Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Mkao wa Kadhia za Ummah

Kuvunjwa kwa Khilafah na Majanga Yaliyofuata Juu ya Ummah

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya mkao wake wa kawaida kila wiki mnamo Jumamosi, Rajab 1, 1442 Hijria, sawia na tarehe 13/2/2021 M, mkao wa Kadhia za Ummah, ambalo ulisimamishwa kwa wiki kadhaa kutokana na hatua za kiafya za janga la virusi vya Korona. Mkao huo ulikuja mwanzoni mwa mwezi wa Rajab al-Khair, sanjari na kampeni ya kiulimwengu inayoongozwa na Hizb ut Tahrir katika mwezi huu mtukufu, ambayo inaafikiana kumbukumbu ya karne moja ya kuvunjwa kwa Khilafah kutoka 1342 Hijria hadi 1442 Hijria, chini ya kauli mbiu "Juu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah ... Isimamisheni Enyi Waislamu, Imarisheni!"

Anwani ya mkao huu ilikuwa: "Kuvunjwa kwa Khilafah na Majanga Yaliyofuata Juu ya Ummah". Wazungumzaji walikuwa Ustadh Nasser Ridha Muhammad Uthman, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, na Ustadh Al-Nazir Mukhtar, mwanachama wa Hizb ut Tahrir.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu