Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: “Ima ikomboeni Palestina au fungueni njia kwa Umma!”

Kwa kuzingatia matendo ya kishujaa yaliyofanywa na Mujahidina mashujaa katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) chini ya kauli mbiu (Kimbunga cha Al-Aqsa) dhidi ya umbile nyakuzi la Kiyahudi, ambalo linaendelea na kuzidi na hujuma yake inayoendelea dhidi ya Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na uzingiraji na ulipuaji wake wa mabomu ambao umeendelea kwa miaka 17 kwenye Ukanda wa Gaza, Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Uturuki inaandaa mikesha jijini Ankara na Istanbul kwa kichwa:

“Ima ikomboeni Palestina au fungueni njia kwa Umma!”

Kukabiliana na hujuma mashambulizi haya ya kikatili na ya kihalifu yanayofanywa na umbile la Kiyahudi, ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya 1,900 na kujeruhiwa zaidi ya 7,000 katika Ukanda wa Gaza kutokana na kurushwa kwa mabomu zaidi ya 6,000 yenye uzito wa tani 4,000, watawala wa nchi za Kiislamu, wakiongozwa na Erdogan wa Uturuki, wamechukua dori ya watazamaji, wakijitosheleza kwa kuwashutumu. Wanamshambulia kila mtu ambaye kwa hakika anajaribu kuhama ili kuwanusuru Waislamu huko Palestina na kuyafunga kwa minyororo majeshi ya Kiislamu yenye nguvu katika kambi zao... Mbele ya mandhari hii ya aibu kutoka kwa watawala, sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Uturuki imetubidi kuandaa tena mikesha hii miwili, baada ya Jumapili iliyopita kuandaa mikesha katika miji 10 mikuu ya Uturuki, kuwanusuru na kuwaombea nusra Waislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na wito kwa majeshi ya Kiislamu kuvunja minyororo ambayo watawala Ruwaibidah wamewaweka ndani ya kambi zao na kusonga mara moja kuwanusuru mujahidina huko Palestina na kuukomboa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa kutoka kwenye makucha ya Mayahudi wanaoukalia kwa mabavu.

Basi kuweni pamoja nasi na mushiriki nasi malipo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu atatunusuru, hata kama ni  baada ya muda.

Jumapili, 30 Rabi’ al-Awwal 1445 H sawia na 15 Oktoba 2023 M

- Wakati na Mahali -

[Mji wa Ankara]

[Mji wa Istanbul]

#Al-Aqsa Flood

#Armies_to_the_Aqsa

#ArmiesToAqsa

#AksaTufanı

#OrdinaryAksaya

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu