- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ripoti ya Habari 11/07/2021
Mwendelezo wa amali umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuunda rai jumla yenye utambuzi kuhusu vifungu vya Uislamu na masuluhisho yake yanazohusiana na nidhamu anuwai za maisha, ambazo zinashughulikia mada anuwai, zikiwemo migogoro ya utawala, kuondoa ruzuku ya mafuta, kukomesha dolari ya forodha, na uhuru wa maamuzi ...
Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, katika eneo la Khartoum, mnamo Juni 21, 2021, walifanya hotuba yao ya kisiasa, katika uwanja wa Jackson katikati mwa Khartoum kwa anwani: "Kuondoa ruzuku ya mafuta, sababu halisi na masuluhisho ya msingi", ambapo mzungumzaji wa kwanza, Bwana Mujahid Adam, alizungumzia sababu halisi za uamuzi wa kuondoa ruzuku ya mafuta uliolazimishwa na serikali kwa watu na akaelezea athari mbaya za uamuzi huu, ambao uliongezea mateso ya watu maradufu.
Ama mzungumzaji wa pili, Ustadh Fadlallah Ali, alionyesha masuluhisho halisi ya kimsingi ambayo yanatokana na imani ya Ummah, ambayo ni fikra kamili ya kisiasa inaloshughulikia matatizo yote ya maisha, na ambayo haitakuwepo kiuhalisi isipokuwa kwa kusimamishwa Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo inakuuza nishati za Umma na inawawezesha watu kutumia rasilimali halisi ambazo nchi imejaa nazo, na kuhakikisha kuwa mahitaji ya kimsingi ya watu yameshibishwa kikamilifu kwa kila mwanajamii. .
Chini ya anwani: "Kutoa Uhuru wa Maamuzi kwa eneo la Blue Nile na Kusini mwa Kordofan, ni Kuivunja Vunja Sudan Iliyobakia," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Madani walifanya hotuba ya kisiasa katika kituo cha mabasi na uwanja wa Soko Kuu mnamo Jumanne, Juni 22, 2021, ambapo Ustadh Abdel Aziz alisisitiza kuwa Serikali ya Mpito inafuata njia ya zile zinazoitwa serikali za kitaifa na inahitimisha makubaliano ya khiyana kama Mkataba wa Juba na kulipa eneo la Kusini mwa Kordofan na Blue Nile uhuru wa maamuzi, ambayo baadaye yatapelekea katika haki ya kujitawala wenyewe na kisha kujitenga.
Kwenye mada hiyo hiyo, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilaya ya mnamo Juni 23, 2021, katika eneo la Omdurman Magharibi huko Souq Libya walifanya hotuba wakihutubia sera inayoitwa: "Kupatia uhuru wa maamuzi kwa Blue Nile na Kusini mwa Kordofan ni kuivunja vunja Sudan Iliyobakia”Ambapo Ustadh Ishaq Muhammad Hussein alizungumza, akianza na habari ya amri mbaya iliyotolewa na Al-Burhan ya kuyapa uhuru wa maamuzi maeneo hayo miwili kulingana na Kifungu cha 8 cha Mkataba wa Juba. Alionyesha pia kwamba makubaliano haya ni sawa na yale yaliyotangulia jijini Addis Ababa mnamo 1972, ambayo yalipelekea kutenganishwa kwa Sudan Kusini mnamo 2011.
Hotuba ya kisiasa ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mji wa Gadharef pia ilikuja chini ya anwani: "Uhuru wa maamuzi ndio mwanzo wa kujitenga na ufujaji wa utajiri," mnamo Juni 24, 2021, katika uwanja wa Rowena King. Akihutubia hadhira, Ustadh Balla Mahmoud, ambaye alianza hotuba yake akielezea kile kilichopeanwa hivi karibuni kwa maeneo hayo mawili (Kusini mwa Kordofan na Blue Nile) kwamba uhuru wa maamuzi ni usaliti mkubwa, na mwendelezo wa utekelezaji wa mpango wa kihalifu wa Amerika kuigawanya Sudan katika nchi kadhaa, kuanzia na Sudan Kusini. Mzungumza pia alitaja kwamba serikali hii, katika pande zake za kiraia na za kijeshi, imekaa kimya na vidole vyake kumi juu ya usaliti huu mkubwa ambao hakuna mtu mwenye akili timamu angeukubali.
Chini ya anwani: "Ubwana ni wa Shariah na Utawala (Sultan) ni wa Ummah," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa mnamo Juni 27, 2021 huko Al-Kalakila Al-Lafa, ambapo Ustadh Al-Fateh Abdullah alizungumza, ambaye alisema kuwa ubwana na utawala ni kwa Sharia na sio kwa watu kujitungia sheria kupitia mabaraza ya utunzi wa sheria (mabunge). Pia aliweka wazi kuwa mamlaka ni ya Umma na umma ndio unaomchagua mtawala wake kwa utiifu halali, kupitia idhini na chaguo.
Hotuba ya kisiasa ya Mashababu ya Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan, eneo la Omdurman Magharibi, kwa anwani: "Kushindwa kwa serikali zilizoundwa na wanadamu ... na Khilafah ndio Suluhisho," mnamo Juni 28, 2021 huko Souq Libya, ambapo Ustadh Abd al-Rahim Abdullah alizungumza, ambaye alisema kwamba serikali mtawalia za Sudan, tangu uhuru na hadi leo, zimekuwa ni serikali za kisekula, iwe za kiraia au kijeshi, na zote zimeshindwa kusimamia na kuendeleza nchi. Badala yake, imetumbukia ndani ya shimo, na bado tunaendelea kuteketea na moto wa serikali hizi zilizoundwa na wanadamu.
Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, katika eneo la Khartoum, walifanyika mnamo Juni 28, 2021, hotuba yao ya kisiasa, ambayo mara kwa mara wanaifanya katika uwanja wa Jackson katikati mwa Khartoum, kwa anwani: "Hukmu za Mfumo wa Serikali katika Uislamu." Ustadh Muhammad Al-Munir, ambaye alianza mazungumzo yake juu ya mpango wa Waziri Mkuu Hamdok unaohusiana na kulinda jukwaa, aliongea ambapo aliregelea migawanyiko kati ya viungo vya ushirika wa mpito, uliowakilishwa na mgawanyiko kati ya viungo vya jeshi na raia, mgawanyiko ndani taasisi ya jeshi na tofauti kati ya viungo vya upande wa raia. Alielezea wazi wazi kwamba sababu ya mgawanyiko na kuvunjika vunjika huku kati ya pande hizo mbili ni kwa sababu ya kutumiwa kwa pande hizi. Taasisi ya jeshi ni tiifu kwa Amerika, na upande wa raia hufanya kazi kwa maslahi ya Ulaya, ikiongozwa na Uingereza. Balozi za kigeni ndizo zilizowaleta watawala hawa.
Kuhusu mgogoro wa utawala, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Dukhainat walifanya hotuba ya kisiasa mnamo Juni 29, 2021 katika soko la Al Kalakila, kwa anwani: "Ni Uislamu pekee ndio unaowaunganisha watu na kutatua matatizo yao,”Ambapo Ustadh Abdallah Hussein alizungumza juu ya hali ya migawanyiko kati ya viungo vya utawala nchini (kiungo cha jeshi - jeshi na msaada wa haraka - wanamgambo wenye silaha - na raia), pia alionya juu ya mpango wa Magharibi wa kuipasua Sudan kwa umbile zaidi ya moja kupitia kuchochea ugomvi wa kikabila na kieneo, akielezea kuwa Uislamu peke yake ndio unaowaunganisha watu baada ya kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu.
Chini ya anwani "Ubatilishaji wa Dolari ya Forodha na Athari zake kwa Bei," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan huko Gadharef walifanya hotuba yao ya kila wiki mnamo Julai 1, 2021 katika uwanja wa Rowena King, ambapo Mhandisi Al-Bashir Ahmed Al-Bashir alizungumzia juu ya ukomeshaji wa serikali wa hivi karibuni wa dolari ya forodha, akionyesha nia na matokeo ya uamuzi huo. Alitaja pia kuwa dolari ya forodha sio noti, bali ni kipimo cha ukusanyaji pesa za bidhaa zinazoagizwa kutoka ng'ambo katika nchi za ukusanyaji za kirasilimali.
Kuhusu mgogoro wa utawala vileviel, kwa anwani: "Mgogoro wa Utawala nchini Sudan na Suala la Mpito," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Kosti walifanya hotuba ya kisiasa mnamo Julai 2, 2021 katika Soko la Rabik, makutano ya reli na barabara ya 50, ambapo Ustadh Musa Abkar Adam alizungumza, akielezea kuwa tangu kuondoka kwa mkoloni wa Kiingereza kutoka nchi hii, watu wa Sudan hawajafurahia utulivu wa kisiasa hata kidogo, na wamekuwa wakiishi katika mgogoro wa kisiasa hadi leo hii. Wakati mwingine raia husaidiwa na balozi za Ulaya, na wakati mwingine zile za kijeshi husaidiwa na ubalozi wa Amerika, na hakuna hata mmoja aliyeweza kutatua hata tatizo moja.
Chini ya anwani: "Kwa kuongeza bei ya mafuta maradufu, serikali ya mpito inayageuza maisha ya watu kuwa jehanamu. Uzalishaji wetu wa mafuta uko wapi?" Mnamo Julai 6, 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya hotuba ya kisiasa katika kituo cha mabasi na uwanja katika Soko Kuu, ambapo Ustadh Sowar alizungumza, akielezea kuwa serikali ya mpito inatekeleza maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na inafanya kazi kupunguza thamani ya pauni, kwa hivyo iliongezeka maradufu bei ya mafuta, ambayo ilisababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa na huduma, ukosefu wa ajira ulienea na wizi ukasambaa na uporaji wa mchana kweupe, na maisha ya watu yakawa jehanamu isiyoweza kuvumilika.
Chini ya anwani hii: "Je! Sudan inapitia mgogoro?" mnamo Julai 8, 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya hotuba ya kisiasa huko Souq Libya, ambapo Ustadh Ishaq Muhammad Hussein, ambaye alianza hotuba yake kwa kuuliza swali hili kwa umma, na ikiwa jibu ni ndio, sababu ni nini na suluhisho ni nini?
Hotuba ya kisiasa ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Kosti, kwa anwani: "Msingi wa Elimu katika Dola ya Khilafah," ilikuja mnamo Julai 9, 2021 katika soko la Rabik, makutano ya reli na Barabara ya 50, ambapo Ustadh Faisal Madani alizungumzia juu ya misingi ya elimu katika Dola ya Khilafah, haswa imani ya Kiislamu; yaani Aqeeda ya Kiislamu ndio msingi wa elimu na mitaala.
"Hakuna mabadiliko ya kweli isipokuwa kwa mfumo wa Uislamu," katika mada hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya hotuba yao ya kisiasa ya kila wiki jijini Gadharef mnamo Julai 8, 2021, karibu na upande wa Uwanja wa King Rowena. Ilitokea hivi majuzi katika nchi za Kiislamu, au yale yanayoitwa Mapinduzi ya Kiarabu, yakiwemo yale yaliyotokea nchini Sudan, ambapo watu walijitokeza kutafuta mabadiliko.
Maingiliano ya watu na mazungumzo haya yalikuwa mazuri kabisa, na walishiriki katika kuchangia, maoni na maswali ambayo yanaonyesha ari ya Ummah huu, upendo wake kwa Uislamu, hamu yake ya kuhukumu kwa Uislamu na kukataa kwake kitu chengine chochote.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
https://hizbut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/sudan/1744.html#sigProIde89755e608