Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ziara ya Waziri wa Kigeni wa Zamani wa Amerika Tillerson Barani Afrika ililenga Umwagaji Damu Zaidi ya Waislamu Kwa Kisingizio cha Mipango ya Vita Dhidi ya Ugaidi 

Na: Ali Nassoro Ali*

Ziara hiyo ilidokezwa na afisa mkuu wa Wizara ya Kigeni kama ufuatiliziaji juu ya mkutano kati ya Waziri Tillerson na mawaziri wa kigeni wa bara la Afrika jijini Washington mnamo Novemba 2017 ulioandaliwa kwa haraka na ambao uhudhuriaji wake ulikuwa mbaya. Ingawa mkutano huu wa mawaziri uligusia kadhia za kibiashara, maendeleo na usalama.

Ziara ya mwisho ya Tillerson iliweka kipao mbele ushirikiano wa kiusalama na usaidizi wa Amerika kwa washirika wake muhimu barani Afrika katika vita dhidi ya al Shabaab nchini Somalia na Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na eneo la Ziwa Chad.

Sera ya Donald Trump ya kuiweka 'Amerika Mwanzo' inalenga kuwatazama wachezaji wengine ima kama washirika au mahasimu au vikwazo katika matarajio ya Amerika ya kisiasa ya kiulimwengu yeye akiwa kama bwana mkuu. Amerika kwa mtizamo wa sera hiyo ni lazima ilazimishe mamlaka yake na ijitanue kama mdhamini wa kiusalama wa kiulimwengu. Kufikia kiwango cha kukarabati na kuboresha sera yake nambari moja ambayo ni kuhakikisha kuwa Uislamu kama mfumo badili hausimami tena dhidi ya mfumo wa kisekula wa kirasilimali ambao Amerika na washirika wake wanang'ang'ana katika kuudumisha kutokana na kudhihirika kuporomoka kwake. Amerika iliamua kuzuru vibaraka wake wa Kiafrika wanaodaiwa kuwa washirika wakuu katika vita dhidi ya ugaidi na mapendekezo kwa kila mshirika kama yafuatayo:   

Kwanza, Ethiopia, iliyo na jeshi kubwa na imara eneo hili, imekuwa ikipigana na al Shabaab tangu 2008. Nchi hiyo inakumbwa na mtafaruku mbaya wa kisiasa na kutojulika hatima yake, lakini ziara ya Tillerson jijini Addis ilitawaliwa na wasiwasi wa kiusalama. Alitumia ziara yake kuhakikisha upya usaidizi wa Amerika kwa serikali hiyo, na kutahadharisha serikali hiyo kutoruhusu kadhia za kindani za kisiasa kuipoteza mwelekeo kutokana na juhudi za vita dhidi ya ugaidi eneo hilo.

Pili, Djibouti, nchi ndogo sana yenye idadi ya wakaazi chini ya milioni moja, imehudumu kama kitovu cha oparesheni za Kiamerika eneo hilo. Huku kimikakati ikiwa iko kaskazini mwa Somalia na upande wa pili wa Bahari Nyekundu kutoka nchi iliyo sambaratishwa na vita ya Yemen. Djibouti ni makaazi ya maelfu ya majeshi ya Amerika katika kambi ya Lemonnier, ambayo ni idadi kubwa zaidi ya mkusanyiko wa majeshi ya Amerika barani Afrika. Maadamu al Shabaab bado ni tishio nchini Somalia, kambi ya Lemonnier itakuwa ndio kitovu cha mtandao wa mashambulizi ya Amerika eneo hilo. Ziara ya Tillerson nchini Djibouti pia ililenga kukabiliana na kukua kwa ushawishi wa China na uwepo wake nchini humo. Katika muongo uliopita, China imemimina mamilioni ya dolari ndani ya kijinchi hicho kidogo na imekuwa ikifanya bidii kujimakinisha kuwa mshirika nambari moja wa maendeleo na usalama wa Djibouti. Hivi majuzi Beijing ilikamilisha miradi miwili mikuu nchini Djibouti: mradi wa mamilioni ya dolari wa barabara ya reli kuelekea nchini Ethiopia na kambi ya kwanza ya kijeshi ya China ng'ambo, jengo pana linaloshinda lile la Amerika.

Tatu, Kenya, ambayo imekuwa mlengwa wa mashambulizi mabaya ya kigaidi kutoka kwa al Shabaab, iko na maelfu ya vikosi vyake nchini Somalia kama sehemu ya AMISOM. Hivi majuzi ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, Amisom, ambao majeshi ya Kenya, KDF, ni sehemu yake, uliungama juu ya muda wake wa kujiondoa kutoka Somalia kufikia 2020 na kusema kuwa muda huo hauna hakika.

Tillerson alikwenda kuihakikishia upya Kenya, mshirika wa kale wa kiusalama wa Amerika eneo hilo, kuendelea kwa Washington kutoa usaidizi wa kijeshi, kijasusi na kifedha ili kubakia vitani nchini Somalia.

Nne, Nigeria, mahusiano ya kiusalama kati ya Amerika na Nigeria daima hayaja kuwa shwari na maafisa wa Nigeria siku za nyuma wamekiuka mipaka ya Amerika katika ununuzi na umiliki wa zana za kijeshi za Kiamerika, hususan rasilimali za ndege. Tillerson alikwenda kuwahakikisha upya usaidizi wa Amerika kwa Nigeria huku akishajiisha maafisa wake kuzidisha vita dhidi ya Boko Haram na kuimarisha ushirikiano wao na dola nyenginezo eneo hilo ambako Boko Haram inaendesha shughuli zake.

Tano, Chad, mwanachama imara zaidi wa G-5, mtandao wa mataifa matano ya kieneo yanayo pigana vita dhidi ya ugaidi dhidi ya Boko Haram eneo hilo, Chad imefedheheshwa na kutajwa na utawala wa Trump kama moja ya nchi nane kuu za Waislamu ambazo raia wake wamepigwa marufuku ya kusafiri nchini Amerika. Tillerson alikwenda kuwashukuru maafisa wa Chad kwa dori yao wanayo cheza katika kupigana na Boko Haram huku akiwahakikishia upya kimya kimya kwamba Wizara ya Kigeni ya Amerika itafanya kila iwezalo kuitoa Chad kutoka kwa orodha ya nchi zilizo athirika na marufuku hiyo ya usafiri.  

Kwa kutamatisha, licha ya majaribio kadhaa ya uongozi wa Amerika ambayo mikononi mwake damu inachirizika na washirika wake kuukoa mfumo wao batili wa kisekula wa kirasilimali kutokana na kuporomoka, Umma wa Kiislamu utabakia imara na kupinga walinganizi wote wa batili walio dhidi ya mwamko na kushikamana juu ya mradi wa Khilafah ambayo itasimama tena hivi punde kwa njia ya Mtume (saw) kwa baraka na usaidizi wa Allah (swt).

(إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ) “Kwa hakika, makafiri hawafanikiwi.” [Al-Muminoon: 117]

*Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir Kenya

*Imeandikiwa kwa ajili ya Gazeti la Ar-Rayah - Toleo 174

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu