Jumamosi, 30 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amerika Yakazanisha Kitanzi Katika Shingo ya Somalia Kupitia Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB)

Na: Ali Nassoro Ali*

Somalia kwa takribani miongo mitatu ilikuwa haistahili kupata pesa kutoka kwa Muungano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Benki ya Dunia (IDA) kwa sababu ilikuwa inadaiwa na Benki hiyo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zaidi ya dolari milioni 800 ambazo ni sehemu ya dolari bilioni 5.5 za deni ambalo kiwango kikubwa ni riba na faini inazodaiwa na mashirika ya kimataifa na wakopeshaji wa kibiashara katika miaka ya 1980.  Amerika ikiwa ndio inayoongoza msururu miongoni mwa wale walioikopesha nchi hiyo pakubwa katika kipindi cha Rais Mohamed Siad Barre aliyekuwa anaegemea Amerika. Hivyo basi, mashirika yanayomilikiwa na Amerika yakaingia katika mchakato wa mabadiliko ili kuiwezesha Somalia kufutiwa madeni yake na kuanza kupokea mikopo mipya!

Juhudi za mpango mrefu baina ya inayoitwa ‘Serikali Mpya ya Somalia’ na maafisa wa IMF na WB wanaofanyakazi ndani ya Mogadishu zikazaa matunda na hivi majuzi imeripotiwa kuwa Somalia imetimiza masharti yote 27 ya fedha ulimwenguni ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambayo yaliwekwa ili kuipa afueni kutokana na deni lake lililopo (Radio Dalsan, 22/09/2018).

Fauka ya hayo, Benki ya Dunia imeidhinisha dolari milioni 80 kama ruzuku kwa Somalia ili kufadhili marekebisho ya fedha za umma, ikiashiria mgao wa kwanza kwa serikali ya nchi iliyo zama kwenye mzozo kwa miaka 30, benki hiyo ilisema (Radio Dalsan, 27/09/2018).     

Somalia ni nchi iliyo na Waislamu wengi ambayo ni muathiriwa wa vita vya ndani kwa ndani vya wakoloni wa Kimagharibi baina ya Amerika na Ulaya hususan Uingereza ili kudhibiti na kufuja rasilimali zake nyingi hususan mafuta na kuutumia mlango wake wa Bahari Nyekundu. Hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya kuanguka kwa Mohamed Siad Barre mtawala kibaraka wa Amerika mnamo Januari 1991, kwa kuwa takribani thuluthi mbili za Somalia ilikuwa imetengewa makampuni makubwa ya Kiamerika Conoco, Amoco, Chevron na Phillips katika miaka ya mwishoni kabla ya Raisi Mohamed Siad Barre kupinduliwa na taifa hilo kuzama katika ghasia.

Ili kuziokoa haki za kibiashara za kampuni hizo, utawala wa Bush uliamua kutuma vikosi vya Amerika (uvamizi) ili kulinda uwekezaji wao wa mamilioni ya dolari chini ya guo la kuhifadhi shehena za misaada za Somalia.      

Mkono wa Amerika na ufujaji wake ndani ya Somalia unaendelea pasina kutingishika huku Mohamed Abdullahi “Farmajo” Mohamed akiwa kama Raisi wake wa sasa tangu 2017. Fauka ya hayo, sera za Kiamerika tangu enzi za Siad Barre hadi leo zinatilia maana tu kuzifuja rasilimali za Somalia.

Lakini, kwa kushindwa vikosi vya Amerika nchini Somalia kutokana na muitiko wa Waislamu kote ulimwenguni wa kuungana chini ya bendera ya “Jihad ili kuwafurusha wavamizi”. Amerika ilifedheheshwa licha ya silaha zake na mafunzo yake ya kiufundi ya hali ya juu katika vita ikilinganishwa na zile za “Mujahidina.”

Tangu wakati huo Amerika imebadilisha mbinu na badala yake kutumia mwito wa kuweka demokrasia na marekebisho ya usimamizi kwa taasisi za Somalia. Kidhati, inamaanisha kuwa Amerika inajaribu kuwafinyanga Wasomali kwa thaqafa nzito ya kisekula ya kimagharibi na maadili yake kiasi cha kuwa kitambulisho chao cha Kiislamu kifutwe kikamilifu! Ili kupata malengo yake maovu Amerika inatumia taasisi zake za kifedha ikiwemo na sio pekee IMF na WB katika kuisaidia serikali ya Somalia kwa fedha zinazo hitajika ili kuinua serikali hiyo na kuhakikisha kuwa inapitisha na kutekeleza sera zake nchini Somalia. Hivyo basi, dori msingi ya IMF na WB ni kujihusisha na kuiteka dola hiyo na kulazimisha sera na wala sio kuchunga mambo ya raia wa Somalia! Kama ilivyo thibitika mnamo 2017 ambapo zaidi ya Wasomali milioni 6 walikabiliwa na baa la njaa huku moja ya sababu zake ikiwa ni kurefuka kwa vita vya kiwakala vinavyoongozwa na Amerika kwa jina la Ugaidi na Misimamo Mikali lakini ukweli ni kuwa vita hivyo vya kiwakala vinalenga kuifuja nchi hiyo!  

Ni dhahiri shahiri kuwa Amerika na taasisi zake za fedha sio tu ni maadui wa Somalia bali pia kwa Kenya ambayo hivi majuzi ilipitisha Mswada wa Fedha 2018 uliomulika mapendekezo ya IMF yaliyopelekea kuwasukuma Wakenya katika maisha ya umasikini zaidi! Suluhisho la haraka zaidi ni kwa Somalia, Kenya na Afrika yote kukata mafungamano na taasisi hizi za Kimagharibi kama IMF na WB zinazo pigia debe sera zenye sumu za mfumo wa kisekula wa kirasilimali chini ya guo la viholoso!

Badala yake, zikumbatie ulinganizi wa Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah haitadhamini tu mwamko halisi wa Afrika bali pia itawafurusha wakoloni masekula na hivyo basi kurudisha matumaini ya Afrika ndani yake na kutumia uwezo wake wote katika kupatikana kwa utulivu na ufanisi.   

*Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

*Imeandikwa kwa Ajili ya Gazeti la Ar-Rayah – Toleo 207

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:50

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu