Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Gazeti la Al-Rayah

Vita vya Kujifanya vya Trump kwa Kampuni za Mitandao ya Kijamii

Na: Dkt. Abdullah Robin

Mojawapo ya nukuu za tweet za Trump inasoma, “HAKUNA NJIA (SIFURI!) yoyote kwamba kura zinazo letwa kupitia njia ya posta kwa vvovyote vile zitakuwa na ulaghai mkubwa. Visanduku vya posta vitaibiwa, kura zitaghushiwa na hata kuchapishwa kinyume cha sheria na kutiwa saini kilaghai. Gavana wa California anatuma Kura kwa mamilioni ya watu, yeyote…” Ni ajabu kwamba Raisi wa dola inayojigamba binafsi kuwa ndio yenye demokrasia kubwa zaidi ulimwenguni anadai kupitia nukuu hii ya tweet kwamba nchi yake haiwezi kuandaa uchaguzi huru na wa haki. Pengine hilo ndilo lililo peleka mtandao wa Twitter kuikashifu tweet yake, zaidi kuliko ukweli kwamba aliyodai yalikuwa na shaka. Trump alionekana kushtuka wakati ‘Twitter’ ilipo ambatanisha ilani katika tweet hiyo kuashiria kwamba yale aliyo sema kuhusu uchaguzi ujao hayakuwa sahihi. Twitter ni jukwaa la mtandao wa kijamii aupendao zaidi Trump kwa kudumisha mawasiliano na wafuasi wake elfu thamanini, ambao ameutumia kutuma maelfu ya tweet wakati tofauti tofauti mchana au usiku. Kampuni za mitandao ya kijamii kama Twitter zimekuwa chini ya shinikizo kwa tuhuma za uongo au za kuumiza katika jukwaa lao tangu uchaguzi wa 2016, ambao umeshuhudia wimbi la habari ghushi na kuongeza wasiwasi kuhusiana na nguvu za mitandao ya kijamii katika kusababisha madhara na vurugu kupitia habari za uongo ama za kupotosha. Pamoja na nadharia za kinjama za ubabaishaji na tiba bandia zinazo zunguka wito wa janga la Covid-19 kwa majukwaa ya mitandao ya kijamii kuchukua hatua kuzidi. Hatimaye, kampuni ya Twitter ikaamua kulenga tweet ya Raisi wa Amerika kwa nembo za kuwaonya watumiaji kwamba maalumati yaliyomo katika tweet yake hayakuwa sahihi.

Trump alijibu kwa kutia saini amri ya utendaji mnamo 28 Mei, ili kufuta kifungu cha 230 cha Sheria ya Adabu ya Mawasiliano, ambacho kinalinda kampuni mfano wa Twitter na Facebook kutokana na hatua za kisheria, kwa maalumati yenye madhara katika majukwaa yao. Hata hivyo wataalamu wa kisheria wamehitimisha kwa kusema kwamba amri hiyo ya utendaji haina athari yeyote kisheria. Zaidi ya hayo, Trump kihakika anafaidika na kifungu cha 230 kwa sababu kinapeana uhuru wa kutumia mitandao ya kijamii bila ya kuchukuliwa hatua kwa uongo wake na matusi yake, na ni dhahiri kwamba amri yake ya utendaji ni mbinu tu ya kuzifanya kampuni za mitandao ya kijamii kuwa na tahadhari zaidi kuhusiana na kuzikashifu jumbe za siku za mbeleni. Twitter inaonekana kuelewa haya, kwa sababu baadaye iliambatanisha onyo katika tweet iliyo fuatia ambayo Trump alitishia kuwapiga risasi watu waliokuwa wanafanya fujo na kupora jijini Minneapolis baada ya polisi kumuua mtu mmoja mweusi aliyekuwa mikononi mwao ambaye hakuwa amejihami kwa silaha yoyote. Twitter ilituma onyo juu ya tweet hiyo, ikisema “imekiuka Sheria za Twitter juu ya utukuzaji vurugu.”

Huku uhasama ukiongezeka kati ya Twitter na Trump, kampuni nyingine ya mitandao ya kijamii ina mahusiano mzuri na Trump. Facebook ilichangia ushindi wa Trump 2016 na kampeni za uchaguzi za Trump endelea za sasa zinaendelea kunufaika kutokana na ukusanyaji maalumati wa Facebook na kuongeza uwezo wa kupima ili kushawishi wapiga kura wapinzani. Trump wakati mmoja alijigamba kwamba Mark Zuckerberg wa Facebook alimpongeza yeye kwa kuwa “nambari moja kwenye Facebook.” Wanachama wa chama cha Amerika cha Conservative ambao wanamuunga mkono Trump mara nyingi wanalalama pamoja na Trump kwamba mitandao ya kijami imetawaliwa na wana-liberali ambao wanaupendeleo dhidi ya wana-Conservative wakati wakihariri au kuondoa jumbe za upotoshaji. Hata hivyo, matangazo yanayo lenga kampeni yanaendeshwa na mashine ambazo zinaubora zaidi wa kuathiri watu kuliko tukio uhariri usio wa mara kwa mara wa jumbe maalumu. huku watu wakijadili kuhusu ni kwa nini baadhi ya jumbe za Trump zinatajwa kuwa za kimakosa ama zakupotosha na Twitter, Facebook itakuwa inalenga maelfu ya jumbe zilizo andaliwa kwa makini kwa makundi maalumu ya wapiga kura walio ratibiwa kwa umakini ili kila mmoja aone jumbe pekee zitakazo mshawishi katika upande aupendao. Trump angali anashinda vita vya habari za kupotosha nchini Amerika na kwa kila janga jipya linalo kumba nchi yake, Waamerika wanagawanyika na kuchukiana wao kwa wao zaidi ya ilivyo kuwa na mashabiki wake wanabaki na yeye. 

Chanzo: Gazeti la Ar-Rayah Toleo la 289, lililo chapishwa mnamo 03/06/2020

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 20 Juni 2020 14:08

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu