Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan

Ripoti ya Habari 30/12/2021

Amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ziliendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kujenga rai jumla yenye ufahamu kuhusu hukmu za Uislamu na masuluhisho yake yanayohusiana na mifumo tofauti tofauti ya maisha. Amali hizo zilizungumzia mada mbalimbali, ikiwemo mgogoro wa utawala na migongano kati ya vitengo tofauti tofauti vya serikali pamoja na mapigano ya kikabila.

Mzozo wa kisiasa nchini Sudan na masuluhisho madhubuti, chini ya anwani hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, katika eneo la Omdurman Magharibi, katika soko la Libya, walitoa hotuba ya kisiasa mnamo Disemba 1, 2021, ambapo Ustadh Abdul Rahim Abdullah alizungumza ambapo alieleza kuwa mvutano baina ya Uislamu na ukafiri ni wa milele na hunalizika tu kwa kuondoa moja kati ya nyingine. Makafiri wanakubaliana juu ya kuupiga vita Uislamu na wanatofautiana katika maslahi yao, na mzozo unaoendelea nchini Sudan ni uthibitisho bora wa hilo.

Mnamo tarehe 8 Disemba 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika soko la Libya yenye kichwa: "Si ya kiraia wala ya kijeshi, bali ni Khilafah ya Kiislamu", ambapo Ustadh Ishaq Muhammad Hussein alizungumza, ambapo alionyesha kuwa imamu hakuweka bayana aina ya kazi yake isipokuwa masharti haya saba yanajulikana. Bali, lililo muhimu ni kuangalia nani anatawala, ili kwamba kazi yake iwe ni kutawala na kushughulikia mambo ya watu kwa mujibu wa hukmu za Uislamu.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan huko El Obeid walifanya konmkao wa kila mwezi katika afisi yake mnamo Jumamosi, Disemba 11, 2021, ambao ulikuwa chini ya mada: "Sudan na Uwezekano wa Kusimamisha Khilafah". Sudan inafurahia, katika upande wa maji, ardhi ya kilimo, mifugo na rasilimali za madini, na mengineyo, pamoja na kigezo cha Uislamu, na vilevile vigezo vya kifikra vinavyotokana na imani ya Kiislamu.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Al-Kalakila pia walitoa hotuba ya kisiasa baada ya swala ya Ijumaa mnamo Disemba 12, 2021 katika msikiti wa kale ulio katikati ya Al-Kalakila, kuhusu mgogoro wa utawala nchini humo, ambapo Mhandisi Basil Mustafa, ambaye alianza hotuba yake kwa kuwakaribisha waumini, alisema kuwa huu ni ujumbe kutoka kwa Hizb ut Tahrir kwa waendao msikitini ili kuwakumbusha juu ya faradhi ambayo wanazuoni wengi wa Ummah wameinyamazia, na ujinga wa Waislamu wengi, na watawala hawakuitekeleza; Dola ya Khilafah ndiyo inayotabikisha hukmu za Uislamu.

Kuhusiana na mada ya utawala huo huo, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Khartoum walitoa hotuba ya kisiasa yenye kichwa: "Mtazamo wa Uislamu wa utawala", mnamo Disemba 14, 2021, pamoja na msimamo wa Jackson ambapo Ndugu Ahmed Jaafar alizungumza, ambapo alieleza sababu za mgogoro wa kisiasa nchini humo tangu unaodaiwa kuwa uhuru na hadi mgogoro wa sasa uliozuka baada ya maamuzi ya Al-Burhan Oktoba 25 iliyopita, na akaweka wazi kuwa kuondoka kwenye migogoro hii kunaweza tu kupitia njia ya kusimamisha dola ya Khilafah, na akabainisha sura ya dola hii, nguzo zake na kanuni za utawala ndani yake, na akawawajibisha waliohudhuria kufanya kazi ya kuisimamisha.

Fahamu ya chama katika Uislamu, chini ya anwani hii Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifatoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi mnamo Disemba 15, 2021 katika soko la Libya ambapo Ustadh Abd al-Rahim Abdullah alizungumza ambapo alihakiki hali ya Waislamu wa kwanza, kwa hiyo walikuwa viongozi wa dunia na wao ndio waanzilishi. Walifanya hivyo kwa kushikamana na kanuni ya Uislamu, kwa hiyo walikuwa kambi moja.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa huko El Obeid mnamo Disemba 16, 2021 katika Uwanja wa Uhuru kuhusu mapigano ya kikabila. Ndani yake, Bwana Hussein Al-Hadi alizungumza akieleza sababu za mapigano hayo, ikiwa ni pamoja na kuinua fungamano la kikabila na kikanda juu ya fungamano tukufu la Kiislamu, kutokuwepo kwa sheria inayomzuia kila mhalifu, kutokuwepo kwa heshima ya dola kudumisha usalama na kujali mambo ya watu, na uingiliaji wa dola za kikoloni kwa kuchochea mizozo ya kikabila, kitaifa na kieneo baina ya wana wa Ummah huu ili waweze kupora mali ya nchi hii.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Kaskazini walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Sabreen Point mnamo tarehe 21 Disemba 2021, yenye kichwa: "Maadhimisho ya Miaka 3 ya Mapinduzi ya Disemba... Dira ya mabadiliko inaelekea wapi?" Ndugu Ahmed Abkar alieleza kuwa mapinduzi yalizuka kubadilisha hali mbaya ya kiuchumi na kisiasa iliyokuwa chini ya utawala uliopita. Kilichotokea ni mabadiliko ya watu, na sio ya mfumo.

Chini ya anwani: "Mfumo wa Uislamu", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan huko El Obeid walitoa hotuba ya kisiasa mnamo Disemba 23, 2021 katika Uwanja wa Uhuru, ambapo Ustadh Muhammad Dafa Allah alizungumza, akielezea jinsi Uislamu unavyodhibiti uhusiano wa mtu kwa Muumba wake, uhusiano wa mtu na nafsi yake na uhusiano wake na wengine, na ni mfumo wa mambo ya maisha. Sio tu dini ya kitheolojia wala dini tu ya kipadri, na huondoa dhulma ya kidini, ikieleza jinsi ya kukidhi ghariza na mahitaji ya kimwili katika mfumo wa Kiislamu, na jinsi ya kukidhi ghariza na mahitaji ya kimwili katika mfumo wa kirasilimali, ambao imeturithisha mateso na ugumu wa maisha kwa sababu unatoka kwa mwanadamu dhaifu na mwenye kikomo, na ili watu waishi maisha ya staha, ni lazima nidhamu za Uislamu zitekelezwe, na hili linaweza kufanywa tu ndani ya kivuli cha dola; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

"Uongo wa mabadiliko ya kidemokrasia", chini ya anwani hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Magharibi, baada ya Disemba 22, 2021, walitoa hotuba ya kisiasa katika soko la Libya ambapo Ndugu Ishaq Muhammad Husayn alianza kwa maswali: Tuko wapi hivi sasa? Na tulikuwa wapi? Na tugeukie wapi? Tangu mwaka 1899 tumekuwa chini ya minyororo ya ukoloni, ambapo kafiri mkoloni alitekeleza mifumo yake ya kibinadamu katika uchumi, utawala, vikwazo na mahusiano ya kigeni kwa mujibu wa mtazamo wake, hivyo Muislamu chini ya ufalme wa Uingereza alikuwa akipigana na ndugu yake Muislamu chini ya bendera ya Italy au Ufaransa.

Chini ya anwani hii: Mabadiliko Yanayotamaniwa, mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Omdurman Magharibi walitoa hotuba ya kisiasa leo, Jumanne, Disemba 28, 2021, katika soko la Libya, ambapo Ndugu Yassin Shugar, aliutaja umati wa watu ambao hutoka mara kwa mara, wakiimba ustaarabu au kutaka mabadiliko ya watu.

Mnamo tarehe 29 Disemba 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Kaskazini kwenye eneo la Sabreen Point yenye kichwa: "Uhuru kati ya Taarifa potofu na Ukweli", ambapo Ustadh Walid Muhammad alizungumza, ambaye alielezea uhalisia wa uhuru, ambayo ina maana ya ukombozi kutoka kwa vikwazo vya kisiasa, kithaqafa na kiuchumi vya mkoloni. Je, Sudan ilikuwa huru kutoka kwa kafiri mkoloni na kukombolewa kutoka kwa vikwazo hivyo?

Je, Sudan ni huru kweli? Chini ya anwani hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika mji wa El Obeid mnamo Disemba 30, 2021 katika Uwanja wa Uhuru, ambapo Ustadh Hussein al-Hadi alizungumza, akielezea kuwa uhuru ni udanganyifu wa Magharibi ambao kwao Waislamu wamedanganyika tangu kuondoka kwa mkoloni wa Kiingereza na majeshi yake tu na kutuacha tukiendelea kifikra na kithaqafa, na kutuacha tukiitukuza bendera ya Sudan iliyobadilishwa na bendera ya Mtume wetu (saw) na tukauacha mfumo wa kijamhuri utawale badala ya Khilafah ya Kiislamu. Mkoloni alitoka na kutuekea watawala kutoka miongoni mwa watu wetu wanaotawala na tawala zake za Magharibi katika utawala, uchumi, sera ya kigeni na ya ndani, na elimu. Alijitengezea mawakala kwa ajili yake ambao wanahifadhi maslahi yake kabla ya maslahi ya watu wao. Uhuru ni hadaa na umma hauwezi kuwa huru katika uamuzi na ubwana wake kwa msingi wa imani yake isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili ambyao itaregea hivi karibuni, InshaAllah. Kutawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, kisha Uislamu ubebe ujumbe wa uongofu na nuru kwa ulimwengu na kuusalimisha kwa mamlaka ya Uislamu.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu