Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimezindua
Kampeni na Kongamano la Kiulimwengu:
Changamoto za Familia na Suluhisho za Kiislamu

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kilizindua kampeni ya kiulimwengu kwa anwani, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” ambayo itamalizikia katika kongamano la kimataifa la wanawake mwishoni mwa Oktoba litakalo hudhuriwa na wazungumzaji kutoka pembe zote za dunia.

“Kiungo cha Familia” ndio jiwemsingi la mwanadamu; familia imara ndio kitovu cha mujtamaa imara, zisotingishika, na zenye mafanikio. Ni muhimu mno katika utoaji usaidizi wa kimwili, kihisia, na kimada na kuwepo kwa hali nzuri ya wanachama wake wote na kuhakikisha uchungaji thabiti na ulezi mwema wa watoto. Lakini, leo kuna mgogoro unaoathiri utulivu na umoja wa maisha ya ndoa na familia katika jamii kote duniani, ikiwemo ndani ya biladi za Kiislamu.

Katika kampeni na kongamano hili muhimu, tutaangazia hatari za mabadiliko ya sura ya muundo wa familia katika ulimwengu wa leo. Pamoja na kutambulisha vigezo vikuu vinvyodhuru taasisi ya ndoa na utulivu wa maisha ya ndoa, ikiwemo dori ya vyombo vya habari na serikali katika kukoleza mgogoro huu. Tutafichua ajenda za kitaifa na kimataifa za kutia usekula katika familia za Kiislamu na sheria za kijamii ili kuwaeka mbali zaidi Waislamu kutokana na Dini yao.  Mwishoni, tutaangazia nidhamu ya kijamii ya Kiislamu na kuonyesha jinsi mtazamo wake wa kipekee katika kupangilia mahusiano ya kijinsia, kwa misingi yake sahihi, maadili na sheria, ukiwemo ufafanuzi wake wazi wa majukumu ya wanaume na wanawake ndani ya maisha ya familia, unavyo weza kulinda ndoa, kukuza utulivu na maelewano ndani ya maisha ya ndoa, kunyanyua cheo cha mama katika hadhi kuu inachostahiki na kuasisi na kuhifadhi viungo vya familia imara zilizo na umoja. Kampeni na kongamano hili pia litafafanua dori muhimu mno ya usimamizi wa Kiislamu chini ya dola ya Khilafah kwa msingi wa Utume katika kukuza, kupigia debe na kulinda viungo imara vya ndoa na familia ili kuonyesha namna gani Uislamu kihakika ndio ngome ya familia!   

Jumatatu, 23 Muharram 1440 H - 03 Oktoba 2018 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Februari 2020 15:03

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu