jamii yake kinyume na Haki, huyo ni kama ngamia anayetumbukia kisimani na kuvutwa kwa mkia wake.” [Abu Daud]. Imam Al-Khatabi amesema katika Ma’alim as-Sunan, “Inachomaanisha ni kwamba ameanguka katika dhambi. Aliangamia kama ngamia, anapotupwa kisimani. Anakuwa amenyimwa kwa sababu ya dhambi lake, na hawezi kutoroka.”

Badr ud Din Al-Ayni Al-Hanafi, aliyefariki mwaka 855 H, amesema katika “Umdat al-Qari” kwamba, “Ama kauli ya Mtume ﷺ: “Kwa nini ulinganie kwenye Ujahiliya? Ina maana, msilinganie msingi wa ukabila. Badala yake, linganieni umoja juu ya Uislamu. Kisha ﷺ akauliza, wana nini? Ina maana, nini kimewatokea kwao, na ni nini sababu ya hilo. Ama kusema kwake, “Uacheni,” ina maana ya kuacha msimamo huu, yaani kuuacha, au kuacha dai hili. Kisha akabainisha hekima ya kuuacha, kwa kusema, “Hakika ni uvundo.” Maana yake ni mbaya, wa kulaumiwa, ya kuchukiza na wenye madhara, kwa sababu unachochea hasira juu ya kisicho sawa na kupigana juu ya batili, ukikaribisha Motoni, kama ilivyoelezwa katika Hadith, “Si katika sisi yeyote anayelingania Uaswabiya, basi na ajiandalie makaazi yake katika Moto wa Jahannam.”

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu