Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Maridhiano Kati ya Ethiopia na Eritrea: Mpango wa Kikoloni wa Kuhifadhi Maslahi ya Warasilimali wa Kimagharibi

Na: Ali Nassoro Ali*

Katika kongamano mnamo 9 Julai 2018 jijini Asmara, Raisi wa Eritrea Isaias Afewerki na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed walitia saini “Tangazo la Pamoja la Amani na Urafiki”. Makubaliano hayo yaliyotiwa saini yaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

Kwanza, hali ya kivita imemalizika,

Pili, mataifa haya mawili yatasonga mbele yakiwa na ushirikiano wa karibu wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiusalama,

Tatu, mafungamano ya kibiashara, kiuchumi na kidiplomasia yatarudi tena,

Nne, uamuzi wa mipaka utatabikishwa na

Tano, amani ya eneo itapewa kipaumbele na mataifa yote mawili.

Makubaliano haya yanajiri baada ya miongo miwili (1998 – 2018) ya mvutano wa muda mrefu baina ya mataifa haya mawili. Mvutano wao ulichochewa na wakoloni kwani Ethiopia ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza na baadaye kugeuka na kuwa kibaraka wa Amerika. Uingereza ulichochea mvutano huu wa Eritrea kutaka kujitenga kutoka kwa Ethiopia na mnamo 1993; ilipewa uhuru wake rasmi na kujiunga na Umoja wa Mataifa lakini ikasalia kuwa hasimu mkuu wa Ethiopia. Amerika kwa upande mwengine ilijitolea kuhakikisha kuwa Eritrea iko katika maelewano mazuri na Ethiopia kwani ni mlango muhimu wa kuingilia nchi vibaraka nyenginezo zilizo jirani na Eritrea katika eneo la Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu.

Yanayoendelea kwa sasa yanajitokeza katika wakati muhimu zaidi wakati ambapo Amerika imejiingiza katika vita kamilifu vya kibiashara na China na Muungano wa Ulaya. Hivyo basi, Amerika inataka kutatua kadhia muhimu za bara la Afrika, kwa kujionesha kuwa mwenye mamlaka ya Kiulimwengu, na hatimaye kutulizia makini Vita vipya ya Kiuchumi vya karne ya 21. Amerika inatafuta:

Kwanza, kukarabati sura ya serikali ya Ethiopia iliyojaa unyanyasaji na hali mbaya za maisha ya raia wake. Kudandia juu ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn mnamo 15 Februari 2018 na kukabidhi hatamu za uongozi kwa Waziri Mkuu mpya Abiy Ahmed mnamo 2 Aprili 2018. Katika hotuba yake ya kupokea utawala, alidhihirishwa kama mwanamageuzi wa kisiasa na kuahidi kuimarisha umoja nchini Ethiopia na umoja miongoni mwa watu wa Ethiopia; kuifikia serikali ya Eritrea ili kutatua mzozo unaoendelea kwa sasa wa mpaka kati ya Eritrea na Ethiopia baada ya vita vya Eritrea na Ethiopia na pia kuufikia upinzani wa kisiasa ndani na nje ya Ethiopia. Raia waliridhika kwa kuwa matarajio yao yalinyanyuliwa na matokeo yake Abiy Ahmed alipokea shangwe za hali ya juu kutoka kwa raia wa Ethiopia yakiwemo makundi ya upinzani ndani pamoja na nje ya Ethiopia.

Pili, kupeana msaada wa kiuchumi kwa Ethiopia ili kumakinisha na kuzima maandamano yanayohusisha vijana kwa wingi ambayo takriban asilimia 50% ya idadi ya wakaazi wa Ethiopia wako chini ya umri wa miaka 18, ambapo yalilemaza serikali ya Ethiopia chini ya Waziri Mkuu aliyepita. Ethiopia kama nchi isiyo na mwambao ambayo kiasi kikubwa cha uchumi wake hutegemea usafirishaji bidhaa za ukulima ng’ambo ilihitaji kwa haraka makubaliano na Eritrea ili iweze kupata nafasi ya kutumia ufuo mpana wa Bahari Nyekundu kama mlango wa kuwafikia washirika wa kibiashara wa Kiulimwengu hususan makampuni yaliyoidhinishwa na Amerika.

Tatu, kupeana jukwaa la kieneo kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ili kushawishi kadhia za kieneo kwa maelekezo ya sera za Kiamerika kama vile:

a) Mipango ya kupambana na ugaidi – Ethiopia iko na jeshi kubwa na imara zaidi eneo hilo na limekuwa likipigana na al Shabaab tangu 2008. Kwa kuwepo na uhusiano mzuri kati ya Eritrea na Ethiopia kunatarajiwa kupanuliwa kwa mipango hii na kuongezwa tanzu zake ili kupangilia upya dori maalumu kwa wanachama wa eneo hilo; ikijumuisha Djibouti kwa kuwa mwenyeji wa kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Amerika barani Afrika na ambayo pia ni muhimu mno kwa kampeni ya Yemen ambayo Amerika inashirikiana na Saudi Arabia katika vita dhidi ya washirika wa Uingereza kutokana na kuchukua uongozi nchini Yemen.

b) Kupambana dhidi ya ushawishi wa China barani Afrika kama ilivyo thibitishwa mnamo Alhamisi 8 Machi 2018 na aliyekuwa Waziri wa Kigeni wa Amerika, Rex Tillerson, katika ziara yake ya kwanza barani Afrika, alisema kuwa nchi za Afrika zapaswa kuwa makini kutopoteza ubwana wao pindi zinapo chukua mikopo kutoka China. Tillerson pia alisema kwamba uwekezaji wa China “hauleti ajira ya kihakika eneo hili” na kukashifu jinsi Beijing ilivyounda mikopo kwa serikali za Afrika. Hivyo basi, yanayojiri sasa kati ya Ethiopia na Eritrea yatapelekea nchi mbili hizi kusimama kama jukwaa jengine la kunali maslahi ya Amerika kupitia kuziunganisha serikali vibaraka wa Amerika na Eritrea.

Yaliyo juu yanathibitisha kwamba Ethiopia na Eritrea zote ni serikali vibaraka zinazotumiwa kuendeleza njama za kikoloni barani Afrika kwa ajili ya manufaa ya mabwana zao wa Kimagharibi.  Ni chini ya Khilafah pekee ambapo maridhiano ya kihakika yatakapopatikana kwa ajili ya manufaa ya Afrika yote kwa jumla.

*Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

*Imeandikwa kwa ajili ya Gazeti la Ar-Rayah – Toleo 192

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu