Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wilayah Sudan: Ripoti ya Habari 13/10/2021

Amali za umma zinazofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ziliendelea katika majimbo anuwai ya nchi ili kuunda rai jumla yenye utambuzi kuhusu vifungu vya Uislamu na masuluhisho yake yanayohusiana na nidhamu tofauti tofauti za maisha. Zilishughulikia mada anuwai, ikiwemo mfumo wa utawala katika Uislamu, mapinduzi ya kijeshi, ukiukaji wa usalama, matatizo ya elimu, na matukio ya mashariki mwa Sudan na mengineyo.

"Taasisi za Dola ya Khilafah katika Utawala na Idara," chini ya anwani hii Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitenga kona katika vyuo vikuu ya mazungumzo na majadiliano katika Chuo Kikuu cha Al Neelain, Kitivo cha Mafunzo ya Uchumi na Jamii mnamo Jumatatu, Septemba 20, 2021, ambapo Yasser Abdullah alielezea uhalisia wa Khilafah kama nidhamu ya utawala ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameikubali kwa Waislamu.

Chini ya anwani hii: "Matatizo ya kibinadamu hayatatatuliwa isipokuwa kupitia Khilafah ya Kiislamu," Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la magharibi mwa Omdurman mnamo Septemba 22, 2021 katika Soko la Libya, ambapo Ustadh Abd al-Rahim Abdullah alizungumza, ambapo alisema kuwa tangu uhuru, serikali sita zimepitia Sudan tangu uhuru: tatu za kijeshi na tatu za kiraia, zilikuwa pande mbili za sarafu moja, ambayo ni Urasilimali, na lilikuwa ni janga kwa taifa.

"Khilafah ndiyo pekee ya kukomesha mapinduzi na upiganiaji mamlaka," chini ya anwani hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Dukhainat walitoa  hotuba ya kisiasa katika Soko la El Kalakila El Lafa mnamo Septemba 23, 2021, ambapo Ustadh Al-Fateh Abdullah alielezea kuwa sababu ya mapinduzi ya mara kwa mara ni kwamba wanasiasa wetu huuchukulia Utawala na mamlaaka kuwa keki, kwa hivyo wanavipigania, wamezama katika shida zao za maisha zilizo sababishwa na wanasiasa hao hao kwa kupitisha mfumo wa kirasilimali uliojengwa juu ya ushuru na mikopo ya riba iliyowalemea watu.

Kwenye mada hiyo hiyo; Mapinduzi Kijeshi: Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Madani katika kituo cha basi huko Al Souq Al Kabeer mnamo Septemba 28, 2021 yenye kichwa: "Mapinduzi ya kijeshi sio suluhisho la mgogoro wa kisiasa, bali suluhisho ni kuuleta Uislamu mamlakani kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida.”

"Je! Mabadiliko yanatokeaje?" Mnamo Septemba 29, 2021, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi, katika Soko la Libya, ambapo Ustadh Ishaq Muhammad Hussein alianza hotuba yake kwa kusema kwamba mwanadamu amefanywa kupenda mabadiliko, kujielimishwa na vivyo hivyo mataifa pia. Umma uliorudi nyuma unataka kufufuka na kusonga mbele, lakini mabadiliko haya yanatokeaje? Je! Ni mapinduzi ya kijeshi? Au uchaguzi unaozileta serikali za raia? Yote haya yalitokea nchini Sudan, na hakukuwa na mabadiliko yaliyotarajiwa.

Chini ya kichwa: "Usalama Uhalifu nchini Sudan, Sababu na Matibabu," Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la El Obeid katika Souq al-Kabeer karibu na Msikiti wa Suwar al-Dahab mnamo Septemba 29, 2021. Ustadh Faisal Makki alizungumzia sababu za ukosefu wa usalama nchini Sudan na kwamba kuna viungo vingi vya mamlaka, ambayo vilifanya vituo vya kufanya maamuzi kuzidi.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Dukhainat pia walitoa hotuba ya kisiasa katika Soko la Al Kalakila mnamo Oktoba 6, 2021 yenye kichwa: "Migogoro ya Sudan inaweza tu kutatuliwa na Khilafah Rashida," ambapo Ustadh Abdullah Hussein alizungumzia juu ya shida za utawala na uchumi wa Sudan, mkutano, elimu, usalama, na mengine, na akaelezea kuwa shida hizi zinatokana na kushindwa kuufanya Uislam kuwa msingi wa utawala.

"Migogoro ya Sudan inazidi na Khilafah ndio suluhisho." Chini ya anwani hii, Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi mnamo Oktoba 6, 2021, katika Soko la Libya, ambapo Sheikh Babiker Mahdi aliwasilisha matatizo ya Sudan, kama vile mgogoro wa mkate na uhaba wa mkate na maji, ukosefu wa usalama na kupanda kwa bei. Alidokeza pia kwamba Hizb ut Tahrir ameandaa katiba ya nchi hii yenye vifungu 191 vilivyotokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (saw). Hizb ut Tahrir inatoa wito kwa watu kuhamasika kujiunga nayo ili kuvitabikisha vifungu hivi.

Chini ya kichwa "Matukio ya Mashariki katika Mizani ya Uislamu," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika mji wa Gedaref mnamo Oktoba 9, 2021, ambapo Ustadh Maysara Yahya alizungumzia uhalisia wa tatizo, sababu zake na jinsi ya kutibu kutoka kwa Uislamu. Na alionyesha ufisadi wa mafungamano ya kikabila, kikanda au kitaifa ambayo kwayo baadhi ya watu wa mashariki mwa Sudan walikuwa wamepotea, na kwa hivyo wanafuata njama za makafiri wa kikoloni ya kuichana nchi yao mikononi mwao.

Hadhira ilifanya maingiliano na uwasilishaji mzuri na wakaishukuru Hizb ut Tahrir kwa kuzungumzia suala hili muhimu na maslahi yake katika kadhia za Waislamu kwa jumla, na moja ya maingiliano yaliyothaminiwa sana ilikuwa ni ujumbe wa maandishi kutoka kwa mmoja wa dada akionyesha imani yake kwa Hizb ut Tahrir na kukisifu kama chama tunachokitegemea kwa sababu katiba yake ni Dini na Sharia. Na akaandika, "Tuko pamoja nanyi, na hatukubali kudhalilishwa au matusi."

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya mkao wake wa kila mwezi katika jiji la El Obeid mnamo Jumamosi, Oktoba 9, 2021, ambao ulikuwa na kichwa: "Uhalisia wa Elimu nchini Sudan, Matatizo na Tiba," ambapo Ustadh Ahmed Wadaa Abdel Karim alizungumzia matatizo ya elimu nchini Sudan, ambayo yanawakilishwa na serikali kutokubali wajibu wao. Katika elimu, wanasiasa, wanafikra na watu walioelimika waliathiriwa na hadhara ya Magharibi, na dola za kikoloni zililazimisha hadhara na fahamu zao kwa nchi za Kiislamu baada ya kuanguka kwa Khilafah Uthmani kupitia uundaji mitaala ya elimu.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Al-Kalalat walitoa hotuba ya kisiasa katika Msikiti wa Sahaba mnamo Oktoba 8, 2021, baada ya swala ya Ijumaa, yenye kichwa: "Hijra ya Mtume… Ushindi na Tamkini" ambapo Mhandisi Basil Mustafa alisema kwamba Mtume (saw) alihamia Madina siku hiyo hiyo. Ijumaa, tarehe 12 Rabi 'al-Awwal ya mwaka wa kumi na nne wa utume, maana halisi ya hijra ni kwamba ilichora mstari wa kugawanya kati ya hatua mbili za ujumbe wa Kinabii: hatua ya da'wah na hatua ya utekelezaji kivitendo. Hadi 1924 M, ilipovunjwa kwa njama za dola za Kikafiri, Waislamu lazima wafanye kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kuiregesha.

"Sera ya Elimu katika Dola ya Khilafah," chini ya anwani hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walianzisha kona ya mazungumzo na majadiliano katika vyuo vikuu, Oktoba 11, 2021. Shabab, Abdullah Yaqoub na Al-Fateh Abdullah walikuwa wazungumzaji, ambapo mzungumzaji wa kwanza Abdullah alizungumzia hali halisi ya elimu nchini Sudan na kuzorota kwake kwa sababu ya ukosefu wa dira wazi kwa Serikali ya Mpito, maamuzi yake punguani, na kutokuwa na hamu ya elimu

"Tatizo la Sudan Mashariki na Njia za Suluhisho" chini ya kichwa hiki, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katika jiji la El Obeid mnamo Oktoba 13, 2021 mbele ya ukumbi wa swala wa Siwar al-Dhahab, ambapo Ustadh Muhammad Dafa Allah alizungumza, akisema kwamba dhulma inayowapata watu wa Mashariki sio ngeni, bali dhulma hiyo ni ya kihakika kwa watu wote wa Sudan tangu kuingia kwa ukoloni na kulazimishwa kwa mfumo mlafi wa kirasilimali kwa nchi hii, ambapo dhulma imetawala kila mahali.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah yaSudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu