Jumamosi, 30 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Somalia Iliyomakinika Kisekula: Ndoto ya Marekani

Na:Ali Nassoro Ali*

Vyombo vya habari vimeripoti kushikwa kwa Mukhtar Robow "Abu Mansur" siku ya Alhamisi, 13 Disemba 2018 akiwa katika mkutano wa kawaida ulioitishwa na rais mshikilizi wa Jimbo la Kusini Magharibi ya Somalia mjini Baidoa. Alishikwa na maafisa wa Ethiopia na mara moja kuhamishwa kambi ya jeshi ya Ethiopia viungani mwa mji kabla kwenda naye Mogadishu.

Mukhtar Robow "Abu Mansur" alikuwa makamu kiongozi na msemaji wa kundi la Al-Shabaab, ambalo mwanzoni lilibuniwa kupigana na "uvamizi wa Ethiopia." Kabla kujiunga na Al-Shabaab, mwanzoni mwa miaka ya 2000 alishiriki katika Jihad dhidi ya Soviet ndani ya Afghanistan ambayo ilipigiwa debe hususan na Saudi Arabia, Pakistan na Amerika. Kisha alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa Vuguvugu la Kiislamu la Somalia, alisaidia kuijenga tena    Al Itihaad Al Islamiyya ambayo ilisambaratishwa mnamo 1997 na jeshi la Ethiopia. Kisha akajiunga na Muungano wa Mahakama za Kiislamu ambazo zilikuwa na mamlaka katika maeneo mengi ndani ya kusini-magharibi ya Somalia kuanzia mwaka 2006 -2007 kisha ikasambaratishwa tena na uvamizi wa Ethiopia.

Mukhtar Robow "Abu Mansur" alikuwa katika orodha ya Marekani ya Zawadi kwa Haki (RFJ) kwa mtu yeyote ambaye atasema alipo kwa kupewa Dola milioni 5 za Marekani terehe 7 Juni 2012. Kisha baadaye alitolewa katika orodha hiyo mnamo 23 Juni 2017 kutokana na mazungumzo baina ya serikali ya Amerika na serikali ya Somalia. Zaidi ya hayo ni kuwa tarehe 13 Agosti 2017 aligonga vichwa vya habari kwa kujisalimisha kwa jeshi la Somalia nakupigiwa upatu kuwa ni uamuzi/uasi wa kihistoria. Kwa mara nyingine tarehe 4 Oktoba 2018 akagonga vichwa vya habari kwa kutangaza kuwa atagombea katika kinyang'anyiro kitakachofanyika tarehe 17 Novemba, 2018 katika Jimbo la Kusini Magharibi (SWS).

Hayo yote yanadhihirisha wazi kuwa hakika Mukhtar Robow si chochote bali ni mtumwa wa Marekani ndani ya Somalia. Kwa kuwa yeye ni maarufu na mwenye ushawishi katika koo yake, hivyo basi, kujitangaza kwake kwa uchaguzi ujao kulisukumwa na Serikali Kuu ili aweze kupambana na Sharif Hassan Sheikh Aden, ambaye wakati huo alikuwa rais wa Jimbo la Kusini Magharibi na alikuwa anazipinga sera za Mogadishu na alikuwa anagombea hatamu ya pili. Lakini mnamo 7 Novemba 2018 Sharif Hassan Sheikh Aden alijiuzulu mara moja baada ya kugundua kuwa hawezi kuhimili mchakato wa Mogadishu na umaarufu wa Robow. Kuondoka kwa Sharif Hassan Sheikh Aden ikawa ndiyo mwisho wa umuhimu wa Mukhtar Robow kwa kuwa kikwazo cha Serikali Kuu ya Somalia hakipo tena. Hivyo basi, Serikali Kuu ikahairisha uchaguzi mara tatu kuanzia 17 Novemba hadi 5 Disemba kisha 19 Disemba 2018. Zaidi ya hayo, waliishinikiza Tume ya Uchaguzi ya Jimbo la Kusini Magharibi ibatilishe ugombeaji wa  Robow kwa kuwa hakupitia Mpango wa Kuwajenga Upya Waasi wa kuwatathmini waliokuwa wanachama wa Al-Shabaab. Lakini, Robow hakutaka kurudi nyuma na hivyo kuilazimisha Serikali Kuu kumtia korokoroni. Hatima yake ikiwa hakushiriki uchaguzi ambao ulishindwa na aliyekuwa Waziri wa Kawi Abdiaziz Hassan Mohamed "Laftagareen" siku ya Jumatano, 19 Disemba 2018.

Amerika inataka kuhakikisha kuwa Somalia inabakia kuwa ya kisekula kiukamilifu ikiendeshwa na vibaraka walioandaliwa kikamilifu mfano Farmaajo na wala sio watu kama "Mukhtar Robow" ambaye bado anaashiria eti Uislamu wa Misimamo Mikali lakini wanaweza kuwatumia watu aina hiyo pale watakapohisi maslahi yao yametishiwa. Licha ya malalamiko ya haki za kibinadamu kutokana na kile kinaochoitwa "zamani yao hatari" umuhimu wao unategemea maslahi ya wakoloni wamagharibi wakiongozwa na Marekani ambaye ndiye mwagaji wa damu wa kwanza ulimwenguni kote na asiyejali haki za kibinadamu kwa kuwa yeye ndiye mmiliki wa mashirika hayo. Hivyo basi, yanayomtokea Mukhtar Robow sio mageni hususan wakati huu ambapo Marekani inataka kuitia mkononi kiukamilifu Pembe ya Afrika kupitia vibaraka wake watiifu wakiongozwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed wa Ethiopia. Kupitia utekelezaji wa sera ya Marekani kuhusiana na Pembe ya Afrika kwa kuziunganisha Ethiopia, Eritrea, Somalia na Djibouti. Hivyo basi, Amerika imemteua Donald Yamamoto kama Balozi wa Somalia baada ya takribani miaka 28 tokea kuangushwa kwa utawala wa kibaraka wao Siad Barre 1991.

Utawala wa Somalia lazima uamke na ufahamu kwamba ushindi, hadhi na cheo cha kweli vinatokamana na amani, usalama na utulivu wa kweli ambao utapatikana tu kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Nayo ni kwa wao kujisalimisha kwa utawala wa Mwenyezi Mungu (swt) kupitia kukumbatia ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah. Khilafah itakayo tawala/hukumu kwa Qur'an na Sunnah na sio kwa mfumo wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake zinazonuka na ikijumuisha ile inayoitwa utawala wa nidhamu ya kidemokrasia, ambayo inadaiwa kuwa ndiyo muongozo sio tu wa Somalia bali wa ulimwengu wote.

وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً"" “Na nani aliye mbora zaidi katika Kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu”

*Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

*Imeandikwa Kwa Ajili ya Gazeti la Ar-Rayah –Toleo 217

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 18 Aprili 2020 15:47

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu