Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Gazeti la Al-Rayah

Uhasama kati ya India na China: Fursa ya Pakistan kuikomboa Kashmir

Na: Abdul Majeed Bhatti

Hivi karibuni, Uchina imepeleka maelfu ya vikosi vya kijeshi katika Mstari Halisi wa Udhibiti (LAC) ikizidisha mvutano na majirani zao India. Kukabiliana na hatua hizi, India ikapeleka vikosi vingi ili kusaidia vilivyoko. Mvutano kati ya nguvu hizi mbili za kinyuklia umekuwa ukitokota kwa muda, hata hivyo, ujanja wa kijeshi wa hivi karibuni unahatarisha kurudiwa kwa vita vya Sino-India vya 1962.

Huko nyuma, mpaka mrefu wa Himalaya wa urefu wa kilomita 3,225 unaogawanya India na Uchina umekuwa nukta tete sehemu ya Aksai Chin. India ilidai Aksai ni sehemu ya Kashmir, na Uchina ikaichukulia ni sehemu ya Xinjiang. Vita vifupi vilivyo sababisha Uchina kuteka utawala wa Aksai Chin na kugeuza LAC kuwa mpaka unao tawaliwa na Uchina pekee. India haikutambua mpaka huo na kwa miaka pamekuwa ni chanzo cha mivutano na uvamizi katika LAC na pande zote mbili.

Kutoa msaada kwa Trump ili kupatanisha mzozo huu kumeleta utata zaidi na ukazua shaka ndani ya Beijing kwamba Washington na new Delhi zinapiga ngoma za vita kimakusudi. Uchina inateseka kutokana na vita vya kibiashara na Amerika na kutishika zaidi na kampeni ya Amerika kiulimwengu ya kufuatilia adhabu dhidi ya Uchina kwa kuanzisha Covid-19. Amerika imetuma manuari kushika doria bahari za kimataifa katika bahari ya China Kusini, na Wizara ya Biashara ya Amerika imefanikisha kuharamisha uuzaji wa vipuri kwa Huawei. Huawei inatilia shaka tamaa ya Uchina kutawala 5G na Al, na kwa kupeana miundo msingi ya mawasiliano kwa onyesho lake la mradi wa 'Belt Road' (BRI).

Uchina pia unaogopa zaidi kuingiliwa na Amerika kwa mambo yake ya kindani. Amerika ingali ina sauti kuhusu dori ya Uchina nchini Hong Kong, na Amerika tayari imepitisha mswada unao waadhibu maafisa wa Uchina wanao husika katika kuwanyanyasa Waislamu wa Uighur. Mswada mwengine uko njiani ukitaka kuiadhibu China kwa unyanyasaji wake wa watu wa Tibet. Ubwana wa kujitawala wa Tibet ndio sababu msingi ya Uchina kupigana na India mwaka wa 1962, wakati New Delhi ilipo chochea uasi katika jimbo hilo.

Kwa ushahidi, kujijenga kijeshi kwa Uchina katika eneo la LAC ni sehemu ya mkakati jumla ilio buniwa ili kuizuia Uchina kutokana na majaribio ya Amerika ya kuidhoofisha. Beijing pia inaandaa ulinzi wake katika ufuo wa bahari ya China Kusini kwa kujenga ngome za kijeshi katika visiwa vyingi. Kando na kuimarisha ulinzi wa kijeshi, Uchina umebana kiganja chake juu ya Hong kong kupitia mpango mpya wa kiusalama ambao una ruhusu Jeshi la Raia la Ukombozi (PLA) kuweka utulivu kwa nguvu. Fauka ya hayo, Uchina umetumia nguvu zake za kiuchumi kuiadhibu Australia – imewekea ushuru wa 80% kwa shayiri (mawele) inayo ingizwa – kwa kutoa rai ya uchunguzi huru kwa vyanzo vya Covid-19.

Kijuujuu inaweza kuonekana kana kwamba Amerika imesukuma Uchina Ukutani, ikidhoofisha uwezo wake wa kujibu mashambulizi. Haya ni madai ya kirongo. Kwa upande wa kijeshi, Uchina unamiliki nafasi nzuri dhidi ya washirika wa Amerika katika eneo hilo. India, Korea Kusini, Japan na Australia zinategemea sana nguvu za Amerika kuweka sawa mizani dhidi ya Uchina. Tangu 2008, uwezo wa Amerika kuonyesha na kudhibiti nguvu umeshuka. Amerika ilifanya marekebisho itikadi yake ya kivita ili kupigana vita vimoja vikubwa na sio viwili. Fedheha iliyoipata nchini Afghanistan kupitia jeshi la akiba na kupapatika kwa Trump kutaka kujiondoa kwa kudumu kumeharibu fahari ya Amerika.

Kwa upande wa mtazamo wa kiuchumi, Uchina imepona kutokana na Covid-19, ilhali uchumi wa Amerika ungali vibaya. Kutokana na uchaguzi unao karibia kwa haraka, Trump hawezi kuhatarisha vita. Zaidi ya hayo, utajiri jumla (GDP) wa Muungano wa Usovieti ulikuwa ni asilimia 50 ya uchumi wa Amerika, na Wanasovieti walishindana na Amerika ana kwa ana kwa zaidi ya miaka arubaini. Leo, uchumi wa Uchina ni asilimia 65 ya uchumi wa Amerika, na inakadiriwa kuupita wa Amerika miaka michache ijayo. Hivyo kama vita vitatokea kati ya India na Uchina, je Amerika iko na uwezo wa kuizuia Uchina? Hakuna uwezekano. Mnamo 2008 na 2014, Amerika

 

haikuwa na nguvu za kuizuia Urusi dhidi ya kuivamia Georgia, na kuiteka Crimea kutoka kwa Ukraine. Uchina ya 2020 iko imara zaidi ya Urusi, na inapeana changamoto kubwa kwa ukubwa wa Amerika katika Asia Pasifiki, na sehemu za Eurasia.

Kama vita vitatokea kati ya India na Uchina, Pakistan itakuwa na fursa ya dhahabu tangu 1947 kuikomboa Kashmir milele. Kuliko kuzikabili nguvu zote za kijeshi za kawaida za India, Pakistan itapata uhafifu, lakini jeshi la India litatumika sana … Huku idadi ya watu wa Kashmir ikiwa upande wa Pakistan kikamilifu, uwezekano wa kuikomboa Kashmir kutoka katika utawala wa Kibaniani uko juu. Silaha za kinyuklia za Pakistan zinapaswa kuhakikisha kwamba majeshi yake yanaweza kufanya kazi ndani ya duara la mbinu rasmi za kijeshi ili kufaulisha ushindi mkubwa wa kisiasa juu ya India.

Kuna hatari ndogo sana ya vita vya kinyuklia. Kinyume ni kuwa, silaha za kinyuklia zinazuia mizozo ya kawaida kuzidi mpaka kufikia kuwa vita vya kinyuklia. Hivi ndivyo haswa ilivyo tokea wakati wa mzozo wa Kargil mnamo 1999, na pia wakati wa vita vya mpaka wa sino-russia vya 1968. Ushindi ungekuwa mwepesi, lau Pakistan ingehamasisha Waislamu milioni 250 ndani ya India – ambao wamenyanyaswa sana na BJP – kufanya uasi wa kiraia na kupanga mipango ya kijeshi pamoja na Uchina.

Kwa ushirikiano na Uchina ufaulu, Pakistan lazima ihakikishie Beijing kwamba Islamabad haitoisaidia India kwa amri ya Amerika. Mnamo 1962, Ayub Khan aliunga mkono sera za Amerika kwa kutounga upande wowote waziwazi lakini kisiri akaisaidia India kwa kushajiisha utaifa wa Kitibetan dhidi ya Beijing. Kuna shaka chache kwamba Modi na Trump watamuomba Imran Khan afanye hivyo hivyo.

Serikali za awali ziliufunga kikamilifu usalama wa taifa na maslahi ya Amerika na zikateseka. Pakistan iliipa uwezo India juu ya Kashmir mnamo 1965, ikaipoteza Pakistan Mashariki mnamo 1971, ilitelekezwa baada ya jihad ya Afghan mnamo miaka ya tisiini na kusalimisha kina chake cha kistratejia mnamo 2001. Baya zaidi ya yote, Amerika ikaitupa Pakistan baada ya 9/11 na kuifanya India kuwa wakala wake mkuu katika eneo. Je, Imran Khan na Bajwa wanamiliki imani ya kimaadili ili wajiondoe kwa usafi katika utumwa wa Amerika na kuikomboa Kashmir? Sote tunajua jibu la hili.

Gazeti la Al-Rayah Toleo 289, Limechapishwa mnamo 03/06/2020

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 20 Juni 2020 13:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu